Utenzi wa Kumuenzi Mwalimu Nyerere.

Oct 9, 2012
39
23
HII NIMEITOA FACEBOOK JAMANI, nikaona nanyi msome, mie nimeupenda sana
huu utenzi!!!!..........................

Uko wapi baba, mwanao mimi nakutafuta/
Ni miaka imepita enzi za baiskeli mpaka sasa kuna Guta/
Njoo upesi baba uwaone wezi wanatupa suluba kimyakimya bila vita/
Ningekutajia majina sema tu moyo unasita.
Wale uliowaacha vijana sasa ni wazee mfano Samweli Sita.
Wale wabunge wako watiifu hawapo tena sasa kuna mafisadi/
Wanataifisha ardhi yako tena hasahasa migodi/
Kisha wanapewa heshma kwa kuchongewa jembe la Gold/
Tuliyemtegemea mtafanana kumbe naye goigoi/
Amekufanana jina tu ila kimatendo bora Toi/
Njoo maramoja baba uturejeshe kwa wakoloni/
Hapa kwenye uhuru tunaish kama motoni/
Sera ya kujuana inawatesa wanazuoni/
Hata waliosoma sana ajira hivi sasa hawazioni/
Yule mwenye kitambi alituletea shule za kata/
Mwenzake amekuja hana jipya ujinga mtupu amepakata/
Heri tumpe faida mchuuzi tuvujishe hli pakacha/
Hawa wapinzani na watawala nao wanafanana kama mapacha/
Bunge lako tukufu sasa wanaimba kwasakwasa/
Wanapeana mipasho waziwazi wanadai hzo ni siasa/
Sheria zimebadilika sasa askari ruksa kufanya mauaji/
Thubutu kuwakemea nawe uende na maji/
Mgambo wa jiji kamgeuza machnga mtaji/
Ushoga na uchangudoa biashara halali katkat ya jiji/

*LEO TUNAMKUMBUKA"
 
Back
Top Bottom