UTEUZI: Rais Magufuli amteua Balozi Wilbert Ibuge kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,060
4,046
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Balozi(Kanali) Wilbert Augustine Ibuge kuwa katibu mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Kabla ya wadhifa huo, Kanali Balozi Wilbert Augustine Ibuge alikuwa Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Amechukuwa nafasi ya Dkt. Faraji Mnyepe ambaye aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ulinzi na Jshi la Kujenga Taifa.

Uteuzi wa kujaza nafasi aliyoacha Kanali Ibuge itatangazwa baadaye.


Uteuzi.jpg
 
Huyu jamaa anaingilia jeshi. Nadhani hii ni hatari kwa manufaa yake. Hauwezi kuijaza wanajeshi kwenye serikali ya kidemokrasia. Unless ameamua liwalo na liwe, full dictatorship
 
Hizi kazi wazitangaze basi jamani watu tushindanishwe (hata kama ni kwa itikadi za CCM basi akina johnthebaptist wapewe. Potelea mbali ila tuitwe na sisi tupeleke wasifu wetu.:)

Maana naona mzee ana fanya recycling tuu wakati vijana wanaambiwa wajiajiri. Nchi ngumu sana hii!
 
Bado tunasubiri ubatizo wa Moto wa makatibu wakuu wastaafu wa CCM msitutoe kwenye reli
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom