Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,333
- 72,796
Muhimbili ulipotokea mchanganyo wa operation (jambo ambalo ni la muhimu) na kusababisha mgojwa wa mguu kupasuliwa kichwa na wa Kichwa kupasuliwa mguu, kulitokea hofu kubwa juu ya umakini uliopo kwenye utendaji wa Hospitali yetu kuu.
Hofu hiyo sasa imehamia kwa watendaji wakuu wanao husika na teuzi (jambo ambalo ni la msingi kwa shughuli za serikali) kuwa jee kweli wako makini? Mkanganyiko uliojitokeza katika teuzi za Madc, MaDas na wakurugenzi wa halmashauri umeleta picha kuwa kuna watu wanafanya kazi bila kuwa makini.
Jee ni mangapi yanayofanyika kwa mtindo huu bila kufahamika? Kuna mikataba mingapi inayopita kwa mtindo huu na kuja kutuathiri baadae? Sio ajabu baada ya miaka miwili ijayo tukajikuta kwenye matatizo makubwa sana. Bahati mbaya hatupendi kukosolewa bali kusifiwa tuu.