UTEUZI: Maj Gen Zawadi Madawili mwanamke wa kwanza!

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
RAIS Jakaya Kikwete (Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama) amewapandisha cheo maafisa wanne wa cheo cha brigadier General kuwa Major General akiwemo mama Zawadi Madawili.

Zawadi anakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi kupata cheo hicho Afrika Mashariki..pia yumo Brig Ndomba aliyekuwa Kanali na Mkuu wa Mkoa wa Arusha mwezi mmoja uliopita alipandishwa cheo kuwa bigadier na sasa ameongezewa tena..

Pia wamo maafisa wa cheo cha Kanali 15...wanaopandishwa kuwa BRIGADIER GENERAL wakiwemo wanamama wawili Grace Mwakipunda na Lilian Kingazi....

Kamati Kuu mnasemaje ..tunaomba tupate taarifa ya maafisa wote 19 jumla hawa...
 
Hongera kwa mama Madawili.

Nijuavyo mimi kupitia mafunzo yangu ya JKT, sio rahisi kwa mwana mama kufanya kazi kwenye mazingira ya jeshi. Mpaka kufikia hapo huenda huyo mama amejituma mno kuliko wanaume wengi.

Labda kuongezeka kwa wanawake wenye vyeo vya juu kutasaidia kupunguza kwa unyanyasaji wa wanawake kwenye jeshi letu.
 
How comes huyo Ndomba ndani ya miezi michache kapandishwa vyeo mara mbili? some thing fishy somewhere....
 
....kweli mtanzania ..kujituma ndio muhimu..na ni lazima iwe kuwa wanawake waliopandishwa cheo si kwa kuwa ni wanawake la..sababu ya kwanza ya wao kupanda ni lazima iwe kwenye ..uwezo wao wa MEDANI,MAFUNZO[THEORY],VITENDO..USHUJAA NA UZALENDO WAO KWA MAMA TANZANIA...sidhani kuwa wamepewa vyeo ili tu kubalance gender...kwa kuwa vita haijui hayo..

katika siku za karibuni wanawake wengi jeshini wameanza kuonesha uwezo mkubwa tu wa medani..tayari tanzania inaye rubani wa kwanza wa ndege za kivita mwanamke...

nchini AFRIKA YA KUSINI kamanda wa jeshi la anga[AIRFORCE DEFENCE COMMONDER] wa SADF ni MWANAMKE mwenye cheo cha MAJ GENERAL
 
Tunampa hongera mama Zawadi kwa kufikia mafanikio hayo.

Tunaomba akaze buti na asonge mbele na kuwahimiza wanawake wenzie kujituma. Natarajia akitoka Lowassa tutapata waziri mkuu mwanamama.

Ni mtazamo tu.
 
Its embrassing kuwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru bado tuna mambo ya FIRST this first that, wanawake waliachwa nyuma kila nyanja na kumpandisha cheo mwanamke mmoja siyo dawa

dawa ni kuhakikisha kuwa wanalipwa sawa na wanaume na representation yao kila nyanja iongezwe..kwa hili ni too little too late

anyway its a good step
 
Labda niulize tu hawa mabrigedia, majenerali nk wa jeshi letu wanalinganishwa vipi na watu kama hao katika nchi nyingine?

Kuna vigezo vinavyofanana katika kufikia hatua hizo? Hata katika majeshi ya waasi kuna vyeo hivihivi kama kwa kina Savimbi(marehemu Jonas), Joseph Kony (huko kuna vitoto vya miaka 16 vina cheo cha kapteni, meja nk!), John Garang (huyu alikuwa kanali kwenye Jeshi la Sudani, nashangaa hakujiongezea cheo kingine hadi kifo chake, lakini wenzake aliwapa vyeo), Yoweri Museveni (huyu ndio alijipandisha hadi cheo cha Lt.Gen.

Na hata yule Kizza Bessigye ambaye alijiunga na jeshi la NRA akiwa medical laboratory technician aliweza kupanda cheo akiwa msituni hadi kufikia Kanali na Dk! Sasa najiuliza hivi vyeo vinafanana kimsingi (ninamaanisha objectively), au ni subjective tu? Kwa mfano Gen David Musuguri (mstaafu) na Gen Norman Schwartzkopf (mstaafu pia) ni sawa? Nilipoingia chuo kikuu nilijiuliza swali hilohilo kuhusu maprofesa.

Nchi yetu iliporuhusu vyuo vikuu binafsi nami nikapata nafasi ya kuona wanavyopandishana vyeo kuwa profesa, nikagundua kuwa maprofesa kumbe ni tofauti kabisa, na niliposoma vyuo vya nje nikagundua kumbe kuna watu tunawaita maprofesa huko nyumbani kimasikhara kabisa! Sasa sijui kama na jeshi letu ndio hivyo, maana mie uzoefu wangu unashia JKT. Wengine mnasemaje?
 
Mama Zawadi Madawili ni mama mchapa kazi na huwa hana utani wakati akiwa kazini.

Kwa hapo nampongeza Kikwete kwa kumpandisha cheo.

Wanawake sasa waige na kufanya kazi kwa bidii ili nao wafike juu kama ambavyo kinamama wengine wameonesha.
 
Ila nimeshindwa kufahamu inakuwaje mtu mmoja apandishwe vyeo mara mbili ndani ya miezi mitatu,ni ajabu.Hapa kuna kitu.
 
vyeo vya kijeshi inatakiwa viendane..na uwezo .mfano ili kuwa na cheo fulani wanaangalia unaweza kutawala watu wangapi..capt anatakiwa kuwa na wafuasi 30..bregadier anaongoza devitions za askari 10,000..inavyotakiwa ni uwezo wa capt popote pale utakapomkuta uwe kwenye vigezo vya kimataifa.tanzania ni baadhi ya nchi ambazo maafisa wake wana uwezo wa kiutendaji unaolingana na vyeo vyao..inatakiwa bregadier wetu hata akipelekwa sandhurst akipewa mtihani wa kuandaa mkakati wa kivita afaulu sawa au karibu sawa na wa pale uk...sanasana atazidiwa na yule wa ulaya katika matumizi ya technology kwenye mipango....

maafisa wa waasi au nchi zilizotoka vitani..ni tofauti..kwanza wanakuwa wana uhaba wa maafisa wenye uwezo kimafunzo[thuogh in reality wana field experience]..inabidi wapandishane tu vyeo bila mafunzo...lakini kimantiki huwezi kumchukua afisa wa SPLA au kony aliyepeana vyeo kiholela ukampeleka kwenye mission ya kimataifa kwa kuwa anakuwa hayuko kwenye viwango vya kimataifa....

maafisa wengi wa rwandas,burundi ,uganda ets waliopita monduli wakati huko kwao wengi wana vyeo vya ukanali wenzao wa hapa kwetu bado ni maluteni..kwa kuwa nchi yetu yenye despline zaidi ya elimu pia vyeo vya juu vinaenda kwa rika...hata ukiwa msomi vipi huwezi kuwa bregadier ukiwa na miaka 30-38[mfano]..utapandishwa hadi labada luteni kanali..usubiri rika lako....
 

Its embrassing kuwa zaidi ya miaka 40 ya uhuru bado tuna mambo ya FIRST this first that, wanawake waliachwa nyuma kila nyanja na kumpandisha cheo mwanamke mmoja siyo dawa

dawa ni kuhakikisha kuwa wanalipwa sawa na wanaume na representation yao kila nyanja iongezwe..kwa hili ni too little too late

anyway its a good step

on the same note, Mkuu, 'first things' are always there its just a matter of the place and time

for example, in the US, have u ever heard of a woman president? but that possiblity is there, and I am confident you know one of the democratic party contenstats is a woman (Hillary Clinton)

In that case, assuming she will be elected, she will be the first woman president in the history of the united states, and the US got 'independence' quite some years ago.....

so, my take is, we may still have to see more 'first' things in Tanzania,

and, just by the way, is it not the 'first' thing that a minister would sign a mining contract in a 'cafe'? LOL
 
JAKAYA KIKWETE APANDISHA VYEO ASKARI 19.
Muanzisha Mada mbona Jina la Mkuu wa Mkoa wa Arusha Brigedia Samwel Ndomba halipo ktk list hii niliyoitoa Kwenye Gazeti la Tanzania Daima?,wameliacha kimakosa?,ikiwa utaiona post hii tupe maelezo.

Nukuu:
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wanne wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuwa mameja jenerali na wengine 15 kuwa brigedia jenerali kuanzia Oktoba 8, mwaka huu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Idara ya Uhusiano ya Makao Makuu ya Jeshi, miongoni mwa maofisa waliopandishwa vyeo ni pamoja na wanawake watatu.

Tatarifa hiyo inaeleza kuwa hii ni mara ya kwanza katika historia ya JWTZ kwa maofisa wake wa kike kupanda hadi kufikia ngazi ya meja jenerali, tagu jeshi hilo lilipoanzishwa 1964.

"Hii ni mara ya pili kwa mwanamke kupandishwa cheo kutoka cheo cha Kanali na kuwa Brigedia Jenerali," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Inawataja waliopandishwa kutoka brigedia jenerali kuwa meja jenerali kuwa ni Zawadi Madawili, Alfred Mbowe, ambaye ni msemaji wa jeshi hilo, Servas Hinda na Wynjones Kisamba.

Waliopandishwa kutoka kanali kuwa brigedia jenerali ni Kelvin Msemwa, Albert Kigadye, Sebastina Chiwangu, Patrick Mlowezi, Daniel Igoti, Salum Kijuu, Farrah Mohamed na Gerald Kiswaga.

Wengine ni Julius Mbilinyi, Mabula Mashauri, Vincent Mritaba, Charles Jitenga, Charles Muzanila, Grace Mwakipunda na Lilian Kingazi.
Imetolewa kwenye Tanzania Daima.
 
Labda niulize tu hawa mabrigedia, majenerali nk wa jeshi letu wanalinganishwa vipi na watu kama hao katika nchi nyingine? Kuna vigezo vinavyofanana katika kufikia hatua hizo? Hata katika majeshi ya waasi kuna vyeo hivihivi kama kwa kina Savimbi(marehemu Jonas), Joseph Kony (huko kuna vitoto vya miaka 16 vina cheo cha kapteni, meja nk!), John Garang (huyu alikuwa kanali kwenye Jeshi la Sudani, nashangaa hakujiongezea cheo kingine hadi kifo chake, lakini wenzake aliwapa vyeo), Yoweri Museveni (huyu ndio alijipandisha hadi cheo cha Lt.Gen. Na hata yule Kizza Bessigye ambaye alijiunga na jeshi la NRA akiwa medical laboratory technician aliweza kupanda cheo akiwa msituni hadi kufikia Kanali na Dk! Sasa najiuliza hivi vyeo vinafanana kimsingi (ninamaanisha objectively), au ni subjective tu? Kwa mfano Gen David Musuguri (mstaafu) na Gen Norman Schwartzkopf (mstaafu pia) ni sawa? Nilipoingia chuo kikuu nilijiuliza swali hilohilo kuhusu maprofesa. Nchi yetu iliporuhusu vyuo vikuu binafsi nami nikapata nafasi ya kuona wanavyopandishana vyeo kuwa profesa, nikagundua kuwa maprofesa kumbe ni tofauti kabisa, na niliposoma vyuo vya nje nikagundua kumbe kuna watu tunawaita maprofesa huko nyumbani kimasikhara kabisa! Sasa sijui kama na jeshi letu ndio hivyo, maana mie uzoefu wangu unashia JKT. Wengine mnasemaje?
Kwa jinsi ninajua, mafunzo, uwezo wa medani, utawala, uzoefu katika kuongoza vita ndio veigezo vya kimsingi vya mtu kupata cheo cha kijeshi!!! Na vilevile ninavyomfahamu mama Madawili sioni kwa jinsi yoyote kama alistahili hata kufikia kuwa Kanali tu. Hili ni jeshi la kitanzania linaloendeshwa na siasa. Kwa kifupi hana kiwango.

Alipandishwa haraka haraka kwa ajili ya kusaidia kupunguza unayanyasaji wa wanawake jeshini na amekuwa DWA (Director of Women Affairs) kwa muda wote wa utumishi wake!!!

Aliwahi kuakaimu u CP (Chief of Personnel) kwa wiki 1 tu akaharibu na akapewa junior wake.

Sasa kwa U meja jenerali anatakiwa chief wa dept sijui ni wapi atapewa???? Uwezo wake ni mdogo mno. Labda wamuondoe kwenye active service jeshini otherwise tunacheza.

Kwa majeshi yenye kufuata misingi ya kitaaluma hawezi hata kuwa Kapteni lakini kwa TZ tayari ni mkubwa sana. Tz kuna mabrigedia waliopita cadet tu kitu ambacho sio sahihi kabisa E.g Brig Gen S.S Salim Medical officer incharge wa Lugalo keshashindaw hata kuongoza hospital ndogo km Lugalo, na ni mzigo kwa nchi kwa vile ukimuondoa utampleleka wapi kwa cheo hicho??? lazima umuhudumie ulimpa cheo kwa maslahi yako akishindwa kuperform utamtoaje??

Na kuna a lot of staff pale wnajiita specialists wkt wana first degree tu, wengine advanced di[ploma anjiita Radiologist

Kwa nje Jeshi linaonekana safi lakini ni uozo mtupu na kitengo cha kupitishia pesa za umma kwenda mifukoni kwao. Bajeti kubwa lakini matumizi ni nje kabisa ya yaliyopangwa.

Siku zote waliopo jeshini tunaombea isije kutokea vita kwani kitakachofanyika ni kuanza na viongozi wa jeshi then adui atafuata

tunaona ni chombo kitakatifu kisichoguswa na mtu na ndio kiburi kinapoanzia.

Ndomba anastahili lakini kuna mtu kama Seni mtupu sana uliza askari yeyote pale Lugalo km kafurahia Seni kupata u meja gen???
 
FIELD MARSHAL ES:
Tupe udadavuzi wa jambo hili kwa manufaa ya wana JF wote maana Mh.Mzuzu umeunguruma awezavyo lakini nina mashaka na uzito wa tuhuma za mama Meja Jenerali.
 
Tunampa hongera mama Zawadi kwa kufikia mafanikio hayo. Tunaomba akaze buti na asonge mbele na kuwahimiza wanawake wenzie kujituma. Natarajia akitoka Lowassa tutapata waziri mkuu mwanamama.
Ni mtazamo tu.

Tena mtazamo wenye akili! I hope i will be the first one.
 
Nidhamu ni suala la msingi katika jeshi letu, bila shaka mtaniunga mkono kwamba sasa hivi nidhamu ya jeshi letu inashuka kila kukicha watakao bisha nitaendelea kuwabisha. Sababu hasa ya kushuka maadili au niseme tena nidhamu hiyo ni uongozi mbovu. Mfano wa kushuka kwa nidhamu hiyo ni pale utakapoona askari wa JWTZ kujihusisha na ujambazi, askari kuwashambulia raia, askari kulewa wakiwa katika sare, ufuska nk. Vitu hivi ni kinyume na malezi ya jeshi letu. Sasa ikiwa unapata makamanda wachache wanaoonyesha mfano mzuri kutekeleza na kusimamia haya pamoja na majukumu mengine basi ni muhimu kuwaenzi hao wachache ili hatimae jeshi letu liwe na tabia moja.
 
Kwa kifupi Ndomba ni rafiki yake muungwana.
Tena walifanya nae kozi intake moja pamoja na yule bodyguard wake! Alipomteua tu kuwa mgongoni mwake akampa na ukanali juu! senior officer kama Colonel anakuwa mpambe alianzisha BMW!
 
Back
Top Bottom