UTETEZI: 2013 Nilikuwa na tani 4.6 za Korosho ila sijawahi kupanda hata mche wa Korosho

impongo

JF-Expert Member
Feb 18, 2015
8,733
7,610
Nimekuwa nikisikia uhakiki wa wakulima fake wa Korosho kunyanganywa Korosho baada ya kukosa kuonyesha mashamba wanayomiliki hii sio haki.

Mwaka 2013 Nilikuwa na rafiki yangu (marehem kwa Sasa) katika wilaya ya Ruangwa, wakulima walikuwa wakimfuata kuomba ufadhiri wa pesa ya dawa kwa makubaliano ya kutoa Korosho kipindi Cha mavuno alinisihi kupitia yeye nilitoa pesa kwa wakulima 45 katika vijiji vya Nangurugai,Machang'anja, Njenga na chikwale vilivyopo kata ya Narung'ombe.
Baada ya mavuno nililetewa Korosho ili walipe Deni ninalodai kiasi Cha kilo 4640.

Je ingekuwa 2018 si ningenyanganywa Korosho nilizopata kihalali Tena kwa kuwawezesha wanainchi waliokuwa hawana uwezo wa kupata pembejeo?

Serikali waacheni wenye Korosho wasio na mashamba wamezipata kihalali na wao ndio wawezeshaji wakubwa wa kutoa pembejeo kwa wakulima kwa muda muafaka mnawaweka wakulima ktk wakati mgumu mwakani hawatapata pembejeo na Serikali mara nyingi mnapeleka pembejeo muda ukiwa umekwisha au mahitaji kidogo ya kinachotakiwa.

Ahsante
 
Hiyo ndiyo ile niliyosoma kwenye History "Barter Trade" ...! Kwanini wasikulipe pesa? ukiona hivo bado unaendelea kufanya hiyo biashara Barter trade na mwisho wa siku utawaambia wakupe dhahabu ili uwape pembejeo
 
Hiyo ndiyo ile niliyosoma kwenye History "Better Trade" ...! Kwanini wasikulipe pesa? ukiona hivo bado unaendelea kufanya hiyo biashara Better trade na mwisho wa siku utawaambia wakupe dhahabu ili uwape pembejeo
Hivi Kuna mtu asiyetaka pesa yake ilete faida
Una mpa mtu pesa miezi miine lazima utake faida
 
Wakulima hewa
Walimu hewa
Mishahara hewa
Madaktar hewa
Mishara hewa duuh
This is Tanzania brother.
Yajayo yanafurahisha
 
Hivi Kuna mtu asiyetaka pesa yake ilete faida
Una mpa mtu pesa miezi miine lazima utake faida
Kwani tatizo faida? kwanini iwe goods for goods? why asichukue hela mara baada ya mkulima kuuza mazao yake?
 
Mbona langu ni dogo tu mkuu. Unatembea mbereeee ukiwa kifua mbele ikiwa upo 100% sure hakuna kosa mahala. Nilikuwa najaribu kuweka kumbukumbu sawa
 
Kwani tatizo faida? kwanini iwe goods for goods? why asichukue hela mara baada ya mkulima kuuza mazao yake?
Kuchukua pesa ya riba siyo sahihi kwangu ndiyo maana Nilikuwa nachukua mazao !!
Hivi ulishawahi kufanya biashara??
 
Back
Top Bottom