Uchaguzi 2020 Uteuzi wa Charles Kimei ni dhahiri CCM wanataka Jimbo la Mbatia. Na iwe kifo cha dhana ya CCM B

Kwitululu

Member
Mar 30, 2020
41
125
Watu wengi hasa Wafuasi wa CHADEMA tangu Rais Magufuli amsifie Mhe Mbatia hadharani walianza kudhani ni msaliti wa Magruzi, na kuita chama cha NCCR Mageuzi kuwa ni CCM B.

Wakimaanisha NCCR Mageuzi ni mpango wa CCM. Wengi wakaongeza porojo eti NCCR Mageuzi wameahidiwa majimbo 20 mara 50 ambayo watapewa wepesi wa kushinda.

Cha ajabu Jimbo la Vunjo anakowakilisha mwenyekiti wa NCCR Mageuzi. CCM wameteua mgombea mwenye profile kubwa na mwenyekuleta ushindani mkubwa zaidi kwa Mhe Mbatia.

Binafsi hili limenipa udhahidi zaidi kuwa ile mambo ya CCMB mara majimbo 50 ni uchafu uliopikwa mitaa ya Ufipa kuwaondolea NCCR Mageuzi political legitimacy ya kuwa upinzani nchini.

CHADEMA na wafuasi wao maarufu kwa jina la Nyumbu wa mjini wamekua na tabia ya kuchafua kila chama cha upinzani kinachojaribu kuwapa upinzani katika upande wa upinzani nchini.

Mwaka 2015 walikiita chama cha ACT-WAZALENDO NI CCM B.

Mwaka 2011 baada ya kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa huko Zanzibar. Nyumbu alikiita chama cha wananchi CUF kuwa ni CCM B.
 

Automata

JF-Expert Member
Mar 3, 2015
2,636
2,000
CCM ipambane kweli kweli wampeleke bungeni mtu huyu, anafaa kuwa naibu waziri wa fedha, akasaidiane na Dr. Mpango, ama waziri kamili katika wizara zinazo husiana na uwekezaji, biashara, masoko na mambo ya namna hiyo
 

NewOrder

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
1,325
2,000
Yaani unamsifia mteuliwa Dr. Kimei kuwa na profile kubwa lakini unalaumu mawazo ya wafuasi wa Chadema kuhusu habari za CCM B.

Ninadhani mambo haya yalihitaji masa mbili tofauti. Kwa sasa sifia uteuzi wa Dr. Kimei na achana na ujinga na lawama dhidi ya Chadema ambao wameweka mgombea sawa sawa na NCCR Mageuzi.

Vijana wa leo mna tatizo na kukosa maarifa! Huna uwezo hata wa kuchambua na kujipanga kabla hujasema kitu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom