Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Kitendo cha ole kengai sabaya kuwataja Magufuli na mpango ni mbinu za kijasusi ili kujitoa mikononi mwa sheria.

Hoja ya sabaya yakutengeneza,ameona hachomoki hivyo wanasayansi wake wa kisheria na timu yake same kite ten genera hili wakijua Magufuli ana kundi kubwa lililomkubali aliloliacha hapa dunia hivyo hawatakubali kuharibu legacy wanayoitetea.

Mpango yupo madarakani,haitawezekana kumfanya mshitakiwa kwa sheria mbovu na mahakama za ccm.

KWA HOJA HII WAKATI WOWOTE SABAYA OUT,KAMA ATAADHIBIWA ITAKUWA ADHABU ISIYOENDANA NA TUHUMA NZITO ALIZONAZO SASA

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
wewe ni hakimu au ndio ramli tu ilimradi
 
Ina maana siku hizi ukiwa na kesi ya jinai ukisema ulitumwa na Magufuli basi kesi yako inafutwa!
 
Ni mwehu tu anayefikr Sabaya atafungwa....wale mashahidi uchwara waliomsagia kunguni wajiandae jamaa atawakamua mavi vilivyo....!!! Kwa mda mchache pia wale matajir wakubwa walioishadadia kesi karbia wote wamekufa, wakigusa tu hospital kinachofuata ni parapanda , huku mbowe akiwa rumande ....!!! Anyway ngoja nipige pepsi big hapa
 
Sabaya hata akitoka leo hatakuwa na Jeuri,Ubabe na Dharau kama awali,ameshanyooshwa!!!na ni mjinga tu anayeweza kuamini kwamba Sabaya na timu yake HAWATAFUNGWA,hao iwe Jua au Mvua Jela inawahusu,mark my words
 
Bwana wako mbowe analiwa na papasi jera mida hii

USSR
 
Ni mwehu tu anayefikr Sabaya atafungwa....wale mashahidi uchwara waliomsagia kunguni wajiandae jamaa atawakamua mavi vilivyo....!!! Kwa mda mchache pia wale matajir wakubwa walioishadadia kesi karbia wote wamekufa, wakigusa tu hospital kinachofuata ni parapanda , huku mbowe akiwa rumande ....!!! Anyway ngoja nipige pepsi big hapa
Sabaya kufungwa atafungwa MARK THIS REPLY. kwa ngwe hii lazima atachezea mvua. Labda atakuja kuchomoka kwa RUFAA

Na hapa naongelea hii kesi pekee inayoendelea. Kaa ukijua kuna kesi nyingine ile kubwa zaidi bado haijaanza kusikilzwa
 
Ni mwehu tu anayefikr Sabaya atafungwa....wale mashahidi uchwara waliomsagia kunguni wajiandae jamaa atawakamua mavi vilivyo....!!! Kwa mda mchache pia wale matajir wakubwa walioishadadia kesi karbia wote wamekufa, wakigusa tu hospital kinachofuata ni parapanda , huku mbowe akiwa rumande ....!!! Anyway ngoja nipige pepsi big hapa
Huyo Sabaya ana madaraka gani? Ana tofauti na Makonda mtoto kipenzi wa marehemu?
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang'anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.

Sabaya anaendelea kujitetea....

Je utetezi huo una mantiki yoyote?
Raisi wa taifa anaangalia shughuli za duka la rejareja!
Anaona umuhimu mwenye duka kuhojiwa na polisi. Raisi wa taifa hawezi kutoa maagizo kwa Mkuu wa Wilaya husika wala kwa polisi ya mahali walipo?
Akishindwa kutumia njia hizo anahitaji kumtuma Mkuu wa Wilaya nyingine ???
Raisi mwenyewe ??
Utetezi wa Abunuwasi??
 
duuh nashangaa kabisa, mbona kakiri kufanya ujambazi kirahisi hivyo!!!??!! nani atamuamini kutumwa na mamlaka ya uteuzi kwenda kufanya kazi kinyume cha SHERIA?!? kwa sababu mamlaka iliyomteua in organs zote za kufanya hayo,yupo igp, yupo mkuu wa usalama wa taifa, takukuru wapo. leo ole sabaya ambaye siyo mara ya kwanza kutuhumiwa kwa ujambazi anataka kumchafua rais na taasisi yake kwa sababu hawezi kusema chochote!!!! umezama OLE
 
31 Reactions
Reply
Back
Top Bottom