Uteuzi wa AG Werema ni BATILI au halali? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uteuzi wa AG Werema ni BATILI au halali?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAMMAMIA, Jul 6, 2012.

 1. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayotumika sasa, kifungu kifuatacho kinasema:

  Na kwa mujibu wa Katiba hiyo, kifungu kifuatacho kinasema:
  Lakini kwa mujibu wa Katiba hiyo hiyo katika kifungu hiki:

  Kutokana na kifungu hiki cha mwisho, Raisi anapewa uwezo wa kutengua
  lile sharti la kuwa na sifa maalum kwa muda usiopungua miaka mitano na kumteua mtu huyo kuwa Jaji wa Mahakama Kuu lakini sio kutengua sifa ya kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

  Kwa hivyo, kwa mujibu wa Kifungu 113A cha Katiba, kwa maoni yangu, uteuzi wa AG Werema si halali kwa sababu kwenye CV yake Mheshimiwa huyu amejithibitisha mwenyewe kuwa ni mwanachama wa chama cha siasa, yaani CCM.

  Wenzetu mnaojua sheria, naomba mtusaidie zaidi kwa hili.
   
 2. JamboJema

  JamboJema JF-Expert Member

  #2
  Jul 6, 2012
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 1,148
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Hili nalo neno. Kanunni za bunge zinasemaje kuhusu mtu baki kupeleka hoja binafsi bungeni? Nadhani ni muda sasa wananchi tupate fursa ya kuhoji mambo mbalimbali moja kwa moja bungeni.
   
 3. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #3
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Kuna Judge moja albino kule Kenya juzi juzi tu katengua uteuzi wa 47 county commissioners amesema taratibu hazikufuatwa.
  And the government has appealed against the court ruling.

  lakini hapa kwetu hakuna judge mwenye ubavu huo
   
 4. v

  vngenge JF-Expert Member

  #4
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 366
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Watasema ilikosewa co mwanachama
   
 5. Lastname

  Lastname JF-Expert Member

  #5
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 925
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ni la kufanyia kazi werema hana uwezo
   
 6. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #6
  Jul 6, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Katika tafsiri ya kisheria,uteuzi wa Jaji Werema kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ni halali.Kwanza,Werema si Jaji tena(limebaki jina tu).Pili,Werema alikuwa na sifa za kuwa Jaji hivyo kuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu.

  Tatu, ibara zilizotajwa zazungumzia mambo mawili tofauti:uteuzi wa Jaji na ule uteuzi wa Mwanasheria Mkuu.Ibara hizo zikisomwa vyema,hazikatazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuwa na chama.

  Swali linalobaki labda ni hili: Werema ana uwezo wa kuwa na cheo alichonacho? Jibu langu ni hapana.Aliteuliwa kwa kuwa alikuwa Mamluki tangu akiwa Jaji Mahakama Kuu.Wapo wengi tu wanaomzidi.Ni kichwa maji...
   
 7. M

  Msajili Senior Member

  #7
  Jul 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 117
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hoja imekaa kisiasa na kikereketwa zaidi
   
 8. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #8
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Maelezo yako yananishawishi niamini kuwa uko sahihi, ndio maana nikawataka wanaojua hizi sheria watueleze.

  Inawezekana, kwani Tanzania bila ya ukereketwa haiwezekani.
   
 9. Bitabo

  Bitabo JF-Expert Member

  #9
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 27, 2011
  Messages: 1,896
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
  Mkuu hapo kwenye wekundu wakina Shaymaar na Under the same sun watakushukia?
   
 10. f

  fikirikwanza JF-Expert Member

  #10
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 5,935
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Mmmmmmmmmmmmmhhhhhh, sijui kama kuna mtu serikalini wakukusiliza hoja yako hii. Waliompotosha watang'ang'ania hakuna tatizo.
   
 11. Kapo Jr

  Kapo Jr JF-Expert Member

  #11
  Jul 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 935
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 60
  Sasa anasubiri nn kujiuzuru,wanasheria tusaidieni huu nao udhaifu wa jambazi kuu
   
Loading...