UTEUZI: Mustafa Hamisi Umande ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mustafa Hamisi Umande kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Chai Tanzania

Anachukua nafasi ya Mhandisi Steven Mlote aliyemaliza muda wake. Uteuzi wake umeanza Oktoba 08, 2021

FBaPngdXsAIQt9W.jpg
 
Katiba ya Tanzania ina mapungufu, ukishampa Rais wa nchi mamlaka haya yote kisheria si salama kwa ustawi wa nchi kidemokrasia hasa ukizingatia nchi inafuata mfumo wa vyama vingi vya kisiasa, na Rais anatokana na chama kimoja cha siasa, sasa anafanyaje kwa mamlaka haya kutenda haki na usawa kwa raia wote.

Yaani tangu awamu ya TANO hadi sasa ndiyo nimegundua Rais wa Tanzania ni mtu mkubwa sana... maana ukiweka list ya watu anaowateua nafikiri wanafikia zaidi ya 1000 na ushee.
 
Huyu Mwenyekiti ahakikishe MNADA wa Chai unakuja Tanzania...wakulima wa Chai tunataka kuona tija ikiwemo bei nzuri ya majani ya chai kwa sasa bei ya majani mabichi iko chini sana sababu ya gharama kubwa za usafirishaji TZ kwenda MOMBASA then nje.

Mnada wa Chai uletwe Tanzania na sio CHAI yetu yote tuuzie Kenya tunawanufaisha wakenya na ku-export ajira badala ya kutengeneza ajira.

Mheshimiwa Rais tunaomba huyu Mwenyekiti awekewe lengo kuhakikisha chai mnada wake unakuwa hapa nchini ili tupate tija.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom