Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,199
- 4,669
Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta Amemteu Bi Jessica Rose Epel Alupo almaarufu Jessica Alupo kuwa Makamu wa Rais wa Uganda kwa kipindi kuanzia 2021 - 2026
Bi Alupo ni Meja Mstaafu wa UPDF na amehudumu akiwa Waziri wa Elimu kuanzia 2011 na pia ni Mbunge wa kuchaguliwa kutokea Eilaya ya Katakwi
Mheshimiwa Alupo ni msomi wa Shahada ya Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu Cha Makerere na pia anazo Shahada mbili za Uzamili kwenye mahusuano ya Kimataifa ( International Relations) na nyingine Utawala ( Public Administration)
Makamo huyo mteule wa Uganda amezaliwa tarehe 23 Mei 1974 na ameolewa na Meja Innocent Tukashaba
Bi Alupo atachukua nafasi ya Makamu wa Rais wa sasa aliyeteuliwa mwaka 2012 mwenye umri wa miaka 79 Edward Kiwanuka Ssekandi
Bi Jessica Rose Epel Alupo