Uteuzi wa Jaji Werema kuwa Mwanasheria Mkuu uhojiwe Mahakamani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa Jaji Werema kuwa Mwanasheria Mkuu uhojiwe Mahakamani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Katika hali inayothibitisha ukiukwaji na uporomokaji wa maadili katika sekta ya umma ni uteuzi wa Jaji Werema uliofanywa na JK kuwa Mwanasheria Mkuu..........Kisa ni kugonganisha mihimili mitatu ya dola.........


  Katika hukumu iliyotolewa na Majaji 3 nchini Kenya kwenye kesi ya Harun Mwau dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Kenya na Mamlaka ya Kuzuia Rushwa nchini Kenya iliamuliwa ya kuwa ni makosa kwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa Bw. Aaron Ringera au Mwanahaki yeyote kuwa Mkurugenzi Mkuu wa K.A.C.C.- yaani Taasisi ya kuzuia rushwa......................

  Majaji hao kwenye uamuzi wao waliona kuna mgongano mkubwa wa kikatiba kwa Jaji ambaye jamii inamtarajia kuwa ni mtoa haki kuwa upande wa kuwashitaki raia na hivyo hali hiyo ingepunguza imani ya raia kama Mahakama zingeliwatendea haki bila ya upendeleo wakati mmoja wao ni sehemu ya uendesha mashitaka......

  Kwa kauli moja walitengua uteuzi wa Jaji Ringera kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia rushwa ya Kenya......

  Nasi, JK katuingiza kwenye mgogoro wa kikatiba kwa kumteua Jaji Werema kuwa Mwanasheria Mkuu na kusababisha mikanganyiko mikubwa ya kikatiba..........

  Kama Jaji, raia tunamtegemea Jaji Werema awe upande wa kutoa haki na kama Mwanasheria Mkuu tunamtegemea awe mdai haki................kazi mbili zenye migongano ya masilahi na ni kazi ambazo haziwezi kufanywa na mtu mmoja....................

  Ni vigumu kwa raia wa kawaida kuona kuwa hakuna upendeleo pale ambapo Jaji wa Mahakama kuu anapokuwa ni sehemu ya kudai haki na dhana ya upendeleo ipo wazi kabisa na uteuzi wa Jaji Werema ni dhahiri unakinzana na katiba.................

  Kwenye kesi inayofanana na hiyo hapa nchini iliyohusu mawakili kuwa wabunge, Mahakama kuu ilisema katiba inakataza mwingiliano wa mihimili mitatu ya dola lakini Bunge halijatunga sheria za kukataza ushiriki wa mtu mmoja mmoja kuwepo kwenye zaidi ya muhimili mmoja na hivyo mahakama mikono yake imefungwa..............How pathetic....

  Hoja hizi ni dhaifu kwa sababu kazi ya Mahakama Kuu ni kutafsiri sheria na kama sheria hazipo bado wanatakiwa kutoa msimamo wa kisheria unaopaswa kufuatwa...............

  Jingine uamuzi huu siyo wa mwisho kwa sababu Mahakama ya Rufaa haikupewa nafasi ya kutoa tafsiri sahihi ya kisheria.......................kuna uhaja wa uteuzi wa Jaji Werema kuhojiwa Mahakama Kuu na kama majibu ya awali yatarudiwa basi swala hili likakatiwa rufaa mahakama ya juu kabisa ili tuwe na tafsiri sahihi ya kisheria kuhusiana na haya matumizi mabaya ya madaraka ambayo JK amekuwa akiyafanya kwa kuikandia katiba...............

  Jingine hii ni hoja nyingine ya kuwa na Katiba mpya kuondoa migongano ya mihimili mitatu ya dola inayosababishwa na watendaji kwa ubinafsi wao................haina maana kukataza mwingiliano wa mihimili tajwa lakini tukasubiri sheria zitungwe kukataza watu binafsi kutoleta hyo migongano.................huu ni upuuzi wa wazi wa kuibeza katiba kwa kupooza malengo yake kwa kunyima sheria kuundwa.............................


  Ushauri wangu ni kuwa uteuzi wa Jaji Werema kuwa Mwanasheria Mkuu ni ukiukwaji mkubwa wa katiba yetu inayokataza mwingiliano wa mihimili mitatu ya dola na kuna uhaja wa kuangalia uwezekano wa kuiomba Mahakama kuu na hata ikibidi Mahakama ya Rufaa kutoa tafsiri sahihi ya kisheria.........................
   
 2. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mzalendo Ruta,

  Je umeisoma vizuri katiba ya Tanzania? Au unatoa maoni kwa kusikiliza mawazo ya watu tu? Tanzania haina mihimili mitatu isiyoingiliana. Kwa umbali Tanzania ina mihimili miwili na nusu. Hii ni kwa sababu mawaziri ambao ni watendaji wa wizara ni wabunge.

  Vilevile hata kwenye nchi zenye mihimili mitatu, mwanasheria Mkuu hayupo kwenye mhimili wa mahakama. Yupo katika mhimili wa serikali. Hivyo maamuzi yake ya kiofisi, ni maamuzi ya kisheria ya serikali.

  Kwa mfano mtu anapofungua kesi na kuishtaki serikali. Ni mwanasheria mkuu au ofisi yake yenye kazi ya kuitetea serikali. Kwa mfano wakati Mtikila alipofungua kesi ya mgombea huru, ofisi ya mwanasheria ilikuwa ni wakili wa serikali mahakamani. Mtikila alikuwa ni mlalamikaji na vilevile kulikuwa na majaji wa mahakama. Na Mtikila aliposhinda kesi, kwa niaba ya serikali ofisi ya Mwanasheria mkuu ilikataa rufaa.

  Na katika nchi nyingine hata kipindi fulani wakati wa Nyerere, Mwanasheria Mkuu alikuwa ni cabinet member. Hivyo basi maneno ya mwanasheria mkuu yanaweza kuwa na maana tatu. Kwanza kama raia anayo mawazo yake binafsi. Pili maneno yake yanaweza kutoa msimamo wa serikali kuhusiana na masuala ya kisheria. Tatu, maneno yake yanaweza kutumika kama litmus test ya kuangalia je public ina maoni gani.
   
 3. U

  Uwezo Tunao JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 6,947
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Pole yenu, huyo Marehemu samahani WEREMA wala si Mwanasheria Mkuu wangu wala simjui.

  Mwanasheria Mkuu wangu ni yuleee aliyeteuliwa na Dr Shein kule Zanzibar - Mhe Makungu.

  Akili tulivu, uteuzi tulivu.
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Tofautisha ...............what the is................and what the law should be..............................and only the courts cannot sort that out by issuing proper interpretations.........................................

  Jaji kuwa Mwanasheria Mkuu ni ukiukwaji wa mgawanyiko wa majukumu kati ya mihimili mitatu........yapo matatizo katika katiba iliyopo lakini mengine yanakuzwa na kubebana hata kwenye mahakama zetu..................
   
 5. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,018
  Likes Received: 417,508
  Trophy Points: 280
  Tatizo anapokuwa ni Jaji vilevile ........ndiyo utata unapoanzia.............................
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Jan 1, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wewe Ruta sijui ni uelewa wako mdogo ndo maana huwa unakurupukaga tu kwemye thread zako nyingi, Nashauri uwe unatutumia habari tu za magazetini kama unavyofanyaga siku zote na si ku-comment katika vitu ambavyo huna uhakika navyo.
  Ujaji ni professional sio cheo. Ni sawa na wanavyosema daktari (MD) au Engineer au mwl kama nyerere. Pia kuhusu uteuzi rudia kuisoma katiba inasemaje? Usikurupuke tu ukizingatia wewe unajiita mchambuzi (sijui wa hewa) based in Arusha. Swallow it.
   
Loading...