Utetezi wa Nabii Daniel Shillah kwa Mwamposa ni kichekesho

Kamgomoli

JF-Expert Member
May 3, 2018
1,865
3,800
Huyu kijana sharobaro anaejiita nabii Daniel Shillah ametoa crip ya video akimtetea Mwamposa. dhidi ya tukio la maafa lililotokea Moshi.

Anasema kilichotokea ni jaribu la imani kwa Mwamposa kama majaribu mengine yaliyowakumba baadhi ya watumishi km Mwakasege kufiwa na mtoto wake pekee wa kiume, Zakaria na changamoto ya kupata mtoto pekee( Yohana mbatizaji) katika umri wa uzee, Ayubu kufiwa watoto wake wote pamoja na kupoteza mali yake yote.

Nataka Daniel Shillah atambue kuwa sifa ya Mungu ni kufanya mambo kwa haki bila kukosea.Nijuavyo mm km lingekua jaribu basi lingempata moja kwa moja yeye mwenyewe Mwamposa na sio kuua watu wasiohusika. Mwakasege alipatwa na jaribu la kufiwa mtoto yeye mwenyewe na sio muumini wake.Zakali alipata changamoto ya kuchelewa kupata mtoto yeye mwenyewe, Ayubu alipoteza watoto wake wote na mali zake zoote yeye mwenyewe mlengwa wa jaribu.

Je, kwenye hili la maafa ya Moshi Mwamposa kapoteza nini? Kapoteza kipi kilicho chake ? Hajapoteza mtoto, ndugu, mbuzi wala kuku wake tunaanzaje kusema hili ni jaribu lake? Namuuliza prophet Daniel Shillah anatoa wapi Credibility ,(nguvu) ya kusema hili ni jaribu la imani kwa Mwamposa? Hili si jaribu lake ndio maana alikimbia kurudi Dar.kuendelea na shughuli zinazomhusu.

Kwangu hili ni jaribu la wafiwa tuliowaona wakilia na kuomboleza kwa uchungu kwa kuwapoteza mama zao,dada na watoto wao. Kwenye msiba ule sikumuona ndugu yeyote wa Mwamposa akiomboleza. Ndugu zake wako mbeya wakiwa salama salimini, huku mali yake majumba,magari,na pesa zake zikiwa salama Dar es salam.

Kilichotokea maafa ya Moshi ni kafara km aliyofanya TB Jushua huko Nigeria mwaka 2014 ambapo zaidi ya watu 100 walipoteza maisha kwa kupolomokewa na jenga. Kisha T.B.Joshua akaja na visingizio vya kitoto eti kabla ya jengo kuanguka kuna ndege ilipita juu ya jengo.

Ifike wakati Watanzania tuseme enough is enough. Tumepigwa sn na hawa jamaa,tumewatajirisha sn hawa matapeli sasa inatosha. Kapobe akiwa katika ubora wake hakumaliza shida za Watanzania,akaja Babu wa Luliondo,Mzee wa Upako, Gwajima, Geodevie, nabii G.B.Malisa, na leo tunao Mwamposa na Nabii Suguye. Wote hawa toka waanze huduma zao wamezidi kuwa matajiri wakubwa huku waumini wao wakizidi kuwa mafukara wa kunuka. Ndio maana kuna siku mzee wa Upako alisema ukifa maskini ndani ya nchi hii ujue ni FALA. Alichokisema alimaanisha jinsi ilivyo rahis kuwarubuni Wtz na kupata hela kizembe zembe.

Sasa tuseme hatudanganyiki!! Full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wote hao wanaojiita manabii ni matapeli , wote wanatoka Kwenye vyama vya waabudu mashetani ,kazi YAO ni kutapeli watu kwa kuwahadaa akili zao

Ndio maana Huyo Shilla anajiita nabii lkn ana mafundisho tofauti na Tapeli mwenzake mwamposa

Na wote wana Frem/vioks (makanisa) kwa ajiri ya kutapelia wajinga wasiosoma maandiko

Kama Unasoma maandiko , Mungu hajawahi kutuma manabii tena. Kwa wakati mmoja wenye mlengo tofauti ,

Mungu alishatuma sana tu manabii kipind Israel imetoka utumwan babeli , Aliwatuma kwa wakati mmoja

Lakin hawakupingana. , wote ibada ni moja. ,mafundisho ni mamoja , taratibu ni mmoja

Maana wote wametumwa na Mungu mmoja ,

Ila hawa matapeli wapo kwa ajiri ya kuuza maji, mafuta ,keki, na lesso kwa Kudanganya yana upako ,

Cha ajabu eneo kama Sinza Mori, sinza kijiweni ,SINZA makaburini, SINZA madukani wamejazana kila uchochoro ,Na wanasema wametumwa na Mungu .
 
Hakuna jambo gumu kama kumtoa mtu mwenye imani kwenye imani yake...ni kama hivyo,hao wanaosali kwa Mwamposa hawawezi kuliona hili kama unavyoliona mimi na wewe....tayari wamechukulia hilo jambo kama jaribu la imani

#sAd​
 
Simkumbuki ni nani ili yupo kati ya uliowataja hapo juu alisema kwamba wachawi wanateteana wanapopata majanga nafikri akirejelea mchawi mmoja aliyedondoka Iringa juu ya kanisa halafu ikaja kudhaniwa mchungaji alitengeneza igizo! Na wao wamekuwa wale wale wakifanya jambo wanaungana! Wamekuwa kama Democrats na Republican wa Marekani!
 
Huyu kijana sharobaro anaejiita nabii Daniel Shillah ametoa crip ya video akimtetea Mwamposa. dhidi ya tukio la maafa lililotokea Moshi.

Anasema kilichotokea ni jaribu la imani kwa Mwamposa km majaribu mengine yaliyowakumba baadhi ya watumishi km Mwakasege kufiwa na mtoto wake pekee wa kiume, Zakaria na changamoto ya kupata mtoto pekee( Yohana mbatizaji) katika umri wa uzee, Ayubu kufiwa watoto wake wote pamoja na kupoteza mali yake yote.

Nataka Daniel Shillah atambue kuwa sifa ya Mungu ni kufanya mambo kwa haki bila kukosea.Nijuavyo mm km lingekua jaribu basi lingempata moja kwa moja yeye mwenyewe Mwamposa na sio kuua watu wasiohusika. Mwakasege alipatwa na jaribu la kufiwa mtoto yeye mwenyewe na sio muumini wake.Zakali alipata changamoto ya kuchelewa kupata mtoto yeye mwenyewe, Ayubu alipoteza watoto wake wote na mali zake zoote yeye mwenyewe mlengwa wa jaribu.

Je kwenye hili la maafa ya Moshi Mwamposa kapoteza nini? Kapoteza kipi kilicho chake ? Hajapoteza mtoto, ndugu, mbuzi wala kuku wake tunaanzaje kusema hili ni jaribu lake? Namuuliza prophet Daniel Shillah anatoa wapi Credibility ,(nguvu) ya kusema hili ni jaribu la imani kwa Mwamposa? Hili si jaribu lake ndio maana alikimbia kurudi Dar.kuendelea na shughuli zinazomhusu.

Kwangu hili ni jaribu la wafiwa tuliowaona wakilia na kuomboleza kwa uchungu kwa kuwapoteza mama zao,dada na watoto wao. Kwenye msiba ule sikumuona ndugu yeyote wa Mwamposa akiomboleza. Ndugu zake wako mbeya wakiwa salama salimini, huku mali yake majumba,magari,na pesa zake zikiwa salama Dar es salam.

Kilichotokea maafa ya Moshi ni kafara km aliyofanya TB Jushua huko Nigeria mwaka 2014 ambapo zaidi ya watu 100 walipoteza maisha kwa kupolomokewa na jenga. Kisha T.B.Joshua akaja na visingizio vya kitoto eti kabla ya jengo kuanguka kuna ndege ilipita juu ya jengo.

Ifike wakati Watanzania tuseme enough is enough. Tumepigwa sn na hawa jamaa,tumewatajirisha sn hawa matapeli sasa inatosha. Kapobe akiwa katika ubora wake hakumaliza shida za Watanzania,akaja Babu wa Luliondo,Mzee wa Upako, Gwajima, Geodevie, nabii G.B.Malisa, na leo tunao Mwamposa na Nabii Suguye. Wote hawa toka waanze huduma zao wamezidi kuwa matajiri wakubwa huku waumini wao wakizidi kuwa mafukara wa kunuka. Ndio maana kuna siku mzee wa Upako alisema ukifa maskini ndani ya nchi hii ujue ni FALA. Alichokisema alimaanisha jinsi ilivyo rahis kuwarubuni Wtz na kupata hela kizembe zembe.

Sasa tuseme hatudanganyiki!! Full stop.

Sent using Jamii Forums mobile app
Crip = Clip
 
Hawa Manibii Feki hawa kwa kweli wataendelea kuwatafuta watanzania wajinga maana wanasema wajinga ndiyo waliwao,

Manabii hawa feki huwa wanawatengeneza watu kwa muda mrefu sana kwa ajili ya kufanya maigizo kwenye mahubiri feki ili kuwaaminisha mamia ya wanaofulika kwenye mahubiri yao kuwa kuna uponyaji wa kweli kumbe ni watu wanatengenezwa,wanalipwa pesa nzuri ili kuwavutia watu,ama kweli wajinga nidyo waliwaoooooooooooo
 
Back
Top Bottom