Utetezi wa Sabaya: Amwangushia zigo Hayati Magufuli na kudai Gavana Luoga na Makamu wa Rais Dkt. Mpango walifahamu

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
12,571
2,000
Uthibitisho atatoa tu.
Atautolea wapi?!!

Narudia, ushahidi ambao ungeweza kumsaidia ni wa kimaandishi but there's no way hizo nyaraka eti zinaweza kuelekeza `afanye aliyofanya!! Ndo maana nimesema nyaraka bila shaka zitakuwa na clean instruction lakini akapigiwa simu achukue "hatua zaidi when necessary"!
Kwa hiyo kama alipewa maagizo ya ziada yasiyo fuata sheria si ndo maana tunasema wote mtoaji na mpokeaji ni vululuvululu!!
Hiyo ni assumption, na hoja hapa ni kwamba, hata kama alipewa hayo maagizo bado msalaba utabaki kuwa ni wa kwake! Mosi, I doubt kama atakuwa na huo uwezo wa kuthibitisha! Pili, mamlaka ya uteuzi kwa nafasi yake ni ex-president ambae amefariki lakini hata kama angekuwa hai bado isingemsaidia!!
Halafu Sasa cha kujiuliza kama saa mbaya mmoja anakiri alipewa maelekezo yasiyofuata sheria kuwa akaumize watanzania jiulize ni wangap wamepewa maelekezo ya hivyo na ni watanzania wangapi wameumizwa na dikteta? Mkiona watanzania tunalilia katiba mpya ndo mjue twalia kwa mengi.....TUNATAKA KATIBA MPYA
Nijiulize mara ngapi wakati hilo tumelisema sana wakati wa uhai wa JPM?!

Narudia, tuna-overrate sana umuhimu wa katiba mpya pale tunapodhani kila tatizo solution yake ni katiba mpya na kudhani lau kama tungekuwa na katiba mpya tayari basi tatizo husika lisingetokea!

Katiba mpya ni muhimu sana, tena sana lakini tuna-overrate mno umuhimu wake!!!

Tena kama katiba mpya yenyewe ndo hizi za kufanya miongoni mwa wajumbe kuwa wabunge waliopo huku bunge lenyewe likiwa na over 95% CCM ndo wala usitarajie chochote cha maana!!

Padri au Sheikh hawatakiwi kumuogopa polisi au umma ili wasifanye maovu bali wanatakiwa kumuogopa Mungu kutokana na maandiko matakatifu yanavyosema!

Hata hivyo, nao bado ni miongoni mwa watenda maovu!!! Na wanapochelea kutenda uovu wanaogopa sana mamlaka za kidunia au jamii kuliko kuogopa makatazo ya maandiko takatifu!!

Hiyo ndo jamii tuliyonayo, na ndo maana, wakati Kenya inapata katiba mpya tuliisifia kweli kweli lakini hadi kesho uovu wa viongozi upo pale pale!
 

Intelligence Justice

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
1,456
2,000

c&p​

What to do when your boss asks you to do something unethical or illegal​

"It can feel like a lose-lose — but you should never comply with an illegal request."

"Most of all, know that your self-protection is paramount," Taylor explains. "Misdeeds, ....., illegal hiring and .... can plague you for a lifetime if you decide to engage — professionally, morally, and in extreme cases, legally."

Again, if you think (or know) the request is illegal, do not comply.
That was not a request rather an instruction and commanded order for compliance as such no discretion or option. The definition you have subscribed here does not apply probably in the non-impunity administrative business offices
 

Mgeni wa Jiji

JF-Expert Member
Jul 27, 2017
4,861
2,000
Mkuu,

Yule alikuwa mkuu wa wilaya kisiasa lakini kiutawala ni mjumbe wa kipenyo
Sasa Mkuu pote pote si kuna taratibu za kufuata?, Ninachokiona hapa ni mwamba kuna namna alikuwa nje ya taratibu za kisheria.

Hapa polisi wakienda kukamata mwalifu wanaweza kuiba pia na wakikamatwa watashitakiwa kwa wizi na kama wakijitetea kuwa walipewa oda na OCD kwenda kufanya waliyofanya watakuwa hawana tofauti na utetezi wa Mr. Ole Sabaya.

Huu ndio mtazamo wangu Mkuu
 

white wizard

JF-Expert Member
May 18, 2011
6,250
2,000
Wakili anae endesha kesi ya sabaya ana uwezo mdogo sanaa kisheria, yaan mpaka hapo kamtia hatiani mteja wake. Rasmi sabaya hachomoki sababu wakili uwezo mdogo. Hoja ilitakiwa Sabaya kuwapiga wale au kuiba vitu pale na uwezekano wa kutokuwepo kwenye eneo husika.
Sasa mkuu, mimi toka mwanzo nilishaona hata wakili wake,
Hawezi kutoka wilaya moja na kwenda wilaya nyingine bila mwenye mamlaka katika wilaya husika au eneo hilo kuwa na taarifa 'trust me' siri ndio iko hapo lakini kwa wataalama wakiruhusiwa kuunganisha vijiini vya matendo utaamini hicho ndico kilicho tokea huyui katoswa tu kwa sababu ya nyota iling'ara kupindukia kiasi cha kutisha mamlaka.

Kwa usalama zaidi hii kesi itagota na kulazimisha kutogota.......
Nitakuwa mtu wa mwisho kuliamini hilo!!kwani kuna wilaya moja hivyo alienda kukamata bangi, hadi ikawaletea shida , DC, DSO, OCD, na wao walilalamika japo kwa chini chini!!bangi nayo ni ya mtu kutumwa toka wilaya moja hadi nyingine?huyu alikuwa ameshazoea tu kwa misifa yake!!mimi nadhani hao waliotumwa kuungana naye, kama angewataja kwa majina, wangeweza kuwa mashahidi wake wazuri!!
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,485
2,000
Hujaeleweka vizuri,unajaribu kusema kama JPM alikuwa akimtuma Sabaya kufanya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha basi yawezekana na Mbowe alituma watu kufanya ugaidi??
Kwa hili pia nae SIRRO ajitafakari kiwango cha usafi wake, wala asijaribu kujitwisha u malaika
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
2,093
2,000
Watu wameshangaa kijana Ole sabaya kuwataja baadhi ya viongozi wa juu kwamba walielewa/ kumtuma kile alichokifanya na sasa ameshtakiwa nacho.

Binafsi nimekumbuka nasaa za IGP Sirro kwamba Freeman Mbowe ni binadamu siyo malaika anaweza kukosa kwa namna yoyote ile.

Mungu ni mwema wakati wote!
Hizo ni kesi mbili tofauti na hazifanani kwa vyovyote.Unalinganishaje kesi ya Sabaya mnyang'anyi/mporaji na Mh.Mbowe anayebambikiwa shtaka asilowahi kutenda?

Sabaya hawezi kuwa level ya Mh.Mbowe katika jambo lolote zaidi ya Utu.

CCM mjibuni Sabaya wenu,aliyoyanena mahakamani mbele ya kiapo ni kweli?

Kama ndivyo; CCM kitakuwa chama hatari sana na hakifai kubaki madarakani.

Mwenyekiti wenu alikuwa anawatuma watumishi wa umma kupora Mali,kuteka,kufilisi raia wema wa nchi hii?

Msihamishe magoli,Ni kweli kuwa Dr wa fedha na Professor wa benki wanafahamu hayo ya Sabaya?
 

crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,587
2,000
Hizo ni kesi mbili tofauti na hazifanani kwa vyovyote.Unalinganishaje kesi ya Sabaya mnyang'anyi/mporaji na Mh.Mbowe anayebambikiwa shtaka asilowahi kutenda?
Sabaya hawezi kuwa level ya Mh.Mbowe katika jambo lolote zaidi ya Utu.
CCM mjibuni Sabaya wenu,aliyoyanena mahakamani mbele ya kiapo ni kweli?Kama ndivyo; CCM kitakuwa chama hatari sana na hakifai kubaki madarakani.Mwenyekiti wenu alikuwa anawatuma watumishi wa umma kupora Mali,kuteka,kufilisi raia wema wa nchi hii?
Msihamishe magoli,Ni kweli kuwa Dr wa fedha na Professor wa benki wanafahamu hayo ya Sabaya?
Una point nzuri ila la Mbowe tuachie tu Mahakama. Mahakama zile zile zilizomtoa Mdude na kumrudishia Mbowe zile faini alizotozwa isivyo halali.
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
2,093
2,000
Una point nzuri ila la Mbowe tuachie tu Mahakama. Mahakama zile zile zilizomtoa Mdude na kumrudishia Mbowe zile faini alizotozwa isivyo halali.
Tunatakiwa kuwa wakweli,Mh.Mbowe siyo Gaidi na wanachofanya ni kumuadhibu kwa kutompeleka mahakamani.

Wanafahamu kabisa hana kosa hilo na shauri likifanyika kwa Haki anashinda.Hivyo wanahakikisha wanamfanyia Psychological Torture.

Tudai Katiba Mpya ya Wananchi ili kukomesha mateso kwa Watanzania.CCM hawajawahi kuwa na nia njema na Wananchi wa Tanzania zaidi ya matumbo yao.
 

Bwana PGO

JF-Expert Member
Mar 17, 2008
44,575
2,000
Watu wameshangaa kijana Ole sabaya kuwataja baadhi ya viongozi wa juu kwamba walielewa/ kumtuma kile alichokifanya na sasa ameshtakiwa nacho.

Binafsi nimekumbuka nasaa za IGP Sirro kwamba Freeman Mbowe ni binadamu siyo malaika anaweza kukosa kwa namna yoyote ile.

Mungu ni mwema wakati wote!
Acha ujinga please! Acha ujinga
 

crocodile

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,587
2,000
Tunatakiwa kuwa wakweli,Mh.Mbowe siyo Gaidi na wanachofanya ni kumuadhibu kwa kutompeleka mahakamani.Wanafahamu kabisa hana kosa hilo na shauri likifanyika kwa Haki anashinda.Hivyo wanahakikisha wanamfanyia Psychological Torture.
Tudai Katiba Mpya ya Wananchi ili kukomesha mateso kwa Watanzania.CCM hawajawahi kuwa na nia njema na Wananchi wa Tanzania zaidi ya matumbo yao.
Siwezi kuwa mkweli kwa kitu nisichokijua. Hiyo sentensi yako ya mwisho ni uthibitisho wa hoja zako zimefungamana na mlengo wako wewe binafsi wa kisiasa.

Kiufupi hauko neutral. Wapo watu wengi tu wameitumikia nchi hii with sweat and blood wakiwa huko CCM na binafsi nawajua.

Kwa suala la Mbowe, nitasubiri pande zote wanasemaje Mahakamani.
 

Felix

JF-Expert Member
Mar 9, 2014
843
1,000
Watu wameshangaa kijana Ole sabaya kuwataja baadhi ya viongozi wa juu kwamba walielewa/ kumtuma kile alichokifanya na sasa ameshtakiwa nacho.

Binafsi nimekumbuka nasaa za IGP Sirro kwamba Freeman Mbowe ni binadamu siyo malaika anaweza kukosa kwa namna yoyote ile.

Mungu ni mwema wakati wote!
Yote uliyo ongea hapo juu yanahusiana na matendo ya dhambi, sasa unamalizia na Mungu ni mwema nyakat zote ndoo nin sasa?

Ni sawa na Binti kutoa ushuhuda kanisani akisema "jaman shetani alinipitia nikapata mimba kwa kuzini, lakin mimba hiyo imetoka" arafu akamalizia Bwana Yesu asifiwe jaman...... Yaan asifiwe kwa lip!!!!
 

Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
2,093
2,000
Siwezi kuwa mkweli kwa kitu nisichokijua. Hiyo sentensi yako ya mwisho ni uthibitisho wa hoja zako zimefungamana na mlengo wako wewe binafsi wa kisiasa.

Kiufupi hauko neutral. Wapo watu wengi tu wameitumikia nchi hii with sweat and blood wakiwa huko CCM na binafsi nawajua.

Kwa suala la Mbowe, nitasubiri pande zote wanasemaje Mahakamani.
Bado umepita mle mle,sikuwa nakujibu wewe ila CCM wote wanaojaribu kuhalalisha na kutetea matendo ya Sabaya kwamba alitumwa kutenda uhalifu?Wanajitahidi kuihusisha kesi hiyo na ile ya kuchonga dhidi ya Mbowe.Je,Sabaya ni CHADEMA?Mbowe ni CCM?
Suala la Mimi kutokuwa Neutral halina mashiko kwenye suala lililopo mezani.Tusimamie Haki kutendeka kwa wote kwa kufuata Sheria.
Dawa ya kuitibu Tanzania dhidi ya majeraha ya utawala mbovu wa CCM wakitumia katiba mbovu iliyowapa mamlaka ya kutumia vyombo vyetu vya ulinzi ni kwa kudai Katiba ya Wananchi.Drawing Table ni Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba(Tume ya Warioba).Tuache porojo.
 

Lucky Star

JF-Expert Member
Jul 16, 2017
1,505
2,000
Hujaeleweka vizuri,unajaribu kusema kama JPM alikuwa akimtuma Sabaya kufanya ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha basi yawezekana na Mbowe alituma watu kufanya ugaidi??
Kwamba kwa JPM ameshtakiwa aliyetumwa, ila kwa Mbowe aliyetumwa ndiye kashtakiwa.
 

Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
35,670
2,000
Magufuli kuwa kibaka wa kuvunja maduka ya watu na kupora fedha haimfanyi Mbowe nae awe mhalifu.Unahitaji PhD kujua logic ndogo kama hii?!
 

nashicha

Senior Member
May 29, 2021
134
250
Aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya HAI ametufumbua macho kuwa wateule wa RAIS wanaweza kufanya walitakalo na kutoa visingizio kwa mamlaka za Uteuzi ili kukwepa mkono wa sheria ndio maana tunataka KATIBA mpya tuweze kuwawajibisha tuliowachagua
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom