UTEUZI: Camilius Wambura ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Je mfululizo wa hizi teuzi za kupandisha maSACP kadhaa kwa kuwarusha cheo cha u Deputy Commissioner of Police (DCP) kuwa moja kwa moja ma Commissioner of Police (CP) ni maandalizi ya kumpata IGP mpya ?

Au ni panga pangua tu ya maofisa wa ngazi za juu wa jeshi la Polisi ili liendane na mahitaji mapya ya awamu ya sita?
 
Je mfululizo wa hizi teuzi za kupandisha maSACP kadhaa kwa kuwarusha cheo cha u Deputy Commissioner of Police (DCP) kuwa moja kwa moja ma Commissioner of Polis (CP) ni maandalizi ya kumpata IGP mpya ?

Au ni panga pangua tu ya maofisa wa ngazi za juu wa jeshi la Polisi ili liendane na mahitaji mapya ya awamu ya sita?
Ukiingia nyumba ya kupanga hata ukute ina kila kitu lazima utataka kuiweka kwa ladha yako
 
Trend ya teuzi za maofisa waandamizi wa juu katika jeshi la Polisi :

Toka Maktaba ya Kumbukumbu


RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA VIONGOZI MBALIMBALI FEBRUARI 15, 2016​



4b0c8471-7af1-468a-8852-695061489a60 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akizungumza kuhusu uteuzi wa viongozi mbalimbali ambao ameufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam Februari 15,2016
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa mabalozi watatu katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Rais Magufuli pia amefanya uteuzi wa makamishna wanne wa Jeshi la Polisi na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya vitambulisho vya Taifa (NIDA).
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, imewataja mabalozi walioteuliwa kuwa ni Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro, Mheshimiwa Mathias Meinrad Chikawe na Dkt. Ramadhan Dau.
Vituo vya uwakilishi kwa mabalozi hawa vitajulikana baada ya taratibu husika za kidiplomasia kukamilika.


Kwa upande wa Makamishna wa Polisi, Balozi Sefue amewataja walioteuliwa kuwa ni:
  1. Naibu Kamishna wa Polisi DCP Simon Nyakoro Sirro ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam. Kamishna Sirro anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Mstaafu Suleiman Kova.
  2. Naibu Kamishna wa Polisi DCP Albert Nyamuhanga ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na ameteuliwa kuongoza Idara ya Fedha, Utawala na Lojistiki. Kamishna Nyamuhanga anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Clodwing Mathew Mtweve aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza.
  3. Naibu Kamishna wa Polisi ACP Robert Boaz Mikomangwa ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na ameteuliwa kuongoza Idara ya Intelijensia. Kamishna Mikomangwa anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna (CP) Valentino Mlowola aliyeteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
  4. Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Nsato Marijani Mssanzya ambaye amepandishwa cheo kuwa Kamishna wa Polisi (CP) na ameteuliwa kuongoza Idara ya Mafunzo na Operesheni. Kamishna Mssanzya anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi CP Paul Moses Chagonja aliyeteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Modestus Francis Kipilimba kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Kabla ya Uteuzi huu Dkt. Kipilimba alikuwa Mkurugenzi wa Menejimenti ya Udhibiti (Director of Risk Management) katika Benki Kuu ya Tanzania. Dkt. Kipilimba anajaza nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Dikson Maimu ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Teuzi zote zinaanzia leo tarehe 15 Februari, 2016
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
15 Februari, 2016
 
Tatizo SSH ameruhusu vimemo, baadhi ya majina yanapenyezwa ikija kufanyika proper vetting unakuta mtu hafai hiyo nafasi. SSH anahitaji kuwa mkali akiendelea kulegezea wapiga deal itakula kwake, haiwezekani kila siku kunakuwa na makosa kwenye uteuzi.
Anaruhusu vimemo na kufanyia kazi majungu
 
Back
Top Bottom