Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.

Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi. sijaona unyang'anyi uliotendwa!

mnyang'anyi angechukua receipts machine ya nn?!!
mnyang'anyi angepiga simu kituo cha polisi?!
huo ni unyang'anyi wa wapi?!
 
Mkuu wa wilaya ya Ya Hai anatumwa na Raisi akafanye operation wilaya isio yake ya Arusha? Raisi Hana operative wakuu wa wilaya ya Arusha au mkuu wa mkoa wa Arusha hidden operative wa kufanya hiyo Operation...
Toka Hiyo kesi inaanza nilijua lazima Sabaya atatoa utetezi huu, maana ni kweli kuna mambo mengi kinyume na sheria Magu alikuwa anawaagiza hawa waovu wenzake. Na Sabaya anataja hayo maagizo ya kupewa na rais, maana anajua kuna wengi sana walikuwa wakiagizwa na Magu kufanya kinyume na sheria, na walikubali maana walikuwa wanafaidika na huo uovu, wao binafsi, na pia walikuwa wanalinda ajira zao kwa kumnufaisha huyo mtu muovu.

Mfano ule uporaji wa fedha za kwenye mabureau de change, shambulizi la Lisu huko kwenye makazi ya wabunge Dodoma, huku polisi wakiwa wameondolewa eneo la tukio. Hakuna kiongozi mwingine yoyote anayeweza kutoa amri zile zaidi ya rais. Hata haya mashitaka ya ugaidi dhidi ya Mbowe, ni maagizo ya rais Samia ili katiba mpya isidaiwe. Tunaposema tunataka katiba mpya, sehemu mojawapo ni haya madaraka ya rais kuendesha mambo ya uovu, huku katiba ikimpa kinga ya kutoshtakiwa.
 
Kwa hiyo Sabaya anataka kusema kuwa tatizo ni huyu kibwengo?
View attachment 1890876
Duh!!!!
FB_IMG_1612012763868.jpg
 
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru.

Sabaya hana makosa kama alikuwa anatekeleza maelekezo ya aliye mteua, naamini kama Magufuli angekuwa hai angemtetea Sabaya bila kigugumizi, lkn pia kama Mama Anna Mgwira ange kuwa hai ange mtetea Sabaya bila kigugumizi.
 
Mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya unyang’anyi wa kitumia silaha na Kupora Mali na fedha ,Lengai ole Sabaya (34)ameiambia mahakama kuwa alitumwa na rais marehemu John Magufuli kuvamia duka la Shaahid Store ili kumkamata Mmiliki wa duka hilo, Mohamed Saad.

Akiongozwa na wakili Mosses Mahuna wakati akitoa utetezi wake mbele ya hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo wa mahakama ya hakimu Mkazi Arusha,Sabaya alidai yeye bado ni mtumishi wa Serikali ila alisikia tangazo la kusimamishwa kazi kutoka Kwa Rais Samia Suluhu.

Alidai kuwa siku ya tukio Februari 9 mwaka huu majira ya saa 9 kasoro alasiri alipigiwa simu na Mamlaka iliyomteua na kumpatia maelekezo ya kwenda kufanya kazi maalumu Arusha na kumtaka aongozane na watu wanne waliokuwa wakimsubiri uwanja wa ndege wa Kimataifa Kilimanjaro KIA.

Sabaya alidai kuwa walipofika Arusha wakiwa na wale watu wanne ambao ndio wenye taarifa zote walielekea eneo husika waliokuwa wameelekezwa na Mamlaka husika katika eneo la duka la Shaahid store lililopo mtaa wa Soko kuu jijini Arusha.

Akihojiwa na Wakili Mahuna kuhusu kazi aliyokuwa akiifanya kabla ya tarehe 9.2.2021 ,Sabaya alidai alikuwa ni Mkuu wa Wilaya ya Hai Mkoani kilimanjaro na aliteuliwa na Rais Hayati Dkt John Pombe Magufuli tarehe 29.7.2018.

Lengai Ole Sabaya anaeleza mahakama kuwa alitumikia wadhifa huo kwa kipindi cha miaka 2 na miezi 10 na alikoma kuhudumu wadhifa huo tarehe 13.5.2021 baada ya Rais Samia Suluhu kutengua nafasi yake kupisha uchuguzi .

Sabaya ameieleza Mahakama kwamba baada ya kufikia katika duka hilo walimkosa Mmiliki wa duka na ndipo alipowasiliana na mamlaka iliyomtuma kazi hiyo, ambayo ilimjibu kwamba imeshafanya mawasiliano na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Kenan Kihongozi na imeelekeza watu waliokutwa eneo la tukio wapelekwe kituo cha polisi kwa mahojiano zaidi ili kusaidia kupatikana Kwa mhusika wa duka aliyekuwa akitafutwa.

Anaeleza kuwa suala la yeye kupatiwa maelekezo na Mamlaka ya uteuzi ni Jambo la kawaida

kwani miezi mitatu kabla ya siku ya tukio 9.2.2021 alipewa maelekezo ya kufanyakazi maalum na kubaini mtambo wa kutengeneza fedha bandia na kukamata fedha bandia sh,milioni 800 jijini Dar es salaam.

Sabaya anaeleza kuwa katika zoezi hilo alikuwa msimamizi mkuu ambapo Hata Gavana wa Fedha Prof Florian Luoga pamoja na aliye kuwa waziri wa Fedha hapa Nchini Dkt Philp Mpango ambaye kwasasa ndiye Makamu wa Rais wanalijua.

Sabaya amedai kuwa hajawahi kufikia katika duka la Shaahid Store na kupora kiasi cha sh, milioni 2,769,000 na kisha kumpiga human Jasim , Bakari Msangi, Salim hasani na Ally shabani na kuwatisha Kwa silaha na kwamba hamfahamu mshtakiwa mwenzake anayetajwa Kwa jina la Daniel Mbura na pia Silvester Nyegu hakuwa naye siku ya tukio.
 
hii kesi haina tofauti na ya Prof. Mahalu naye wakati alipo shitakiwa alidai alitumwa na aliye kuwa Rais wa awamu ya 3 Mkapa, kweli Mkapa walikuja na kumtetea Mahalau na Mahalu aliachiwa huru...
We Màtaga acha kujitoa akili,
Mimi nikikutuma uende ukauwe mtu,na ukakutwa eneo la tukio unauwa na ukakamatwa utasema Mimi ndiyo nilikutuma?
 
Katika kesi inayoendelea dhidi ya aliekuwa dc wa hai sabaya...ameieleza mahakama kuwa Yale aliokuwa anayafanya pamoja na operation zote yalikuwa ni maagizo kutoka kwa MAGUFULI na Dr mpango...na ametekeleza operation nyingi kupitia maagizo yao.
 
Duh.....Mungu anamuona lakini!

Amejitetea kiume sana

Makamu wa Rais Dr Mpango na DC mstaafu Dr Kihongosi watakuwa mashahidi wake muhimu kama katiba inaruhusu.

Rais mstaafu Mkapa aliwahi kupanda kizimbani kumtetea Prof Mahalu pale Kisutu!
Aulizwe dikteta Magufuli kama alitoa maelekezo hayo kwa DC badala ya ocd wa eneo husika
 
Back
Top Bottom