UTEUZI: Dkt. Nicolaus Herman Shombe ateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NDC

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Nicolaus Herman Shombe kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC)

Anachukua nafasi ya Marehemu Prof. Damian Gambagambi aliyefariki akiwa katika nafasi hiyo. Kabla ya kuteuliwa, Dkt. Shombe alikuwa Kamishna wa Mipango, Wizara ya Fedha

9FE43E70-E35F-47A8-9663-75B64C0BEFB5.jpeg
 
Kwani Rais wa nchi si huwa anafanya kazi akiwa popote mkuu au mambo ni tofauti na ninavyofikiria ?
Sasahivi Rais ni Makamo wa Rais mpk ataporudi hata baraza la mawaziri likiitishwa leo akayeongoza ni Makamo wa Rais, kama anafanya kazi popote kwanini asiongoze akiwa huko huko?
 
Ubaya upo mkuu, kuteua ni gharama sn huyo mtu analipwa vitu vingi na anayeondoka analipwa pesa ndefu sn
Aliye "ondoka" katika nafasi hiyo alifariki mkuu.

Kwahiyo shirika lingeendelea kukaa bila mkurugenzi?
 
Ubaya upo mkuu, kuteua ni gharama sn huyo mtu analipwa vitu vingi na anayeondoka analipwa pesa ndefu sn
Hamna jinsi ndugu yang. Tumvumilie tu kama jinsi tulivyomvumilia mwenyekiti wetu alieenda kulewea ruzuku za chama na michango yetu. Huku akitelekeza makao makuu ya chama. Ameshindwa hata kupanga rangi ya kuzugia!

2528007_20200919_173148.jpg
 
Sasahivi Rais ni Makamo wa Rais mpk ataporudi hata baraza la mawaziri likiitishwa leo akayeongoza ni Makamo wa Rais, kama anafanya kazi popote kwanini asiongoze akiwa huko huko?

Anaendelea kuongoza na ndio maana katumia mamlaka yake ya kuteua akiwa huko huko.

Suala la makamu wa Rais kuongoza kikao cha baraza la mawaziri haimaanishi kwamba ndio amekua top, maana kuna mazingira ambayo Rais anaweza kuwapo hapa hapa nchini na Makamu wake akaongoza kikao hicho (kwa ruhusa ya Rais).

Vinginevyo useme ni vifungu gani (vyovyote vile viwavyo) vimevunjwa kwa Mh. Rais kufanya uteuzi akiwa nje ya nchi.
 
Nani ambaye amekaimu? kuna haraka gani ya kuteua akiwa huko nje?
 
Back
Top Bottom