Uteuzi wa Jaji Kiongozi Kufanyika Mapema Mwezi Ujao

NEVIOT

Member
Nov 26, 2013
29
8
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Tanzania FAKIHI JUNDU [Miaka 65] anatarajiwa kustaafu mapema mwezi July 2014. JUNDU amedumu katika nafasi hiyo tangu mwaka 2009.

Habari nilizozipata kutoka kwa jamaa fulani ni kwamba Rais atamteua Mwanamama MWANAISHA ATHUMANI KWARIKO [Jaji Mfawidhi - Songea] kuwa Jaji Kiongozi.

Endapo tetesi hizi ni za kweli, inatarajiwa Jaji huyo kuwa mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo.

Bado nafatilia kujua wasifu wake na endapo ana sifa zinazofaa kuwa Jaji Kiongozi. Baadhi ya watu nimesikia wakiwa na mawazo tofauti kwamba uteuzi huo huenda usifae na kukubalika kwa majaji wakongwe katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Ikumbukwe kwamba kwa mujibu wa Katiba ya mwaka 1977, Jaji Kiongozi ndio Mkuu wa Mahakama Kuu na ni msaidizi namba moja wa Jaji Mkuu katika kuongoza Judiciary.
 
Sijawahi ona faida mahususi ama mabadiliko ya maana yaloletwa na hizi teuzi, zaidi ni bra bra zile zile za miaka nenda rudi!
 
Joyce Banda amenifanya ni tafakuri upya kuhusu wanawake na madaraka makubwa .....kwani bi mkubwa mkora pale mjengoni nilishamfutilia mbali......
 
hakuna jipya uteuzi hata angechaguliwa nani propaganda tu,mahakama zinawafunga wanyonge na kuwabeba matajiri.utumbo tu
 
Back
Top Bottom