Uteuzi wa baraza la mawaziri, na kumpitisha Chenge kugombea uspika kasha no 1. ya ccm

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Katika awamu hii ya uongozi ccm kupitia maamuzi mbalimbali ya vikao vyake na utendaji wa raisi Kikwete na serikali yake inaweza kujikuta inafanya "blander" nyingi katika kujaribu kukabliana na changamoto zinazoikabili hasa kwa kuwa Kikwete amejikuta ametoa ahadi nyingi alipokuwa akijaribu kumpiku mshindani wake mkuu Dr. Slaa kipindi cha kampeni.

Blander ya kwanza ninayoiona ikiitishia ccm ni kumpitisha Chenge kuwa mgombea uspika wa bunge la Jamhuri ya Muungano. Nasema hii ni blander, tena ni kashfa kwa sababu Chenge ni mmoja wa watu ambao public image yao imechafuka vibaya kwa ajili ya kashfa yake ya "vijisenti" hivyo kumnyima "moral authority" ya kuongoza chombo chenye hadhi ya bunge. Chenge na ccm isijidanganye kuwa kuchaguliwa kuwa mbunge kwa Chenge ni ushahidi wa imani ya watanzania kwake. Jimbo alilogombea wananchi wake hawako aware na mambo mengi ya ndani ya nchi. Wao ni "victims" wa "engeneered ignorance." Chenge angegombea jimbo kama Ubungo sidhani kama angeambulia kura 200.

CCM ikimpitisha Chenge itakuwa imewaambia watanzania wote wanaotumia ubongo wao sawasawa kuwa kimeamua kuuenzi ufisadi rasmi bungeni na kuling'oa meno bunge lisiweze kuwang'ata WALA NCHI. Itakuwa imeweka kwa makusudi pazia mbele ya Watanzania ili wasiweze kuona kupitia wabunge wao nini kinachotokea serikalini. Itakuwa imetimiza azma yake ya kulipiza kisasi kwa wabunge wake (wa ccm) waliosimama kidete katika ile kashfa ya Richmond na nyinginezo baada ya kushindwa kuwaengua.

Blander ya pili inafanana na ya kwanza. Hii inamhusu Kikwete mwenyewe katika kuteua baraza la mawaziri. Kwanza Kikwete atahitaji timu yenye sio tu uwezo wa ku-deliver, bali pia na utashi wa kisiasa kutekeleza ilani ya chama na ahadi zake, watu ambao hana. Wakati huo huo anao ushawishi wa kugawa nafasi hizo kwa kulipa fadhila za waliomsaidia kuingia ikulu kama alivyofanya kipindi kilichopita, bila kusahau shinikizo la maswahiba wake wa jadi kama Lowasa, Rostam, to mention a few. Sitaki kutaja ajenda zake za siri za kuingiza nchi kwenye OIC, na kuwaandaa watakaomlinda atakapokuwa ametoka kazini, kuwapatia kazi wale wa damu yake (Ridhiwani?) na ya uzao wa mentors wake (Mwinyi) zitakazomlazimu kuweka baadhi ya watu kwa makusudi hayo.

Hayo yote yanamweka njia panda, hata imwie vigumu hasa kulingana na hulka yake kuteua baraza effective. Uwezekano mkubwa ni kujikuta ana genge la mawaziri watakaoifanya serikali yake kushindwa kutekeleza ahadi zake ambazo baadhi yake ni karibu na "utopia." Blander mbili hizi ndio nadhani za kwanza na zitakazo-trigger nyingine nyingi. Yangu macho.
 
umenena kweli mkuu hata nimeliona hilo harafu ukizingati kuwa kulipa ni jambo la hatari sana kwa nchi yetu,
kwanza tuende mbele turudi nyuma utakumbuka kuwa naye ni mmoja wa mafisadi walio chini ya meza,
lakini wa kuwawajibisha angekuwa ni mtu asiye ndani ya ccm kwa maana moja ya heshima ndani ya ccm ni kulinda
uovu wa mtu (mwenyekiti) wao pale anapoonekana ana njia moja ama mbili ziendazo kushoto kwa maadili ya uongozi
wa heshima, kipindi kilichopita tumeyashuhudia mengi toka ndani ya ccm wakitaka kujaribu kuzima moto wa Richmond
kwa madai ya kuilinda serikali tena vikao vikafanyika chini yake kikwete
 
Hayo yote yanamweka njia panda, hata imwie vigumu hasa kulingana na hulka yake kuteua baraza effective. Uwezekano mkubwa ni kujikuta ana genge la mawaziri watakaoifanya serikali yake kushindwa kutekeleza ahadi zake ambazo baadhi yake ni karibu na "utopia." Blander mbili hizi ndio nadhani za kwanza na zitakazo-trigger nyingine nyingi. Yangu macho.

Ni lini JK amewahi kuteua Baraza effective? Kila siku watu wake wanamtetea kwamba ana wasaidizi wabovu kwenye wizara na hata Idara za serikali. Je, mtu makini anaweza kuteua wasaidizi wabovu? Mtu mwenye hulka ya kuteua baraza effective angeweza kuwa anasukumia lawama kwa wasaidizi wake kwamba ni wabovu?
 
Asante Keil ku-highlight hiyo statement. Nimekosea tu kuiweka kwa namna ambayo kwa haraka inaonekana kama tungo tata. Lakini maana yangu siyo kusema ana hulka ya kuteua baraza effective hata kidogo. Hana hulka hiyo, na hata kama angeshateua wakati wowote hiyo isingeitwa hulka. Ukiingalia vizuri hiyo statement utaona ina maana kuwa kulingana na changamoto hizo zinazomkabili, yuko njia panda, na kulingana na hulka yake hataweza kuteua baraza effective. In other words, hulka yake (ya kutaka kuwapendeza maswahiba) haitamruhusu kushinda hizo changamoto na hivyo hataweza kuteua baraza effective. Context ya maelezo yangu inaonesha vizuri maana yangu ni nini. Thank you Keil.
 
Back
Top Bottom