Utengenezaji wa sabuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utengenezaji wa sabuni

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Kamongo, Feb 13, 2011.

 1. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Mimi ni mtumishi wa uma,nimejaliwa kupata mtaji kidogo,nataka nianzishe kiwanda kidogo cha kutengeneza sabuni,je ni vitu gani vinahitajika na soko lipo la bidhaa hiyo?hapa tz
   
 2. A

  Ahungu Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu Mjasiriamali matarajiwa!
  Biashara yeyote ni upatikanaji wa "soko" - yaani wanunuzi. Ni kazi yako kufanya utafiti wa kuwepo kwa "soko". Wengine hawatakusaidia sana. Pili, unataka kutengeneza sabuni ya aina gani? - Kwa maana kulingana na matakwa ya "soko" lako! Sabuni ya maji, unga, manukato (na ya aina gani?) na maswali mengi. Je, unaijua stadi ya utengenezaji sabuni? Kama la.
  soma vitabu, ingia kwenye websites kama - "Instructables" au tembelea watengenezaji sabuni wadogo na wakubwa! Nipigie tafadhali - 0784360034

  Nakutakia mafanikio mema.

  RA
   
 3. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,189
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sabuni ipi?

  Liquid, Powder au Miche ya Sabuni
   
 4. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  mimi nataka kujikita ktk utengenezaji wa sabuni za miche na za kuogea ila sina utalaamu,nimesikia sido wanafundisha,pia nataka kujua machine za kutengeza sabuni zinapatikana wapi
   
 5. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,358
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Mkuu ninauzoefu wa kutengeneza sabuni za mi
  che. soko lipo kubwa mmno.kwani viwanda havikidhi mahitaji ndio sababu bado tuna import sabuni.
  Machine ya kutengeneza sabuni -Ploder ni milioni7,ya kukata chips milioni1 ,na clutcher ya kupikia sabuni ni around 3millioni,ila unaweza kuanzia kupika ktk mapipa ya lita200(siyo kazi rahisi kutumia mapipa)
  hivyo unahitaji around milioni11 kwa ajili ya equipment.

  tatizo ni Mali Ghafi. mafuta ya kutengeneza sabuni yanatoka nje ya nchi ,hivyo yanaagizwa na viwanda vikubwa ,viwanda vidogo wananunua kwa dili kutoka kwa madalali.
  kuna mafuta ya mise yanatoka mbeya,na kigoma haya ni rahisi ila kama upo dar gharama ya usafiri ni kubwa.\

  competitors
  Sabuni ya kiwanda kidogo huwa na ubora zaidi ktk maji ya chumvi/kisima ambayo ndio maji yanayotumika na watanzania wengi,sabuni za viwanda vikubwa huwa zimechujwa sana(highly refined and processed oils)hivyo hazifai ktk maji ya visima.
  watengeneza sabuni za mikono kutoka kigoma huwa wanamwaga sabuni nyingi ktk soko la DAr ,wanarudi a month later kuchukua pesa,hivyo jiandae kushindania nao.
  Viwanda vikubwa sabuni zao zinapendwa mjini e.g Dar,Arusha na Mwanza ambako kuna maji ya bomba,hivyo tarajia soko la mikoani na vijijini,
  ili uwafikie hawa wateja inabidi uunde distribution network ya whole sellers,pale manzese kuna maduka ya wapemba ya whole sale ukiwapelekea mzigo wanakulipa hapo hapo,wao huwa wanawauzia watu wanaopeleka bidhaa za maduka mikoani.e.g pruduct yangu nilikuwa siioni madukani in Daresalaam.nilipodadisi nikagundua ipo very popula in Kibaigwa dodoma.so nikisupply mzigo jamaa wanaotoka dodoma hawanunui kitu kingene zaidi hiyo sabuni.
  ------------------------
  kama utafungua kiwanda mitaani na siyo ktk industrial zone e.g pugu road,epza :)
  jinpange kupambana na TFDA,bora ya TBS
  Afisa biashara
  TRA
  mwen
  yekiti wa serikali za mtaa.

  Packaging ya product yako ni muhimu sana,ndiyo maana wachina wanauza vitu vyao kwa wingi wao wanajua packaging and presentation nzuri za quality.
  kwa sabuni ya mche ni kutengeneza mabox.nenda pugu road kiwanda kinaitwa Commercial printers wao wanabei nzuri na ni wazoefu kwa ajili ya SME s wenye viwanda vidogo.watakufanyia design ya box,inabidi uende na miche yako ili wawe na uhakika wa vipimo vya carton.

  kwa ushauri zaidi wa michanganuo ya biashara na faida muone BABALAO atakushauri vizuri zaidi mpaka jinsi ya kupata mkopo. :)
   
 6. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #6
  Feb 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,415
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  Kuna hawa jamaa wa Tanzania Business Creation Company wanatoa semina kwa wajasiriamali wanaotaka kumiliki viwanda vidogo vidogo. Mafunzo wanayotoa ni pamoja na utengenezaji wa:
  sabuni za kufulia na kuogea
  sabuni za maji
  shampoo za kila aina
  dawa za viatu
  bleaching agent
  petrolleam jelly etc.

  waweza wasiliana nao kwa simu 0715851665 / 0784851665 / 0765871665
  Pia wanayo mitambo ambayo wanatengeneza wenyewe na kuiuza kwa ajili ya kutengenezea sabuni za miche. Wako Sinza Mori
   
 7. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #7
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,358
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  thanks,je hizi semina wanazotoa ni kiasi gani kuattend?
   
 8. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #8
  Feb 14, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,415
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  Sina uhakika na gharama zao. Jaribu kuwapigia watakueleza.
   
 9. Sita Sita

  Sita Sita JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 1,189
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu dawa za viatu ndo nini?
  Hawa jamaa ni waswahili wenzetu au wachina?


   
 10. L

  LAT JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,524
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  kweli wachina kiboko..kumbe kuna mpaka mayai ya kichina ...watu wamenunua egg chops na kababu zilizotegenezwa na mayai ya kichina pale royal bakery kawe matokeo yake matumbo yamewauma na wameendesha vibaya sana
   
 11. MIUNDOMBINU

  MIUNDOMBINU JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 450
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  mkuu new mzalendo umetoa ushauri mzuri sana kwa huyu ndg yetu.kweli unauzoefu ktk eneo hilo.big up bro.
   
 12. Nyenyere

  Nyenyere JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,415
  Likes Received: 1,843
  Trophy Points: 280
  Kaka hiyo no shoe polish. Inavyoelekea ni waswahili wenzetu na ni mradi wa kanisa liitwalo Word Alive Church lililopo Sinza Mori.
  Wanauza mtambo wa kutengeneza sabuni za miche unaotoa miche 150 pamoja na mishumaa 500 kwa siku. Pia watakuunganisha na watengenezaji mitambo wa china na kukusaidia kuagiza.
   
 13. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,358
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  thanks for u r recognition,nigongee senks basi :)
   
 14. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru wote mliotoa michango yenu
   
 15. K

  Kamongo JF-Expert Member

  #15
  Mar 7, 2011
  Joined: Mar 20, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Je machine za kutengeneza sabuni hapa tanzania zinapatikana wapi?
   
 16. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #16
  Mar 7, 2011
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mkuu asante sana kwa maelezo. Ni muda mrefu nimekuwa nikijaribu kutengeneza sabuni lakini nashindwa, huwa zinatoka zikiwa ngumu sana na zinachubua mikono au wakati mwengine zinakuwa laini sana, nikitafuta formula za utengenezaji wa sabuni ktk mitandao hazinipi ratio ya kiasi cha mafuta na sabuni, mwishowe nikaamua kuachana na mradi wa kutengeneza sabuni. Lakini kwa maelezo haya nimehamasika na nafikiria kuanzisha tena, nitakutafuta wakti utakapowadia
   
 17. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #17
  Mar 8, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,358
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  karibu tutashare knowledge :usa2:
   
 18. A

  Akiri JF-Expert Member

  #18
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,440
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Asante sana ndugu umetusaidia wengi .thankx in advance
   
 19. m

  massoyevod New Member

  #19
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utengenezaji wa sabuni
  mimi naomba mnipatie ufahamu hasa wa malidhafi zitumikazo kutengeneza sabuni za miche na unga,ili niweze kuanzisha utengenezaji wa sabuni (Homemade soap )
   
 20. m

  massoyevod New Member

  #20
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli mmetupa elimu ya kutosha kwenye huu utengenezaji wa sabuni,labda kutaka kufahamu zaidi naomba mnielimishe kuhusu malighafi zinazotumika na kiasi gani nitumie ili niweze kutengeneza sabuni ya mche na unga kwa matumizi ya nyumbani.utengenezaji wa ngu ni mdogo sana (Homemade soap)
   
Loading...