The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,296
17,010
Rais Samia Suluhu kafanya mabadiliko madogo kwenye baraza la Mawaziri na mwanasheria mkuu wa Serikali kama ifuatavyo
  1. Rais Samia Suluhu amemteua Dkt. Stergomena Tax kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa, anachukua nafasi ya marehemu Elias Kwandikwa
  2. Dkt. Ashatu Kijaji ameteuliwa kuwa waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya habari kuchukua nafasi ya Dkt. Faustine Ndugulile ambae uteuzi wake umetenguliwa
  3. January Makamba anachukua nafasi ya Merdard Kalemani wizara ya Nishati
  4. Makame Mbarawa anachukua nafasi ya Chamuriho wizara ya ujenzi na uchukuzi
  5. Dkt. Feleshi anachukua nafasi ya Kilangi kuwa Mwanasheria mkuu wa Serikali


EFDFD2F4-C9D6-40D3-8C5D-8C6C1B7977FC.jpeg

AE5C9471-2694-41CE-9AD8-3B7AAB10503E.jpeg
 
As long as Mwigulu bado yupo kwenye Baraza, naweza kusema hii haitoshi-alituambie tuhamie Burundi.

Halafu hawa kina Makamba ndio watu pekee wa kuwa Mawaziri? Ni kweli wanawazidi wenzao uwezo au ni influence tu za wazazi wao ndio zinawafanya wapate kipaumbele?

Kama si hivyo, basi ni wazi CCM kuna ombwe kubwa la watu wanaofaa kuwa viongozi katika hii nchi.

Watanzania tuendelee kudai Katiba mpya tupate watu wapya kuongoza hii nchi kwani hata hawa walioenguliwa bado kesho wanaweza kurudi tena katika Baraza la Mawaziri.

Chama kilekile, Watu walewale (wanaachiana tu viti) na matokeo yake maisha ya watanzania yanabaki kuwa yale yale miaka nenda, miaka rudi.

Pathetic!

Problems can not be solved by the same level of thinking that created them-Mchungaji Msigwa.
 
44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom