Uteuzi umeiua Tasnia ya Habari wa kasi ya Turbo

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,551
11,879
Tulimsikia Rais live akiwa Arusha.

Akitamka kupokea message za kuomba salio kutoka kwa mmojawapo wa waandishi waandamizi nchini.

Huo ni mfano na uthibitisho tosha kwamba waandishi wa nchi hii ni mabingwa wa kupokea zile bahasha za rangi ya Kakhi.

Baada ya mtindo wa kuteua baadhi ya viongozi wa sekta za Umma.

Kutoka kwenye sekta ya habari nchini kushika kasi.

Jambo hili limegeuka tatizo au kansa inayokula waandishi na tasnia nzima ya habari nchini.

Badala ya kutoa content za habari zenye kuzingatia weledi wao na masharti ya taaluma yao.

Sasa sekta ya habari kila mmoja anashindana na mwenzake kuhakikisha walau mteuzi amemuona.

Kila Mtangazaji amegeuka kitengo cha CCM na serikali yake.

Kila mwandishi au Mtangazaji nchini Tanzania, anaota kuja kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi wa maendeleo au msemaji wa Ikulu.

Hususan Watangazaji wa luninga wao hata kuficha hisia zao pale wanaporipoti habari zao,utadhani kada wa CCM ambae kasahau kuvaa sare ya CCM siku hiyo.

Hata wale viongozi wa jukwaa la wahariri nchini, sasa nao wanaota kwenda Ikulu kuwa wasemaji wa Serikali.

Kwa hali hii,wananchi wamepoteza ari ya kusoma au kununua Magazeti.

Kwa sababu wanakutana na habari zilezile ambazo tayari walikwisha ziona kwenye Luninga majumbani kwao.

Yamebaki magazeti machache ambayo bado yanaandika habari za kiuchunguzi nchini.

Lakini nayo yakigubikwa na kashfa mbalimbali za kutumika na baadhi ya watu ili kuwamaliza kisiasa,kibiashara au kitaaluma nk.

Wananchi wengi kwa sasa wanaamini habari za kwenye magroup ya WhatsApp na Mitandaoni kuliko vyombo rasmi vya uhabarishaji nchini.

Hii kansa inapaswa kutafutiwa muarobaini wake kabla haijafika pabaya zaidi.

commonmwananchi.
100101
 
Waandishi nao ni binadamu ndugu zangu 😂😂.

Ila kwa hali iliyofikia nchi hii ahahahaaa, kazi ni kubwa sana, hao hao waandishi wanajua ili ufanye kazi vizuri lazima umwage sifa na shukurani kwa walioshika mpini.

Wanafaham ili ule kwa urefu wa kamba lazima uchutame, hakuna mwandishi anayetaka kuona anafukuzwa kwenye press au chombo chao akipokei barua ya mwaliko kwenda kuripoti tukio, lazima wafagilie.

Wengi mnadai katiba nyingine ambayo itatoa nafasi kila mtu kuwajibika kwa nafasi yake na kuondoa ombwe la 'unijui mimi ni nani' vinginevyo hakuna cha mhariri wala raia wote kazi ni moja...
 
Waandishi nao ni binadamu ndugu zangu .

Umenena Ya Moyoni Mwako Mkuu TODAYS
 
Kwani hili dongo linawagusa na waandishi nguli kama akina P pia🤔
 
Tulimsikia Rais live akiwa Arusha.
Akitamka kupokea message za kuomba salio kutoka kwa mmojawapo wa waandishi waandamizi nchini.

Huo ni mfano na uthibitisho tosha kwamba waandishi wa nchi hii ni mabingwa wa kupokea zile bahasha za rangi ya Kakhi.

Baada ya mtindo wa kuteua baadhi ya viongozi wa sekta za Umma.
Kutoka kwenye sekta ya habari nchini kushika kasi

Jambo hili limegeuka tatizo au kansa inayokula waandishi na tasnia nzima ya habari nchini.

Badala ya kutoa content za habari zenye kuzingatia weledi wao na masharti ya taaluma yao.

Sasa sekta ya habari kila mmoja anashindana na mwenzake kuhakikisha walau mteuzi amemuona.

Kila Mtangazaji amegeuka kitengo cha CCM na serikali yake.

Kila mwandishi au Mtangazaji nchini Tanzania, anaota kuja kuwa mkuu wa wilaya au mkurugenzi wa maendeleo au msemaji wa Ikulu.

Hususan Watangazaji wa luninga wao hata kuficha hisia zao pale wanaporipoti habari zao,utadhani kada wa CCM ambae kasahau kuvaa sare ya CCM siku hiyo.

Hata wale viongozi wa jukwaa la wahariri nchini, sasa nao wanaota kwenda Ikulu kuwa wasemaji wa Serikali.

Kwa hali hii,wananchi wamepoteza ari ya kusoma au kununua Magazeti.
Kwa sababu wanakutana na habari zilezile ambazo tayari walikwisha ziona kwenye Luninga majumbani kwao.

Yamebaki magazeti machache ambayo bado yanaandika habari za kiuchunguzi nchini.

Lakini nayo yakigubikwa na kashfa mbalimbali za kutumika na baadhi ya watu ili kuwamaliza kisiasa,kibiashara au kitaaluma nk.

Wananchi wengi kwa sasa wanaamini habari za kwenye magroup ya WhatsApp na Mitandaoni kuliko vyombo rasmi vya uhabarishaji nchini.

Hii kansa inapaswa kutafutiwa muarobaini wake kabla haijafika pabaya zaidi.

commonmwananchi.
100101
Hakuna waandishi ni makanjanja tupu
 
Back
Top Bottom