Uteuzi Mchanganyo wa Watendaji Waleta hofu juu ya Umakini Uliopo

Ipo siku atamteua Messi kuwa DED Babati,halafu baada ya kugundua amekosea atatangaza kuwa kamtumbua.
 
Muhimbili ulipotokea mchanganyo wa operation (jambo ambalo ni la muhimu) na kusababisha mgojwa wa mguu kupasuliwa kichwa na wa Kichwa kupasuliwa mguu, kulitokea hofu kubwa juu ya umakini uliopo kwenye utendaji wa Hospitali yetu kuu.
Hofu hiyo sasa imehamia kwa watendaji wakuu wanao husika na teuzi (jambo ambalo ni la msingi kwa shughuli za serikali) kuwa jee kweli wako makini? Mkanganyiko uliojitokeza katika teuzi za Madc, MaDas na wakurugenzi wa halmashauri umeleta picha kuwa kuna watu wanafanya kazi bila kuwa makini.
Jee ni mangapi yanayofanyika kwa mtindo huu bila kufahamika? Kuna mikataba mingapi inayopita kwa mtindo huu na kuja kutuathiri baadae? Sio ajabu baada ya miaka miwili ijayo tukajikuta kwenye matatizo makubwa sana. Bahati mbaya hatupendi kukosolewa bali kusifiwa tuu.
Ndiyo hapo sasa!! Mkataba wa kurasa 300 watakuwa makini kweli na kila mstari ni muhimu kuuelewa tena kwa kingereza!!
 
Wakukurupuka katika ubora wake. Tulianzia mbali katika ukurupukaji, kwanza kwa kusema rais wa Libya ni Saddam Hussein, baada ya hapo tukakurupuka kuliweka bunge gizani, tukaendelea kukurupuka kwenye suala la sukari, tukakurupuka suala la udom na kutoa lugha za maudhi- VILAZA, kumbe Jesca wetu nae ni kilaza, tukaja kupiga stop mikutano na makongamano ya vyama tukasahau kuwa tarehe 23 july tunapaswa kukutana, mpango wa kukurupuka unaendelea sasa ni kwenye uteuzi wa nafasi nyeti za serikali. Mwaka huu kila rangi tutaona. Ila naomba tu walio teuliwa kimakosa ikulu ikawatangaza kimakosa walipwe hivyo hivyo kimakosa kwani wamekwisha athiriwa kisaikolojia. Kimsingi napendekeza walipwe fidia kwa usumbufu walopata ikiwemo wa kisaikolojia
 
Muhimbili ulipotokea mchanganyo wa operation (jambo ambalo ni la muhimu) na kusababisha mgojwa wa mguu kupasuliwa kichwa na wa Kichwa kupasuliwa mguu, kulitokea hofu kubwa juu ya umakini uliopo kwenye utendaji wa Hospitali yetu kuu.
Hofu hiyo sasa imehamia kwa watendaji wakuu wanao husika na teuzi (jambo ambalo ni la msingi kwa shughuli za serikali) kuwa jee kweli wako makini? Mkanganyiko uliojitokeza katika teuzi za Madc, MaDas na wakurugenzi wa halmashauri umeleta picha kuwa kuna watu wanafanya kazi bila kuwa makini.
Jee ni mangapi yanayofanyika kwa mtindo huu bila kufahamika? Kuna mikataba mingapi inayopita kwa mtindo huu na kuja kutuathiri baadae? Sio ajabu baada ya miaka miwili ijayo tukajikuta kwenye matatizo makubwa sana. Bahati mbaya hatupendi kukosolewa bali kusifiwa tuu.
Wengi wanaanza kuogopa! Lakini si ndio mataokeo ya kampeni za pushups mlizovutiwa ninyi vijana? Sasa hofu ya nini tena? Kumbukeni:
"The hallmarks of bad government are:
1. Ambiguity,
2. Arbitrariness
3. Capriciousness
 
Tuna wakati mgumu sana maana hata akaamua kuteua Wakurugenzi wa Manispaa wa Ubungo na Kigamboni wakati hizo Manispaa hazina bajeti wala Baraza la Madiwani. Wakuu wa MaDED na MaDAS ambao si waajiriwa wa Serikali.

Kazi ipo mwaka huu.
 
Ndiyo hapo sasa!! Mkataba wa kurasa 300 watakuwa makini kweli na kila mstari ni muhimu kuuelewa tena kwa kingereza!!

Lakini kuna watu ukilisema hilo watakuambia HAPA KAZI TUU. Sio ajabu sasa ni kazi tuu kama afanyazo punda, anabebeshwa mzigo na hajui unaenda wapi.
 
Nimedokezwa kwenye uzi mmoja kuwa meneja wa City Styles Hotel ya Sinza Bw Luhende Pius Gerard naye ameula kuwa DED wa Itigi na elimu yake ya Certificate ya Hotel Managemet. Tanzania ya viwanda tutaisikia bombani
 
Sasa huyo anaenda kuwaongoza watu kama Afisa kilimo wilaya ambaye unaweza kukuta ana masters ya Kilomo na uzoefu wa kazi miaka 20, Afisa mipango ambaye ana elimu ya kutosha na mzoefu wa mipango ya serikali katika level ya Halmashauri miaka kadhaa, Mganga mkuu wa wilaya na sifa zake za kutosha nk nk kweli atawaongoza kweli huyo kuelekea mapinduzi ya maendeleo au yeye atakuwa KIONGOZI wa KUONGOZWA?
Tuwe wakweli kabisa, zamani Wakurugenzi wa hizi Halmashauri walikuwa watu wanachaguliwa miongoni mwa wazoefu na wenye elimu ya kutosha na utendaji usio na shaka miongoni mwa hao niliotaja. DED sio mtu wa kujifunza atafanya nini katika majukumu yake bali tayari anapaswa kuwa mwenye weledi wa kujua nini kinatakiwa kufanyika kukabili changamoto zilizopo wilayani kwake.
Ukweli vichekesho tutaviona ndani ya miaka miwili tuu dhidi ya style hii ya uteuzi.
 
Mimi hadi nimeogopa sana, maana hata awamu ya 4 ambayo inanangwa sana kwamba haikuwa makini katika mambo mengi lakini ukweli unabaki palepale kuwa haikuwahi kuchanganya majina (hata moja tu) katika teuzi zake.
 
Awamu ya nne ilikuwa na tatizo la kuendekeza uswahili swahili tuu lakini ilikuwa inajaribu kuwa systematic. Sasa hivi ni mfano kama unaenda club ya pombe za kienyeji saa tatu usiku na kuwakuta member mle ndani washachanganya mambo walivyo.
 
Back
Top Bottom