Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,882
Mambo ni Moto
Katika sakata linaloendelea linalomkabili Ndugu Lengai Ole Sabaya, utetezi wake unaacha watu midomo wazi.
Mimi sio mwanasheria lakini Kwa akili ndogo tuu niliyonayo namuona Ole Sabaya na mawakili wake wakishindwa kutoa utetezi wenye mantiki.
Utetezi wa Sabaya kuwa alitumwa na Wakuu wake wa kazi waliomteua kufanya Uhalifu ni utetezi wa kijinga Sana ambao mtu mwenye akili asingeweza kuusema Mahakamani.
Kusema alitumwa ni dhahiri anakiri kosa kuwa alifanya, na moja Kwa moja anajitia hatiani.
Ole Sabaya Kiujasusi tayari ameshakosa Weledi katika Kazi yake. Anaposemwa alitumwa na Rais Magufuli ambaye Kwa sasa ni Marehemu, Kwa kazi maalumu, hii inamaanisha kuwa Sabaya yupo katika mfumo wa ujasusi iwe direct au indirectly.
Hivyo Jambo la kwanza kwenye majukumu yake lilipaswa kuwa Siri ndipo mengine yafuate
Moja ya kanuni za kazi maalumu ni siri, hasa kazi maalumu/operations zisizokuwa na majina na zisizoundwa kisheria.
Operations ambazo hazifuati kanuni Rasmi, ni unapigiwa simu na unatekeleza.
Operations za hivi, anayetumwa anapaswa azifanye Kwa weledi pasipo kuleta athari mbaya ambazo zitamtia hatiani, kwani zimtiapo hatiani yeye ndiye atahusika 100% katika adhabu.
Kijasusi, mtu anapopewa kazi maalumu hata akikamatwa hapaswi kusema ukweli kuwa alitumwa na wakubwa wake, hapaswi kuwataja waliomtuma, anapaswa kutumia mbinu zingine za kujihamu au kuficha siri.
Sabaya Kama alitumwa na Hayatti Magufuli, hii ilimaanisha taasisi ya Urais ilikuwa inajua misheni hizo, hivyo hakupaswa ajitetee kuwa alitumwa na Rais kufanya Uhalifu kwani Kwa kufanya hivyo anamdhalilisha Hayatti Magufuli na Taasisi ya Urais ya wakati huo.
Kama ni kweli alitumwa, basi angekaa kimya na kujitetea Kwa namna zingine, alafu Kwa vile alitumwa na taasisi ya Urais, basi mabosi wake Kwa vile wengine wapo na wanatambua misheni hiyo, wangetafuta namna ya kumnasua. Lakini sio kuwataja, Kwa kuwataja ni tayari ameshavujisha Siri pasipo yeye kujua.
Sabaya pasipo kujua, kauli yake unazidi kuwapa nguvu Wale wote waliokuwa wakiituhumu serikali na watu wasiojulikana.
Kwa kifupi, Sabaya amekosa Weledi.
Hata Kama akitoka basi tayari ameshavujisha Siri za wakubwa wake, na Hana sifa za kuwa mtu wa vitengo Kwa mambo ya kiusalama.
Ilimpasa afe kiume. Akaze Tai shingoni.Mabosi zake ndio wamnasue. Lakini utetezi wake bado unamuweka pagumu zaidi.
Robert Heriel