UTEUZI: Camilius Wambura ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

31 May 2021

BAADA YA KUTEULIWA NA RAIS SAMIA, DCI WAMBURA, CP HAMAD WAFUNGUKA MBELE YA IGP SIRRO "SITAKUANGUSHA"​



Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IJP Simon Nyakoro Sirro amewavalisha cheo na kuwaapisha SACP Camilius Mwongoso Wambura na ACP Hamad Khamis Hamad kuwa Kamishna wa Jeshi la Polisi.

Baada ya kupandishwa cheo hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Mhe. Samia Suluhu Hassan.


Kamishna wa Polisi (CP) Wambura ameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai nchini (DCI) na Kamishna wa Polisi (CP) Hamad amekuwa Kamishna wa Fedha na Lojistiki wa Jeshi la Polisi.

Source : Millard Ayo
 
31 May 2021

IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO MAKAMANDA WA POLISI, MULIRO AJA DSM, MUROTO ASTAAFU


Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Simon Sirro amefanya mabadiliko madogo kwa Makamanda wa Polisi, ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi. Katika mabadiliko hayo, .

Naibu Kamishna wa Polisi Lucas Mkondya amehamishwa kutoka kuwa Kaimu Kamishna wa Fedha na Logistiki Makao Makuu ya Polisi Dodoma kuwa Mkuu wa Usalama Barabarani nchini.

Na Kamanda wa polisi wa mkoa wa Kipolisi Rufiji, - Onesmo Lyanga amehamishwa kwenda kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma kuchukua nafasi ya Kamanda Gilles Muroto ambaye anastaafu.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Ramadhan Ngh'anzi amehamishwa kutoka kuwa Boharia Mkuu kwenda kuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza.

Huku Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mwamini Rwantale akihamishwa kutoka Kanda Maalum ya Dar es Salaam ambako alikuwa Mkuu wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimali watu kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Tazara.


IGP Sirro pia amemhamisha Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mwanza, - Muliro Jumanne kwenda kuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, kuchukuwa nafasi iliyoachwa na Kamishna wa Polisi Camillius Wambura.

Kamishna Msaidizi wa Polisi Zuberi Chembera, yeye amehamishwa kutoka Makao Makuu ya Upelelezi Dodoma kwenda Makao Makuu ya Polisi Zanzibar kuwa Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa jinai Zanzibar kuchukua nafasi ya Kamishna wa Polisi Hamad Khamis Hamad.


Naye Kamishna Msaidizi wa Polisi Stella Richard amehamishwa kutoka kuwa Kamanda wa Kikosi cha Polisi Tazara kwenda kuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida.

Source : Millard Ayo
 
"Incompetence" ni pamoja na kutokuwa makini kwenye uteuzi unaoishia kwenye "kutengua", au unaonaje mkuu 'kabulala
Alw
"Incompetence" ni pamoja na kutokuwa makini kwenye uteuzi unaoishia kwenye "kutengua", au unaonaje mkuu 'kabulala'!
Always inakuaga Ngumu kumwambia Mkubwa kwamba amekosea(especially a leader of a Nation... instead Sisi subjects wake inabidi tukosoe Kwa staha na kuwalaumu wasaidizi wake..but in a real sense , malalamiko yetu yanamlenga yeye but in a polite tone.
 
Alw

Always inakuaga Ngumu kumwambia Mkubwa kwamba amekosea(especially a leader of a Nation... instead Sisi subjects wake inabidi tukosoe Kwa staha na kuwalaumu wasaidizi wake..but in a real sense , malalamiko yetu yanamlenga yeye but in a polite tone.
Hilo ni sehemu ya matatizo yetu, kutosema au kutokuwa wawazi, badala yake tunazungukazunguka tuuu. Hii ni tabia ya kinafiki, na haifai kabisa.
Kiongozi ni binaadam, anakosea kama wengine wote. Akiambiwa amekosea ni dhambi?
 
Kuna,uteuzi mwingine unakuja ZPC (ZONAL POLICE COMMENDER ) MA RPC KAENI MGUU SAWA
Wewe dogo fiksi sana. Mara useme Diwani nje, Mara uteuzi wa Ma RPC.

Halafu una wiki mbili tu tangu ujiunge humu JF
 
Back
Top Bottom