Utetezi wa Yanga na wachezaji wake kwa TFF na Mashitaka Juu ya Refa Mu-Israel Mkongo

Hoja ya AZAM kulalamikiwa kiasi cha kutaka TFF ianzishe uchunguzi rasmi napende niongeze ushahidi wa mechi yao ya jana dhidi ya Rivu shooting. Msemaji wa Ruvu shooting bwana Massau najumuisha katika orodha wa mashahidi wangu kwenye hii kesi.
 
ushindi wa hoja zangu unaanza kujionyesha baada ya leo tff kukubali kufanya uchunguzi juu ya madai ya rushwa. sasa nashauriana na wataje wangu ku-compile ushahidi wa nguvu kuonyesha jinsi refa aliyesababisha fujo na usumbufu kwa wateja wangu alivyopokea rushwa. hoja zangu nyingine zitaamriwa baada ya tibaigana kupewa faili. hoja ya uhalali wa kamati na mgongano wa kimaslahi nayo inazidi kupata nguvu baada ya kuonekana ikichelewesha kwa makusudi nyaraka za kesi ya wateja wangu.
 
Wewe wakili naomba utofaitishe mambo ya mpira wa miguu na kesi zako za mambo mengine ya kijamii.naomba yanga watafute wakili anayejua mambo ya soka pengine atawasaidia.kwanza najibu hoja zako kama ifuatavyo..ntajibu chache kwa ajili ya muda.HOJA namba1.Unapuzungumzia ukubwa wa adhabu.hivi wewe ni wakili wa wapi mtu kukataa kumpa mtu mkono na mtu kumtandika mtu ngumi kweli hayo makosa yanafanana kweli!wewe wakili wa wapi? hata juzi kule ulaya tumeona mechi kati ya liverpoor na man utd uliona alichomfanyia Surexz dhidi ya beki namba tatu wa man utd kwa kukataa kumpa mkono hakuna adhabu aliyopewa...na hivi ndivyo soka na sheria zake zinavyosema.Ukimtandika mtu kwa ngumi au kosa kubwa kama hilo au kumpiga mshabiki adahbu kali inapaswa kutolewa na labda kukusaidia FIFA sheria zake kidogo zipo tofauti za mahakama,na kama kweli zingekuwa zinaingiliana basi adhabu aliyopewa mwasika ni ndogo sana kwani pamoja na kufungiwa kucheza basi angekamatwa na polisi paleplae na kushtiakiwa na jamhuri kwa kosa la kupigana na mda huu angekuwa ananyea debe Ukonga .

Unapozungumzia ushahidi wa tv hivi wewe unaangalia tv moja tu ya clouds mbona itv na chanell 5 na nyingine zote kama startv wameonyesha waziwazi,au unataka kusema wachezaji wa yanga wameonewa hawakumpiga mwamuzi?na kama hawakumpiga unalalamika kuwa adhabu waliyopewa ni kubwa kwa kosa gani.?UCTUCHANGANYE bahati mbaya sina mda wakutosha ila kama wewe ndio wakili wa yanga katika hili wamechemsha
KASENENE
LLB,MBA,MSSA
 
Asante na nashukuru angalau wewe umekuwa wa kwanza kujibu kwa hoja. lakini napenda nikukumbushe kuwa ili liwe kosa lazima litajwe kwenye sheria na kwa upande wa soka kanuni. hatutumii ulinganifu wa makosa kwa akili zako. mfano ukiangalia mambo yanayopelekea kujenga hoja ya kosa la kubaka ni mengi. nitakushangaa kama mtu aliyebaka kwa kukamatwa kwa kumuingilia mtoto wa shule na yule aliye muingilia mtoto na kumpa mimba. huwezi kusema huyu kabaka kidogo na huyu kabaka sana. kwa mantiki hiyo lazima uangalie kwanza kosa linaelezewa vipi na kanuni. kosa hapa ni vitendo visivyo vya kimichezo. kesi hii ingekuwa kwenye mahakama ya kawaida utetezi ungebadilika. kuhusu ushahidi lazima uwasilishwe rasmi. ndio maana kwenye mahakama ya kawaida ukileta kitu kama mkanda wa sauti au picha unaweza kupelekwa kwa mkemia au authority zilizopo kuthibitisha uhalali wake na lazima upokelewe. technology iliyopo inafanikisha picha kuchezewa. nadhani unakumbuka picha ya mheshimiwa zeutamu na hata picha ya kidole cha chuji kikiwa kirefu kama cha jini. tunachotaka ni ushahidi usio na shaka. karibu
 
Simba na Yanga zinaua mpira wa Tanzania na kinachosubiriwa ni kifo tu cha soka. Kila idara inayohusu soka kuna mwana simba au yanga anayetaka timu yake ipate upendeleo au anatumia mamlaka yake vibaya kuzipendelea. Matokeo yake ni kuwa timu zingine zinanyimwa haki na hazipati manufaa ya uwekezaji katika soka. Na kama Azam wamejiingiza katika mkumbo wa kuhonga waamuzi basi ujue soka limeoza. Kuna haja gani ya kuwekeza katika mfumo rushwa? Nchi ya hovyo huishia kufanya vitu vya hovyo katika kila jambo

HIVI TUSEME MPAKA LINI ILI WATU WAELEWE??? Mimi nasema kwa ujasiri mkubwa tena sana nasema kwa ARI MPYA na NGUVU MPYA na KASI MPYA Simba na Yanga zinaua mpira wa Tanzania na kama TFF na wadau wasipo stukia hili tutazika soka letu moja kwa moja . Kuna mifano mingi inajidhihirisha katika ARGUMENTS zangu.
>>>Moja kwa kipindi kirefu tumeshuhudia jinsi marefa wanayozibeba timu za simba na Yanga ( Na ndio maana siku hizi timu hizi zinaingia na kutolewa round ya kwanza tu!!!AIBU). Tofauti na zamani walau ushindi wao ulikuwa halali maana timu nyingi za mikoani zilikuwa za mashirika ya serikali hivyo zilikuwa zinatoa ushindani wa kutosha.
>>> Nijambo lisilopingika kuwa kwa miaka ya sasa mathalani kila idara inayohusu soka nchini Tanzania si ajabu kusikia kuna mwana simba au yanga anayetaka timu yake ibebwe!! ama ipate upendeleo. Mtu huyu atatumia kila aina ya ushawishi ama mamlaka yake ili kuibeba ama simba au yanga ambayo anaipenda. Matokeo yake soka linakuwa la Yanga na Simba tu. Hata mahala ambambo moja wapo ya timu hizi ni dhaibu bado utashanga bingwa ni Yanga ama Simba
>>> Kuna Mambo yanayotokea uwanjani ambayo tukiacha ushabiki wa Simba ama yanga lazima tuukemee
>>> Mathalani uchezeshaji mpira!! Marefa wengi wamekuwa wakizibeba Simba na Yanga
>>> Ni hivi Karibuni miezi michache iliyopita kocha wa Mtibwa TOM OLABA aliwahi kulalamika kwamba Simba na Yanga zinabebwa na marefa tena akatoa onyo kali kwama ugonjwa huu ukiachwa kuendelea ipo siku TANZANIA TUTAUWANA KAMA KENYA mwisho wa kumnukuu''' Sasa tujiulize hivi kweli mpaka mtu atoe maneno makali namna hiyo bado tu hatuamini kuwa kuna ukweli wa yasemwayo? Naishauri TFF ifuatilie mambo haya na kutoa onyo kali kwa marefa
>>> Ngoja nitoe Mifano michache ambayo nimeshuhudia hivi karibuni ya jinsi marefa wanavyozibeba Simba na Yanga
1. Katika Mechi ya Yanga na Villa Goli la yanga lilikuwa TATA kabisa wala hakuna ubishi Mchezajiwa Yanga alimrukia kipa akiwa ameshika mpira ukamponyoka Yanga wakachukua wakapasiana wakafunga refa kakubali!!!! AIBU sana hii
2. Simba na Mtibwa ....Kulikuwa na move upande wa kushoto sasa beki wa mtibwa alipokuwa anafuata mpira mchezaji wa Simba akamkwatua refa akapeta ...ajabu alivyopeta na simba kuchukua mpira mchezajiwa simba akaguswa kidogo tofauti hata na alivyoguswa wa Mtibwa refa kapiga filimbi Simba wakapoga faulo na kufunga Huu ni unyama
>>> Hivi Tanzania soka ni Simba na Yanga tu kwanini timu zingine zinanyimwa haki na hazipati manufaa ya uwekezaji katika soka.
NAPENDA KUSEMA KUWA HILI HALIKUZI BALI LINAUA SOKA LETU
'''''Nchi ya hovyo huishia kufanya vitu vya hovyo katika kila jambo.....mwisho wa kunukuu'''
 
nakubaliana na wewe kwamba mambo yote hayo yapo. lakini bado sidhani ni kosa la yanga na simba. nadhani ni kosa la usimamizi mbovu wa soka hapa kwetu kuruhusu mambo hayo kutokea. mfano kado alipeleka mesg za rushwa tff lakini hadi leo nadhani uchunguzi unaendelea. cha ajabu baadhi ya watuhumiwa ni baadhi ya wajumbe kwenye kamati tunazozilalamikia hapa. kama tff inamkataa wambura kwa kukosa uadilifu iweje hawa inawakumbatia. kasenene unaliona hilo? siamini kuwa yanga na simba kupendwa na watu wengi ni tatizo la kuua mpira. kuna watu wa nje wanalisifia sana hilo. mbona kunawakati fat ilikuwa makini tukapata timu kali kiasi cha kuchukua ubingwa au kuzifunga yanga na simba mara nyingi. una ikumbuka pamba ya mwanza, tumbaku, mecco na nyingine nyingi. tukiziua simba na yanga tukaiacha tff kama ilivyo mpira ndio utakuwa bye bye. tubadili kwanza tff ili zije timu strong ili simba na yanga zife naturally.
 
Wewe wakili naomba utofaitishe mambo ya mpira wa miguu na kesi zako za mambo mengine ya kijamii.naomba yanga watafute wakili anayejua mambo ya soka pengine atawasaidia.kwanza najibu hoja zako kama ifuatavyo..ntajibu chache kwa ajili ya muda.HOJA namba1.Unapuzungumzia ukubwa wa adhabu.hivi wewe ni wakili wa wapi mtu kukataa kumpa mtu mkono na mtu kumtandika mtu ngumi kweli hayo makosa yanafanana kweli!wewe wakili wa wapi? hata juzi kule ulaya tumeona mechi kati ya liverpoor na man utd uliona alichomfanyia Surexz dhidi ya beki namba tatu wa man utd kwa kukataa kumpa mkono hakuna adhabu aliyopewa...na hivi ndivyo soka na sheria zake zinavyosema.Ukimtandika mtu kwa ngumi au kosa kubwa kama hilo au kumpiga mshabiki adahbu kali inapaswa kutolewa na labda kukusaidia FIFA sheria zake kidogo zipo tofauti za mahakama,na kama kweli zingekuwa zinaingiliana basi adhabu aliyopewa mwasika ni ndogo sana kwani pamoja na kufungiwa kucheza basi angekamatwa na polisi paleplae na kushtiakiwa na jamhuri kwa kosa la kupigana na mda huu angekuwa ananyea debe Ukonga .

Unapozungumzia ushahidi wa tv hivi wewe unaangalia tv moja tu ya clouds mbona itv na chanell 5 na nyingine zote kama startv wameonyesha waziwazi,au unataka kusema wachezaji wa yanga wameonewa hawakumpiga mwamuzi?na kama hawakumpiga unalalamika kuwa adhabu waliyopewa ni kubwa kwa kosa gani.?UCTUCHANGANYE bahati mbaya sina mda wakutosha ila kama wewe ndio wakili wa yanga katika hili wamechemsha
KASENENE
LLB,MBA,MSSA

Nadhani kama kweli wewe ni mwanasheria kama mimi utakuwa sasa umeelewa nini maana ya ushahidi mbele ya sheria. Wenzio TFF waliotumia ushahidi wa TV wameshindwa kabisa kuuwasilisha ndani ya week mbili.
 
ndugu wakili naona kazi yako imeanza kuzaa matunda..
 
kazi kweli eti hapo ndio mnataka muwe kama wakina macdonald mariga.....thubuuuuuutu
 
Back
Top Bottom