nygax
JF-Expert Member
- Jun 4, 2017
- 1,371
- 865
Amani iwe kwenu,
Nadhani wengi wetu tunakumbuka namna ambavyo Dr. Wilbroad Slaa alivyoleta mshituko mkubwa katika ulimwengu wa siasa, baada ya kutangaza rasmi kwamba anastaafu siasa.
Maamuzi haya aliyafanya baada ya yeye mwenyewe kusema hakuridhishwa na mchakato mzima wa kumpokea na hatimae kumpitisha mwanasiasa `machachari' Edward Lowassa kutoka CCM, aipeperushe bendela ya CHADEMA kwa mwavuli wa UKAWA, katika uchaguzi mkuu wa 2015.
Maamuzi haya yalimfanya apokee kila aina ya matusi na kejeli, huku wengine wakimbatiza jina `Dr. mihogo', wengine wakamwita msaliti na wengine wakimtukania hata familia yake.
Baada ya taarifa za uteuzi wa Dr. Slaa kuenea katika mitandao ya kijamii, kunajambo ambalo si la kawaida limeibuka hasa ktk upande wa upinzani,
wanalalamikia mbinu za Mh. Rais kuwateuwa wapinzani katika nyadhifa mbalimbali, akiwemo slaa, kwamba ni mbinu za kuuwa ama kudhoofisha upinzani.
Swali fikirishi: Wapinzani bado walimhesabu Slaa kama mpinzani? Ama Mh. rais amekosea kumchukua Dr. Slaa kama assert?
Nawasilisha.