Uteuzi wa CEO mpya wa Air Tanzania

Mfumo haudumazi maana una kanuni na bila kanuni Kampuni haiendi mwisho wa siku mtaishia kutumbuana... so mifumo ya makampuni nyingi ni mizuri tatizo ni uaminifu wa wafanayakazi na management pia... kuna watu huwezi wadhania kama wanaiba kumbe ni vibaka hatari makazini bora vibaka wa nje

Kwa hiyo hicho unachoita mfumo si suluhisho, right? Maana unasema mifumo ipo mizuri lakini lakini bado wafanyakazi si waaminifu. So, what is mfumo good for?
 
Isiingiliwe na inahitaji kupata mtu makini wa kusimamia hilo shirika ambaye hata Pombe mwenyewe hawezi mburuza huyo mtu
Keshapatikana tayari. Mkerewe wa Nansio, Engineer wa Mitambo ya kuongoza ndege. Master Degree.
 
Nasikia tayari serikali imetoa tangazo la kumuajiri CEO mpya wa air Tanzania, serikali iwe makini sana kumuajiri CEO, huyu ndiye anayeandaa dira na mwelekeo wa kampuni,

Anashawishi na anaongoza shirika, naomba serikali imuajiri mtu wa nje kama wazungu wazoefu waliofanya kazi hizi kwa makampuni makubwa na yamekuwa kwa kasi leo hii tunayaona yakiwa na mafanikio makubwa.

ATCL imeshabadilisha ma CEO sijui mara ngapi wote hakuna ambaye utendaji kazi wake umeonekana kuifufua ATCL kazi ilikuwa kuajiri tu huku wakijua hakuna kazi wafanyakazi hao wanazozifanya.

JPM liangalie swala hili utawalaumu watendaji kazi wako bure kumbe mlimchagua mtu ambaye sio sahihi kuisimamia ATCL. ukimchukua CEO mzungu mwenye uwezo mkubwa na umpe pesa ATCL itafukuzana na KQ (Kenya Airways) hapa sio pa kuchezea eti CEO lazima awe mtanzania, na akiwekwa mtanzania nawapa miezi 6 tutampima nitarudi tena hapa kuwapa jibu.

watanzania sio kwamba hatuna uwezo hapana ila tuna katabia flani hivi ndio maana wengi tunapata taabu sana kufanya kazi kwenye mashirika ya kimataifa wengine tunakimbia wengine tuna survive na wengine tunakomaa,

Hapa anatakiwa mzungu ambaye hawezi kupoke vi MEMO kutoka kwa nani eti katibu mkuu wa chama ameandika kimemo kuwa mwanaye apewe nafasi kwenye ndege huku hamna hela na nauli, kingine JPM ATCL isiingiliwe na siasa iache iwe huru kabisa ijiendeshe na uongozi wake ujitegemee, vinginevyo tutachekwa sana tu.

Awe CEO anayelipwa kutokana na uzalishaji, ambaye ataona uchungu kuajili watu wengi 'redundant' na kuwa'overpay' wasiohusika na uzalishaji halisi!
 
Back
Top Bottom