Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
- Thread starter
- #21
Tanganyika haikuwahi kuwa zao la watu wa Tanganyika; vinginevyo wazee wasingetaka uhuru kutoka kwa Mwingereza. Tanganyika ni zaidi ya nchi au mipaka au jina. Labda watu warudi nyuma na kujifunza historia yetu kidogo. Tanganyika ilizaliwa katika misingi yake ambayo mtu aliposema "Mtanganyika" ilijulikana anamaanisha nini. Labda watu mrudi na kusoma hotuba za kuelekea Uhuru, ya siku ya Jamhuri na Hotuba ya Nyerere Umoja wa Mataifa baada ya maadhimisho ya Uhuru. Misingi ambayo ilikamilika katika Tanzania. Tanzania ni zao la njozi ya Tanganyika.
Inanishangaza watu wanatukuza "Tanganyika" lakini hawataki kuangalia misingi ya Tanganyika ilikuwa nini na wengine hata hawajui ilikuwa ni nini. Huwezi kuwa na Tanganyika bila kurudia misingi yake! Ni sawa na mtu ambaye anataka kurudia nyumba aliyokuwa nayo lakini bila kurudia alipoijengea. Aidha utakachopata sicho - japo inaweza kufanana na ukaita ni chako. Tanganyika na Tanzania haviwezi kutenganishwa. Hata bila Zanzibar - Tanzania inaweza kuwepo kwa sababu Tanzania ni zao la Tanganyika.
Kinyume na watu wengi wanavyosema wakati wa Muungano Tanganyika haikupoteza utambulisho wake, iliukamilisha na inapaswa kuendelea kuukamilisha kwa kuelekea Shirikisho la Afrika ya Mashariki. Kuirudia Tanganyika ni kurudia kitu ambacho tulikiacha na kutaka kurudia nyuma ya historia. Ndio maana huwezi kuwakuta wazee waliofahamu uhuru na harakati za uhuru wanalilia Tanganyika - kama wapo wachache tu.