UTEUZI: Jaffar Haniu ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu); amrithi Gerson Msigwa

Mmoja anahusika zaidi na mambo ya ofisi ya rais kama teuzi na tenguzi za rais, mwingine anahusika mambo ya serikali nzima kama kujibu habari za Tanzania kujihusisha kuuzia silaha waasi Burundi.
Hahaha!

Jen Psaki ni White House spokeswoman.

Ila kila wizara ina msemaji wake mkuu.

Nadhani hivyo ndivyo inafaa iwe.

But I digress. Nisije kuambiwa nahoji kisa simpendi huyo Mama.

Manake sasa hivi hatupaswi kuhoji chochote kile.
 
Kwa nini msemaji mkuu wa serikali awe tofauti na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais, Ikulu?
Msemaji Mkuu wa serikali anahusika na taarifa za serikali na anatoa ufafanuzi, kauli na msimamo wa serikali juu ya jambo lolote hata la nje ya nchi.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais anahusika na Ikulu peke yake na Rais wake, sio wizara wala idara yoyote nje.
 
Rais sasa hizi teuzi nazo ziishe, umefika muda wa kuchapa kazi. Kuna masuala ya ajira, katiba mpya n.k
Rais wa Tanzania kikatiba ana mamlaka makubwa sana ya teuzi, teuzi haziwezi kuisha kwa sababu watu wanaoteuliwa na rais ni wengi sana.

Na kila siku watu wanafariki, wanastaafu etc. Wanatakiwa wengine wateuliwe.

Hivyo teuzi haziwezi kuisha.

Cha kufanya ni kubadilisha mamlaka ya uteuzi rais asiwe na watu wengi sana wa kuwateua.

Siku za nyuma teuzi zilikuwepo, ila zilikuwa hazitangazwi sana. Kipindi cha karibuni hapa ndiyo wameanza kutangaza kila teuzi. Ndiyo maana zinaonekana nyingi sana siku hizi.
 
Rais John Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambako alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais mteule wa nchi hiyo, Edgar Lungu ili kushughulikia tatizo la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 16 mkoani Kagera.

Taarifa ya iliyotolewa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Jaffar Haniu jana usiku ilisema badala yake, Dk Magufuli amemtuma Makamu wake, Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha katika sherehe hizo. Sherehe za kumwapisha Rais Lungu zinatarajiwa kufanyika kesho Lusaka.

Source : Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom