hapa hatu fanyi mashindano ya waislamu wala ukristo, na haina haja ya kutia chumvi kwenye kidonda, tujaribu kuweka muelekeo wakurekebishana , hasa katika suala kama hili la dini, na ukabila. na suggestion ya mtoa mada sio mbaya saana, au tuseme amekosea jinsi alivyo iwakilisha, lakini kuna point kama hizi zifuatazo kitaaluma lakini, kwamba unapochagua watu wa ssehemu mbali mbali , dini mbali mbali kuna saidia kupata muono wa watu wengine juu ya kitu fulani. eg ukimchagua muislamu wa rifiji, si pia utapata maono ya watu wa rufiji, na hata maono ya ndugu zetu waislamu juu ya sayansi, pamoja na ujuzi wa muhusika katika hiyo sayansi.kwa hiyo hapa utapata vitu vitatu kwa pamoja. hata ukachanganya na muarusha/meru/maasai utapata pia experience ya watu wa huko, tunajua na tunaelewa kwamba ni vigumu katika kila jambo kuwa fair kama tunavyo penda lakini kila jambo likiwa na uwigo mpana linakuwa na manufaa
Ama kwa hakika JF ni kielelezo cha mfubau wa vichwa vya waTz..This shows exactly why we are so backwards...
Umeambiwa waziri ameunda timu itakayochochea nyanja za kisayansi..hili ni jambo la manufaa ukiliangalia hata kwa micro au macroscopic level: Lakini hebu tazama pumba ambazo zimeshavurumishwa:
1. Udini
2. Ukanda
3. Ukabila
4. Kudhani kuwa walioteuliwa wamepewa ULAJI..
5. n.k.
Kaazi kwelikweli..
...ukiwa unafikiria kitu katika minajili ya ukabila jua wewe ndio mkabila namba moja!!!!
ndugu administrator naomba huyu jamaa ashughulikiwe......
Tanzanianjema
Prof Nchimbi-Msolla of SUA is a brilliant plant breeder, married to Prof Peter Msolla's bother (the football coach, Mshindo Msolla). I just can't understand how this is related to IT&C. May be terms of reference (ToR) for the task of the committee include biotechnology (which is her area of expertise). Otherwise this might be another Bongo Dar as well!!
Nimependa ulivyoonyesha uzuri na manufaa ya diversity.Mchanganyiko mara zote huleta faida kubwa.Ndiyo maana nchi za wenzetu hutilia mkazo sana hili jambo.America wana mpaka Diversity Lottery ili kualika vipaji kutoka mataifa mengine kwa vile wanajua maana yake.Huku kwetu tutaishia kubaguana kwa misingi ya udini, ukabila, jinsia,nk na tutabaki mikia siku zote.
Nafahamu taaluma za Prof. Luhanga, Dr. Mwamila na Miss. Munyagi, wote ni wahandisi. Hao wengine pia either ni wahandisi au wamesoma sayansi, sina uhakika na wengine. Maybe hapa kigezo ni kuwa msomi katika nyanja hizo, na hata jina la hiyo kamati ni Kamati ya ushauri katika masuala ya Teknolojia na Mawasiliano. Sasa kama wasomi wa makabila au kanda nyingine labda wengi ni wa Arts au something else, huoni probability ya kupatikana mtu wa huko pia inashuka?
NImefurahishwa sana na namna ulivyoandika
Mwalimu alisema, "Hatumchagui mtu kwa kabila lake wala dini yake".
Mi nadhani uwezo wao umezingatiwa zaidi kuliko kitu kingine chochote.
Tume/Kamati zikiundwa kwa kubalance dini, makabila n.k bila kujali utaalam zaidi hatutafika. Tusubiri ili tuwapime kwa kazi yao.
Ndugu zako wanadai WOTE NI WAKRISTO, JE NA WEWE UNASEMAJE?
Tanzania hatuna tatiuzo la udini...
wewe kama wamekunyima uteuzi, usilete hasira zako hapa, usijemalizia hasira zako hapa ukatufanya sisi wanaJF tuungane na wewe kumbe wewe una vita nao. jamani, huyu jamaa hana point. hii kitu ingeondolewa kabisa. ulitaka wakuchague wewe na wamekutosa kwasababu hauna sifa hizo, sasa unalilia nini? hivi kuna udini unaweza kuongelewa hapa tz kweli? kama tukianza hivyo mbona mawaziri wengi tu wangebadilishwa kwasababu mkuu wa nchi kawapendelea sana watu wa dini fulani. lakini sisi tunaojiamini hilo halitutii shaka, kwasababu elimu tunayo na tutaishi kwa namna zozote zile. period.
"cynic" kwa level yako ya kufikiri na kutoa solution, hebu tupatie majina ya Tume yako ambayo ungeunda. Acha mawazo yaliopitwa na wakati.
Kampa shemeji yake? Hapa vilevile kuna tatizo.
Msolla aunda kamati ya kuchochea sayansi
James Magai
WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Profesa Peter Msolla ameunda Kamati ya ushauri katika masuala ya Teknolojia na Mawasiliano ambayo pamoja na majukumu mengine itaishauri Serikali namna ya kuwavutia vijana wasome masomo ya sayansi.
Prof. Msolla alisema hayo ofisini kwake jana, kabla ya uzinduzi wa Kamati ya ushauri wa masuala ya Teknolojia na Mawasiliano ambayo iliundwa hivi karibuni.
Wajumbe wa Kamati hiyo ni Profesa Mathew Luhanga , Profesa Burton Mwamila, Profesa Suzan Nchimbi Msolla, Profesa Keto Mshigeni na Margareth Munyagi.Wengine ni Dk.Tito Mwinuka na Margareth Komba ambao mi wajumbe wa sekretarieti.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo ambaye ni Makamu Mkuu Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Luhanga, alsema Kamati yake itatumia uwezo wake utakaoisaidia Wizara katika utendaji wake kwa ajili ya maendeleo ya Taifa na kwamba wiki ijayo watakaa kutafakari namna ya kutekeleza majukumu hayo.
Tuma maoni kwa Mhariri
© Mwananchi Communications Ltd 2006- 2009
Hivi hakuna wanasayansi wanaofaa kuwepo kwenye kamati hii kutoka kwinginepo? Na wote ni wakristo!
Ni kweli, huyu mama ni shemeji yake.
Binafsi sina tatizo kama mtu ana ujuzi unaotakiwa. Ndio maana huu mjadala ungeonekana una mwelekeo iwapo ungeangalia kama walioteuliwa wote wana sifa za kuwa kwenye kamati. Suala la udini na ukanda visingekuwa na maana sana kwa sababu hawatafuti technolojia ya kuendesha misikiti au makanisa wala mkoa. Tunapoteza sana muda wetu kujadili mambo ambayo hayana tija.