UTEUZI: Rais Museveni amteua Jessica Rose Epel Alupo kuwa Makamu wa Rais wa Uganda

Uzalendo Wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
1,119
2,000
Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta Amemteu Bi Jessica Rose Epel Alupo almaarufu Jessica Alupo kuwa Makamu wa Rais wa Uganda kwa kipindi kuanzia 2021 - 2026

Bi Alupo ni Meja Mstaafu wa UPDF na amehudumu akiwa Waziri wa Elimu kuanzia 2011 na pia ni Mbunge wa kuchaguliwa kutokea Eilaya ya Katakwi

Mheshimiwa Alupo ni msomi wa Shahada ya Sayansi ya Siasa kutoka Chuo Kikuu Cha Makerere na pia anazo Shahada mbili za Uzamili kwenye mahusuano ya Kimataifa ( International Relations) na nyingine Utawala ( Public Administration)

Makamo huyo mteule wa Uganda amezaliwa tarehe 23 Mei 1974 na ameolewa na Meja Innocent Tukashaba

Bi Alupo atachukua nafasi ya Makamu wa Rais wa sasa aliyeteuliwa mwaka 2012 mwenye umri wa miaka 79 Edward Kiwanuka Ssekandi

Alupo.jpg

Bi Jessica Rose Epel Alupo​
 
Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Inamana Uganda wameshindwa kabisa kumshtaki huyu dikteta uchwara kwa Mungu kama tulivyofanya TZ
Akitoka Madarakani Mwanae ( First Son ) Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni ' Commando ' akiwa ndiyo Kiongozi wa Kikosi cha Makomandoo na Ulinzi wa Baba yake Special Force Command ( SFC ) atamrithi na tayari Mwanae huyo ana Jeshi lake Kivuli ambalo liko ' very Loyal ' Kwake na pia hata 75% ya Wakubwa Jeshini nchini Uganda na Wanajeshi wa Uganda wanamkubali na Kumpenda sana.
 
Lakasa chika7

JF-Expert Member
Jan 7, 2017
378
1,000
M

Mbn hatari
 
Prince Kunta

JF-Expert Member
Mar 27, 2014
18,528
2,000
Akitoka Madarakani Mwanae ( First Son ) Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni ' Commando ' akiwa ndiyo Kiongozi wa Kikosi cha Makomandoo na Ulinzi wa Baba yake Special Force Command ( SFC ) atamrithi na tayari Mwanae huyo ana Jeshi lake Kivuli ambalo liko ' very Loyal ' Kwake na pia hata 75% ya Wakubwa Jeshini nchini Uganda na Wanajeshi wa Uganda wanamkubali na Kumpenda sana.
Hicho kikosi ndo kilimshambulia yule jenerali na kumuua mtoto wake!!
 
Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
4,411
2,000
Uganda nayo itaongozwa na Rais mwanamke hata kama ni kwa muda mfupi.

Katiba ya Uganda inaelekeza kuwa, endapo Rais aliyepo madarakani atafariki basi Makamu wa Rais atashikilia kiti kwa kipindi cha miezi 6 kabla ya uchaguzi kuitishwa. Endapo kipindi kilichobakia ni chini ya mwaka mmoja basi uchaguzi hautaitishwa mpaka ifike kalenda ya Uchaguzi.

Ni tofauti kidogo na hapa kwetu ambapo makamu wa Rais anakuwa Rais kwa kipindi kilichosalia.
 
Poisonous

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
42,477
2,000
Hicho kikosi ndo kilimshambulia yule jenerali na kumuua mtoto wake!!
Ndiyo na tatizo Kubwa ndani ya Jeshi la Uganda na hata katika Idara yao ya Ujasusi Jeshini ya CMI na hara zile zingine Mbili za ISO ( ya ndani ) na ESO ( ya nje ) kumejaa ' Usaliti ' mkubwa sana na humo humo kumejitokeza Makundi ya ' Kimafia ' yenye Kazi kubwa ya ' Kuua ' tu Watu ' Tishio ' kwa Urais wa Museveni au wale ambao wanapinga ' First Son ' Muhoozi Kainerugaba kuja kuwa Rais.

Na aliyekuwa ' Mratibu ' Mkuu wa Vitendo hivi vya ' Kimafia ' nchini Uganda alikuwa ni Amama Mbabazi ( aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uganda ) ambaye nae kwa sasa ' anawindwa ' mno ' Kuuwawa ' na Ndugu za wale waliouliwa ' Kinyama ' kwa Maelekezo yake.
 
Chen Hu

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
4,025
2,000
Kwani hawa jamaa katiba yao inasemaje kuhusu makamo wa rais kuwa rais.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom