UTEUZI: Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi TAKUKURU

Acha Maswali ya Kitoto,
Nimekupa mpaka mifano ya JWTZ na Jeshi letu la Polisi kutumia neno Forces tunapotamka kwa Kiingereza!

Tanzania People's defense forces na Tanzania Police Forces

Nilijua uelewa wako ni mdogo sana tangu awali Ndio sababu nikakufundisha kuwa Kamishna ni Cheo cha Kijeshi ukabisha kwa kuwa umekariri Jeshi ni JWTZ, pekee!
Nikakupa Mfano Mwingine kuwa Mkuu wa Majeshi yetu kwa Kiingereza ni Chief of Defence Forces itoshe kujua kuwa kuna Majeshi Mengi Ndio sababu anaitwa Mkuu wa Majeshi sio Mkuu wa Jeshi.

JF ni kisima cha Elimu naamini umeelimika Leo kuwa Jeshi Maana yake sio JWTZ pekee japo utakuwa ngumu kukiri!
Swali military ni nini?
 
tatizo la mkulu anaamini akimteua mtu kuwa brigedia, kamanda etc, kwenye masuala yanayotakiwa kutumia akili na wala sio nguvu ndio ataleta ufanisi. hata hivyo nampongeza kwa kazi zake.
kuna meja jeneral mmoja kamchagua Katibu Mkuu kwenye wizara nyeti hana msaada wowote zaidi ya kuwa mzigo tu
 
Bregadia General Hata Kama angebaki Jeshini bado angekuwa anampigia Salute Full Kamishna wa Jeshi la Polisi na Valentino alikuwa Full Kamishna kwa Cheo cha Kijeshi!


Walipochemka ni Kagera
RC ni Meja General Kijuu Halafu Msaidizi wake ni Kamishna Diwani Athumani!
Hujui Mamsuala ya kijeshi we mjinga wewe. Luteni wa jeshi aweza kuwa mkubwa kuliko mlowola sembuse brigedier?Kachochee maharage acha kuchangia usiyoyajua
 
Hapo jamaa naona analamba mishahara miwili kwa mpigo,Watu na bahati zao
Hakuna cha mishahara miwili hapo, atafanyia kazi alipopewa teuzi lakini atalipwa sehemu moja tu, labda kama kuna posho kwenye huo uteuzi ndio atakuwa anakula.

with my weather
 
kwenye taasisi ya upelelezi hauhitaji ujasusi, unahitaji knowledge ya upelelezi wa makosa ya jinai wa kitaaluma. sio ujasusi wa kijeshi, hapo takukuru kuna hadi waalumu, wanachunguza waalimu, wahasibu, wanachunguza wahasibu, wachunguzi wapo wa aina nyingi, hivyo ni taasisi isiyohitaji mtu anayetumia manguvu (jeshi) bali ujuzi wa akili kumkichwa, unaijua takukuru lakini? ndo maana wanafanya kazi hata luck up ya kuweka mahabusu wanaowakamata hawana, ni kwasababu ni taasisi inayotakiwa kutumia akili sio nguvu. upo hapo?


Tatizo lenu mkimsikia Fulani mwanajeshi mnadhania wanatumia nguvu tu kama ni hivyo wangejiongoza kuruta na brigadier's wasingekuwepo hivi kuna eneo linalohitaji utumiaji wa akili kama kwenye vita au jeshini?hawa ndio wanao plan na kuumiza vichwa kuliko taasisi yeyote ile


Comment yako inaonyesha ulivyo kariri na uelewa mdogo ,

By the way jamaa ni mwanasheria, wakili ,jasusi nk nk

Bado unazo hizo doubts zako au hujui jeshini kuna hackers ,doctors ,lawyers nk
Na inawezekana jamaa ana experience kubwa kwa field aliyofanyia kazi kuliko hao unaotawataka
 
Uzuri wa Mijadala kama hii haihitaji Matusi wala Kshfa kama kweli unataka kuelimishwa sio kubisha!

Mie nimezungumzia Bregadia Generali nawe ukaja kuandika Bregadia ukidhani ni cheo kimoja au Bregadia Jeneral kifupi chake ni Bregadia,

Labda nikupe Formula rahisi tu, siku nyingine kukiwa na dhifa ya Kitaifa Ikulu ( AU POPOTE) tazama wanavyokaa Askari wa Majeshi yetu kwa Protocal ndio utajua Kamishna wa Jeshi la Polisi na Bregadia generali wa JWTZ yupi ni Mkubwa

Unajua kuwa ASP wa Jeshi la Polisi akikutana Luteni wa JWTZ basi luteni anapiga Salute?
Unaposema brigedia au brigedia jenerali elewa ni cheo kimoja

with my weather
 
Swali military ni nini?

Unapouliza swali ukijibiwa katika ustaarabu wa kawaida lazima ulete mrejesho Kama umeelewa kabla ya kuuliza lingine
Uliuliza Jeshi kwa Kiingereza ni nini nikakujibu ni Forces sasa badala ya kujenga hoja yako kuanzia hapo au kutoa maoni yako kwny Hilo jibu langu unakimbilia kuuliza swali lingine, Mjadala huwa hauendi hivyo
 
mi hata sielewi tunakolazimishwa kwenda
maana makamanda wa jeshi wanapewaga hadi nafasi za kichama..
na kuna vyeo hupandi hadi uwe na kadi hai ya chichemi..
wakupambana na adui asivuke mpaka anapambana na kile ambacho wengine hukitumia kushawishi kupitisha sheria ama kukuwadia wanaume ndani ya vyama..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bregadia General Hata Kama angebaki Jeshini bado angekuwa anampigia Salute Full Kamishna wa Jeshi la Polisi na Valentino alikuwa Full Kamishna kwa Cheo cha Kijeshi!


Walipochemka ni Kagera
RC ni Meja General Kijuu Halafu Msaidizi wake ni Kamishna Diwani Athumani!

Kuna point nilitaka kuiweka sawa upate kuelewa, deputy kamishina wa polisi ni sawa na kanali kwa jwtz Kamishina wa polisi cheo hiki ni sawa na bregadia jenerali(*) , inspector jenerali wa polisi ni sawa na meja jenerali kwa jwtz(**).
na ndio mana silo kuna watu 2 anawapigia saluti kwa sasa luteni jenerali (***) na jenerali (****)

For this case Valentino ni mkubwa kwa kuwa alipata rank kabla ya Mbungo japo rank ni sawa lakini ni nani alianza kukipata hicho cheo, by similar case utaona hapo kagera kuwa Kiju ni mkubwa kwa Diwani Athmani
nipo tayari kukosolewa
 
Sawa kivipi, uzito wa mwili, kijinsia au umri? fafanua
Kicheo sawa, tatizo lipo kwenye madaraka na utendaji.
Hapo kwenye uteuzi sijaona tatizo kwani cheo madaraka na uteuzi ni vitu tofauti.

Lazima muelewe kwanza kwenye madaraka mtu anayopewa na rais basi yanamata kuliko cheo chake.

Mtu anaweza kuwa {Meja general, brigedia general, DCP, SSP au hata SACP} akipewa madaraka na rais ya kuwa Mkuu wa mkoa basi elewa kwa madaraka yake lazima apigiwe Salute na CDF au IGP, kwa mantiki hio wote walio chini ya hao ni lazima kusalute.

with my weather
 
Mwalimu anakuwa mwanafunzi wa mwafunzi wake!
Si poa kiuhalisia!
Watanzania wengi uelewa wetu katika masuala mbalimbali ya kitaalumu ni mdogo

Tunaokoteleza stori mitaani mwisho wa siku mtu anakomalia kitu utadhani ana uhakika nacho bila kujua kuwa watu wanaoelewa wanamchila tu.
Munawezaje kumshusha mtu aliyebobea katika utumishi katika taasisi inayoshughulikia upelelezi wa makosa ya jinai na kumkweza ambaye kazi zake hazihusiani na jinai

Mlowola amebobea katika upelelezi wa masuala ya wizi wa fedha na kughushi na ni wasomi wachache waliopata kozi za namna hiyo nje ya nchi katika majeshi yetu na wengi wao wa kizazi cha Mlowola walitoka polisi, maana wakati huo Takukuru walikuwa ni kitengo ndani ya polisi.

Nani awe juu ya nani kwangu mimi si suala la kuzingatia, la kuzingatia nani mwenye sifa za kiueledi za kuongoza TAKUKURU kama yalivyo majukumu ya taasisi hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania wengi uelewa wetu katika masuala mbalimbali ya kitaalumu ni mdogo

Tunaokoteleza stori mitaani mwisho wa siku mtu anakomalia kitu utadhani ana uhakika nacho bila kujua kuwa watu wanaoelewa wanamchila tu.
Munawezaje kumshusha mtu aliyebobea katika utumishi katika taasisi inayoshughulikia upelelezi wa makosa ya jinai na kumkweza ambaye kazi zake hazihusiani na jinai

Mlowola amebobea katika upelelezi wa masuala ya wizi wa fedha na kughushi na ni wasomi wachache waliopata kozi za namna hiyo nje ya nchi katika majeshi yetu na wengi wao wa kizazi cha Mlowola walitoka polisi, maana wakati huo Takukuru walikuwa ni kitengo ndani ya polisi.

Nani awe juu ya nani kwangu mimi si suala la kuzingatia, la kuzingatia nani mwenye sifa za kiueledi za kuongoza TAKUKURU kama yalivyo majukumu ya taasisi hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona umeshindwa kuona logic ya comment yangu.
Kwa vyovyote vile cheo cha Brig Gen ni kikubwa kijeshi ukilinganisha na Comissioner.
Kumbuka kuwa Taasisi ya Takukuru ilikuwa ikiongozwa na Brig General Kamazima hapo nyuma.
Kimsingi huyu Brig Gen Mbungo amepewa majukumu madogo kulingana na cheo chake, na kuwa chini ya mtu aliye chini kijeshi.
Hii inaweza leta figisu figisu!
 
Back
Top Bottom