Utenzi wa Tanzania - Miaka Hamsini ya Uhuru (Beti 100) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utenzi wa Tanzania - Miaka Hamsini ya Uhuru (Beti 100)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Dec 5, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Utangulizi


  Nilipata wazo la kuandika utenzi huu* kuanzia mwaka jana. Nilikuwa nimekusudia kuandika Utenzi wenye beti 1000 kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Lakini katika uvivu wangu na mihangaiko ya dunia nimejikuta nimeishia kwenye hizi beti 100 za utenzi huu wa Tanzania. Maadhimisho ya miaka hamsini ya Uhuru ni maadhimisho siyo ya mipaka ya nchi, siyo ya jina na kwa hakika kabisa siyo maadhimisho ya kupita kwa muda. Ni maadhimisho – naamini- ya utu wetu.

  Kwamba, katika miaka hamsini iliyopita tumeweza kufanya kile ambacho hakikuwahi kufanywa kwa miaka 2000 iliyopita katika eneo letu. Yaani, kuwaunganisha watu watu wetu wote, chini ya mipaka ile ile, wakiwa huru na haki sawa. Katika utenzi huu nimeelezea jinsi eneo letu lilivyojulikana kama Azania katika masimulizi ya Wagiriki au kama Zenji kwa Waarabu na wakati mwingine kuhusiana na majina ya maeneo ya Kushi na Nubia katika Biblia. Kama jamii ya watu tumepitia mambo karibu yote ambayo yamepitiwa na jamii nyingine za dunia. Kuanzia maisha ya ujima, utumwa, vita, mapigano, na hatimaye uhuru.

  Kumbe basi historia yetu haina tofauti sana na historia ya jamii nyingine za watu ambazo zimesimama katika pande za dunia. Unaposoma utenzi huu ni matumaini yangu utakufanya ujisikie fahari kuwa wewe kama vile mimi ni zao la historia hii. Tumefungamanishwa na historia kiasi kwamba haiwezi kufunguka. Mbele yetu wametutangulia wengi katika historia ambao nao walisimama kutambua utu wao na kuudai mbele ya watawala wa zama zao. Ni hiki ndicho tunachokifurahia kwamba leo tuko huru kuwa watu sawa na wengine – kwa kila hali.

  Ni utu wetu ndio ulikuwa msingi wa kupigania uhuru wetu na unatakiwa kuwa ndio kiini cha kushangilia uhuru huo. Ni vipi tumetumia uhuru huo kuinua utu wetu hili ni swali jingine ambalo kizazi chetu kama kizazi kinachokuja kitahiji kujibu. Je, mambo tunayoyafanya na kufanyiana yanalingana na utu huo? Je, tunatendeana kama watu wenye utu katika sera, sharia, mipango, na mambo tunayoyafanya? Utenzi huu basi ni kukumbushia utu wetu.

  MMM Disemba 5, 2011


  SIFA KWA MUNGU!
  1. Ee Mola ninakujia
  Kwako ninasujudia
  Sifa nakurudishia
  Utukufu enzi pia  2. Ewe uliye Jalia
  Mmiliki wa Dunia
  Hukumu ni zako pia
  Na adhabu ya Jehania  UTANGULIZI  3. Kalamu naishikia​
  Naandika beti mia​
  Kwa tungo nazipangia​
  Zinasifu Tanzania


  4. Ni tungo za historia​
  Ni wapi tulianzia,​
  Na wapi tumefikia,​
  Lengo ni kukumbushia


  5. Nataka kusimulia ​
  Kwa hizi tungo mia ​
  Huku nawahisabia ​
  Mpaka zitapotimia


  6. Tangu walipoingia ​
  Wageni toka Asia ​
  Na wale wa Yuropia ​
  Makabila yalohamia


  7. Ishirini na mia, ​
  Makabila ya Tanzania, ​
  Makubwa madogo pia ​
  Hapa nawasimulia


  8. Na beti zikitimia ​
  Zikifika hizo mia ​
  Kalamu nitaachia ​
  Lengo nitalifikia.


  9. Ujumbe nauanzia ​
  Wa hizi beti mia ​
  Kwa kina nitagusia ​
  Ni wapi tulianzia

  ...

  Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
  Disemba 5, 2011
  Email: mwanakijiji@jamiiforums.com
  Facebook: "mimi mwanakijiji"

  Ω ​
  NB:* - Utenzi huu unaweza kuchapwa popote na mahali popote bila kubadilisha maneno kama sehemu ya maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru. Haki zote za kuunakili zimeruhusiwa bila kubadilisha jina la mtunzi au utenzi wenyewe; lazima kuweka maelezo ya mawasiliano kama yalivyo.
   

  Attached Files:

 2. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Sasa ndugu yangu Mwana kijiji mbona Tanzania haijawahi kupata uhuru.

  Wazungumzia Tanzania ipi?
   
 3. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  [​IMG] ngoja niendele kuisoma kwa umakini kabla sijaijibu
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ukisoma vizuri utaona nazungumzia ipi.
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Dec 5, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,326
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  I sense the call for Tanganyika is coming! Where does it come from???
   
 6. Mkuu wa chuo

  Mkuu wa chuo JF-Expert Member

  #6
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,253
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  nimekubali :poa
   
 7. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #7
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Awali ya yote

  Thalatha inamaanisha tatu na sio thelathini
  Aroba (arba) inaamisha nne na sio arobaini (arbaini)
  kama ambavyo tisa inamaanisha tisa na sio tisiini

  Pili, ningeomba kuelezewa huu 'utenzi', unafuata kanuni gani za uandishi wake?
   
 8. M

  Megawatt B JF-Expert Member

  #8
  Dec 5, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Wewe Mwanakijiji nilikua nakuamini sana, lakini hili...... HAPANA. Hapa unazungumzia Tanzania bwana, Tanzania haijapata uhuru na wala haijafikisha miaka hamsini(50) usituzuge acha kufuata mkumbo
   
 9. U

  UMMATI Member

  #9
  Dec 5, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uhuru wa Tanganyika sio TANZANIA!
   
 10. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #10
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hongera kwa beti mia
  sote tumejionea
  kusoma nimepania
  punde nitachangia
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Tanzania haijawahi kutawaliwa na haina siku ya uhuru bali ni siku ya Muungano tu, atakaepotosha ukweli huu amelaaniwa duniani mpaka mbinguni.
  Nawapenda sana Tanganyika Law Society walijiondoa kwenye unafki huu tangu awali.
   
 12. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #12
  Dec 5, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Nimeishia hapa. Siwezi kuendelea kusoma beti 100 za uhuru wa tanzania. Nitaweza kusoma au hata kuimba beti 10,000 za Tanganyika baada ya uhuru wa kweli tutakapoachana na Zanzibar. Anza kutunga.......
   
 13. s

  semako Senior Member

  #13
  Dec 5, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania haijapata uhuru wewe
   
 14. M

  MAMENGAZI JF-Expert Member

  #14
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Beti nimemalizia
  yote nimejionea
  asante kwa historia
  na mengi kujifunzia

  hongera kwa kuyaona
  makosa yalotendeka
  nchi mbili kuungana
  na mbili kupatikana

  Tanganyika kupotea
  ndilo linatusumbua
  muungano twakosoa
  kwani unatuumbua

  Kutenda kosa si kosa
  kosa kurudia kosa
  tuyakosoe makosa
  haki tusije ikosa
   
 15. Borakufa

  Borakufa JF-Expert Member

  #15
  Dec 5, 2011
  Joined: May 26, 2011
  Messages: 1,503
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Aaah! amechanganya historia ya tanganyika na zanzibar huyu mie nimemwelewa hivyo! lakini ameskip! 9.december ni uhuru wa nchi ipi! mwanakijiji umenunuliwa? maana katika utenzi huu unaonyesha kuwa kwa jinsi mwingiliano wa maisha wakati wa ukoloni tulitakiwa kuwa tanzania since before sivyo? Huoni hii ni history ya kufikirika hii! ebu tengeneza utenzi kama huu specific kwa Tanganyika sawa mkuu usibadilike kaka!
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #16
  Dec 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Hivi Tanganyika ni nchi ya nani? Kwanini watu wanalilia nchi ya mkoloni?
   
 17. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #17
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,275
  Trophy Points: 280
  Labda ungetusaidia kutuonesha Tanzania bara iko wapi nadhani huu utata wote utaisha. United Kingdom inaonesha kila kitu na kila kisiwa status yake,kwa nini sisi tunakuwa matapeli?
   
 18. Lenana

  Lenana JF-Expert Member

  #18
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 422
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  aliyekuambia Tanganyika nchi ya mkoloni nani!?
  :spy:
   
 19. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kwa mara ya kwanza unisamehe ndugu......napata taabu kutamka hili.......lakini nahisi swali hili.....lakini nisamehe kwa sababu nakuheshimu....ila hata kama mkubwa hajambi......akikosea lazima tumseme.......katika hili.....UMETUMIA MASABURI KUPOST.

  Tanganyika ni nchi yangu na si nchi ya mkoloni. Kama ingekuwa nchi ya mkoloni isingesubiri hadi 1964 kusilimu au kubatizwa na kuitwa Tanzania
   
 20. Crucifix

  Crucifix JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 1,618
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Na mimi naongezea
  Beti moja kujazia
  Tanganyika kurejea
  Dua ninaiombea
   
Loading...