UTEUZI: Mtumwa Ameir Khatib ateuliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TCAA

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,393
2,000
Hongera kwake Bi.Mtumwa Ameir Mungu amtangulie ktk majukumu yake mapya.
Tuwe wazalendo tuchape kazi kwa bidii na maarifa.
mhe.Rais amekuamini basi tusimuangushe.
 
secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
5,508
2,000
Katiba yetu mbovu sana hizi nafasi watu wanatakiwa waombe kulingana na qualification zao wanafanyiwa interview ,kwa staili hiyo utapata wajuzi waliobobea mchana kweupe......then wanathibitishwa bungeni.....
watu wenye weledi wanapatikana kwa staili hii.....
 
Mine eyes

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
5,799
2,000
Watawale Zanzibar huko kwao.

Kama Zanzibar ilivyo ni ya wazanzibari, Tanganyika ni ya watanganika.

Ndoa ya ccm na Zanzibar inatuletea vitu vya ajabu sana.

Huu muungano ni muungano wa ajabu sana.
Mkuu na Raisi Huseni na babaake Mzee Mwinyi mbona ni wazaramo..Jumbe pia..
Mawaziri na wawakilishi ni kama desturi huku kuwa watanganyika kwa vile ccm ..80% ..asili ni watanganyika.

Ni vile tu wengi hamjui hilo....hata maofini viongozi wengi ni watanganyika mkuu...yanafichwa tu...

Imani iliyopo huku ni kwamba mtanganyika hawezi kusaliti chama!

Hata huyo mama mkubwa ni watu wanayafunika tu...lakini ukichimba.. manyema tribe!

Anachogomba mpemba ndio kile kile sasa kina kuja huku...mrima!
 
silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
820
1,000
Watawale Zanzibar huko kwao.

Kama Zanzibar ilivyo ni ya wazanzibari, Tanganyika ni ya watanganika.

Ndoa ya ccm na Zanzibar inatuletea vitu vya ajabu sana.

Huu muungano ni muungano wa ajabu sana.
Sawa , Anzisheni basi serekali ya Tanganyika muhudumu watanganyika wenyewe
 
Lizzy

JF-Expert Member
May 25, 2009
24,945
2,000
Hongera nyingi kwake madam Mtumwa. Kwa jinsi alivyo nna uhakika ataitendea haki nafasi yake mpya!!
 
bitimkongwe

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
3,897
2,000
Mkuu na Raisi Huseni na babaake Mzee Mwinyi mbona ni wazaramo..Jumbe pia..
Mawaziri na wawakilishi ni kama desturi huku kuwa watanganyika kwa vile ccm ..80% ..asili ni watanganyika.

Ni vile tu wengi hamjui hilo....hata maofini viongozi wengi ni watanganyika mkuu...yanafichwa tu...

Imani iliyopo huku ni kwamba mtanganyika hawezi kusaliti chama!

Hata huyo mama mkubwa ni watu wanayafunika tu...lakini ukichimba.. manyema tribe!

Anachogomba mpemba ndio kile kile sasa kina kuja huku...mrima!
Na ajitahidi kufanya utafiti acheki asili ya wabunge wanaotoka Zenji atauona ukweli ...... akina Nzori, Mapuri, Mwakanjuki, Castico na wengine wengi tu...... funika kombe mambo yaende!
 
zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,393
2,000
watanzania kinacho wasumbua zaidi ni ROHO MBAYA, ROHO YA KWA NINI yule kapata na sio mimi!!!
FITINA na MAJUNGU kibao haswa kwenye ofisi za umma, kuna siku moja nilienda ofisi moja ya umma kupata huduma ya kudai haki yaani nilikutana na majungu na fitina huko balaa wanalimana wao kwa wao, niliishiwa nguvu zote, nilikata tamaa ya kupata haki, maaana nilijiuliza kama watu wenyewe ndio hawa wapiga majungu na fitina kweli nitapata haki yangu?!
badilikeni.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom