mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,771
- 7,138
Kwa kweli nimesikitishwa na rais Kikwete kumteua Prof benno Ndullu kuwa gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania baada ya kumfukuza kazi Bwana Balali aliyekuwa Gavana. Hii ni kutokana na ripoti ya ukaguzi iliyofanywa na wakaguzi wa kampuni ya Ernst & Young ambayo imeonyesha au imegundua ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma ambao ni wa kihistoria kuwahi kufanyika hapa Tanzania kwa kipindi kifupi hivyo (miezi 2 hadi 3) mwaka 2005 kuelekea kwenye uchaguzi mkuu. Fedha iliyochukuliwa na hawa majizi ni shilingi billioni 133.015!!!
Sasa nirudi kwenye kichwa cha habari. Nimesikitishwa na uteuzi wa Prof Benno Ndullu kwa sababu na yeye ni mtuhumiwa wa upotevu wa hizo fedha za umma. Wakati hizo fedha zinachukuliwa alikuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu na hakufanya lolote kuzuia. Mtu mwenye akili nzuri hawezi kuamini kwamba wakati wizi wa mabillioni hayo ya shilingi yanachukuliwa na hao wezi hakufahamu chochote kabisa. Na kama hakufahamu chochote basi hafai kuwa Gavana, kwa sababu yeye akiwa kama mtu wa pili kwa madaraka Benki Kuu atakuwa alikuwa anahudhuria vikao mbalimbali vya benki au bodi ya wakurugenzi ambavyo vilitoa maamuzi mbalimbali kuhusu uendeshaji wa benki hiyo.
Wakati Katibu Kiongozi Bwana Luhanjo anaongea na waandishi wa habai juzi kuwajulisha maamuzi ya rais kuhusiana na ripoti ya ukaguzi wa Benki Kuu aliema kwamba rais ameagiza bodi ya wakurugenzi ya Benku Kuu ikutane haraka sana ijadili hiyo ripoti na kuwachukulia hatua wote walitajwa kuhusika na u\wizi wa hayo mabilioni. Hii inashangaza sana. Itakuwaje bodi hiyo hiyo iliyoshindwa kabisa kusimamia uendeshaji wa Benki Kuu ambako kumesababisha wizi huo leo hii inaagizwa iwachukulie hatua watuhumiwa? Tuna hakika kwamba baadhi ya wakurugenzi wa Bodi siyo watuhumiwa katika wizi huo? Mie nadhani wengine watakuwa, maana itakuwa ni ajabu huo wizi wa mabilioni ukafahamika na watu wa nje ya Benki Kuu na wasimamizi (yaani wakurugenzi)wa benki wasijue.
Upo uwezekano mkubwa kwamba wamiliki wa hayo makampuni 22 yaliyoiba hizo pesa zetu Prof Benno na wajumbw wa bodi ya wakurugenzi wanawafahamu vizuri na labda wengine ni rafiki au ndugu zao. Ingetakiwa Prof Benno naye afukuzwe kazi mara moja kwa vile ndiye alikuwa msaidizi na mshauri mkuu wa Gavana. Hivyo kumuacha yeye bila kumchukulia hatua yeyote na badala yake kumuongezea madaraka naona kama kitendawili. Hivyo hivyo bodi ya wakurugenzi ingetakiwa kuvunjwa iundwe nyingine mpya. Nadhani kuna kitu hapa kimefichwa au kinalindwa ili sisi wananchi tusifahamu. Kuna wakubwa wanalidwa hapa? Mbona serikali haikusema maofisa wengine wa ngazi za chini ya ugavana waliotajwa kwenye ripoti watachukuliwa hatua gani na ni akina nani? Sioni mantiki ya wale waliotajwa kwenye ripoti ya ukaguzi iliyotolewa na Ernst & Young kuendelea kubakizwa kazini badala ya kuwa nje wakisuburi hatua za kisheria au kinidhamu.
Wakati wa utawala wa awamu ya kwanza mtuhumiwa ye yote yule alikuwa anasimamishwa kazi, uchunguzi unafanyika, maamuzi
yanafanyika kulingana na matokeo ya uchunguzi halafu mtuhumiwa anajulishwa hatua inayofuata. Utaratibu huu ulifuatwa ili kuzuia mtuhumiwa asivuruge uchunguzi wa tuhuma dhidi yake. Katika hii awamu ya nne ya utawala naona mtuhumiwa anaendelea kubaki ofisini ambapo anaweza kuhujumu zaidi uchunguzi na matokeo yake ikaonekana ni majungu. Huu utaratibu haujengi ila unadhoofisha na unachelewesha haki kutendeka. Utawala huu wa Kikwete pia unakuwa slow kufuatilia tuhuma zinazotolewa na watu binafsi, taasisi na hata vyombo vya habari. Matokeo yake ni hasara kubwa kwa taifa.
Kwa kumalizia nasema hivi: Rais amfukuze Prof Benno kazi kwa kusaidia au kuhusika moja kwa moja au kwa kutofanya lolote kuzuia wizi wa shilingi billioni 133.015. Na pia bodi ya wakurugenzi ya sasa ivunjwe na wajumbe wapya wateuliwe. Rais awasimamishe kazi wale wote waliotajwa kwenye hiyo ripoti ya ukaguzi wakati hatma yao inaandaliwa. Na hii isichukue tena muda mrefu, la sivyo itaonekana Dr Balali katolewa kafara tu kuziba watu au vyombo vya habari midomo. Aidha rais amuachishe kazi waziri wake wa fedha Zakia Meghji, kwa vile haonekani kutenda kazi yake kiadilifu.
Source: Uteuzi wa Gavana mpya wa Benki Kuu ya Tanzania