Utengenezaji wa Sarafu(Coins) Mpya

Kabengwe

JF-Expert Member
Oct 20, 2009
240
47
Nimekuwa nikiwaza kwanini BOT hawatengenezi sarafu mpya za sh 5/=, 10/=, 20/= ambazo zitakuwa ni ndogo kuliko sarafu za sh 50/= na 100/=

Sarafu za sh 5/=, 10/= na 20/= zilizopo kwa sasa hazitumiki vijijini ambako kuna watanzania wengi na wengi wao ni wakulima. Kwa hyo, kwa kiasi kikubwa mfuko wa bei huanzia huko kwani vitu haviwezi kuuzwa kwa sh 5/=, 10/= au 20/= tena. Vitu vinauzwa kuanzia sh 50/= na vinaruka mpaka sh 100/=

Mathalani, Ukitaka kununua embe au chungwa kipindi cha msimu vijijini, nilazima utauziwa shillingi 50/= au 100/= coz hizo ndo fedha za chini kabisa zinazotumika huko, Muuzaji hataweza kuuza chini ya hapo hata kama anatamani kuuza kwa sh 30/= . Sasa hilo tunda mpaka lije kufika dar litakuwa linauzwa bei gani?!
The same applies to every food stuff kutoka vijijini

Kitu ambacho kinaweza kufanyika kwa sasa ni kutengeza sarafu mpya za sh 5/=, 10/= na 20/= na kuondoa zile za zamani ambazo hazitumiki kabisa vijijini na kwenye baadhi ya miji! Coz tayari imeshajengeka dhana kuwa hazikubaliwi popote!

Nadhani huu unaweza kuwa mwanzo mzuri wa kukabiliana na mfumuko wa bei

Waelewa wa uchumi naomba mnikosoe kama nimechapia!

Ila kama niko sahihi, unafikiri ni kwann wachumi wetu hawalioni hili?!
 
I think this is good thinking, for a non-economist!! Ila naomba ubadili sehemu ulizoandika "mfuko" wa bei kuwa "mfumuko"
 
Ukitaka kuuza kwa bei ya chini, unauza kwa mafungu! Mathalani, fungu moja lenye maembe 20, kwa shilingi mia (i.e. kila embe moja shilingi tano).

Hata hivyo nakubaliana na hoja yako ya kuongeza wingi wa sarafu hizi kwenye mzunguko wa fedha.
 
Back
Top Bottom