Utendee Haki Moyo Wako

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Leo nimekuja na mada nyingine, kama kawaida ni mada nzuri itakayokupa ufahamu mpya juu ya maamuzi yako yahusuyo mapenzi. Hivi ni kweli kwamba unautendea haki moyo wako? Mpenzi uliyenaye unampenda au unajilazimisha tu kuwa naye?

Somo la leo litakupa mwanga wa kujua haki ya moyo na tamaa za mwili wako ni kipi sahihi kutendewa haki. Elewa kuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi.

Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haklupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi! Kama ndivyo, kwanini uwe mtumwa?

Unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!

Mapenzi ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako! Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!

Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!

Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu!

Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. Hii inaama kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha!

KUJIFUNZA KUPENDA!
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. Hufanya hivyo ajidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo.

"Pesa anazo, magari anayo, hata kama simpendi nitajitahidi kumpenda taratibu," baadhi ya wasichana huwaza hivi. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa.

MADHARA
Yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi wako uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndio msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote.

Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea? Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza kukua.

UNATENDA HAKI?
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaewza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.

Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo. Kumbukeni kuwa nawapenda sana!

JOSEPH SHULUWA
 
haika mbe..sio kwa wanawake tuu but hata kwetu sie nalo hutokea sometimes!!
 
Mapenzi ya kumuona mtu siku moja na kuamua kuwa nae ni kujidanganya. Manake longtime interests, tabia, mwelekeo vitu ambavyo ni muhimu kujulikana ili ujue kama mtakuwa compatible in the long run hujavijua, ndio sababu ndoa nyingi zinavunjika siku hizi hapa tanzania. Tumeiga ile love inayojulikana kwa kudunda kwa moyo mara unapomuona mtu, hiyo ni 'lust'
kupendana at first sight ni nzuri kwa short time relationships based on sex.
lakini kwa maisha marefu, ya kiutu uzima, yenye nia ya kuvumiliana, ni lazima ujue mengi ya mwenzio pamoja na mtazamo wake huhusu mambo ya kiuchumi, mambo ya kijamii, kiimani nk.
ukienda kujifunzia ndani inakuwa ngumu sana hasa pale mwenzio anapokuwa na mtazamo tofauti na wako na wewe unapokuwa hauko tayari kubadili ulekeo wako.
 
Kweli Mungu ni muugwana .. laiti ya moyo yangekuwa hadharani .... wengi tusingependa maana tungeuana ... kuna mfanyakazi mwenzangu alizaa na mwanadada mmoja lakini anamwambia wazi kabisa kwama hampendi mbele yetu ... akamwambia nilikukataza kuzaa ukalazimisha ... ila huyu jamaa yani kamzimia mwanamke mwengine ambaye hana hata habari ... na kishamtamkia kabisa kwamba hata uende wapi hunipati .. lakini yumo tu mpaka kumgharimia kila anachokihitaji ... anaenda puta ... hasikii kabisa
 
Lazima nijifikirie.... hahahaaaaaaa msemo unakera sana huo ila ni muhimu hii itakusaidia kumfahamu mtu japo kwa uchache ila sio natongozwa leo kesho nakubali kudadeki najifikiria miezi mi4 hahahaaaaa
 
leo nimekuja na mada nyingine, kama kawaida ni mada nzuri itakayokupa ufahamu mpya juu ya maamuzi yako yahusuyo mapenzi. Hivi ni kweli kwamba unautendea haki moyo wako? Mpenzi uliyenaye unampenda au unajilazimisha tu kuwa naye?

Somo la leo litakupa mwanga wa kujua haki ya moyo na tamaa za mwili wako ni kipi sahihi kutendewa haki. Elewa kuwa mapenzi ni sehemu ya maisha yetu na kwa hakika maisha yetu hayawezi kukamilika bila kuwepo mapenzi.

Ninapozungumza juu ya mapenzi namaanisha yale yanayotoka moyoni mwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine.
Mapenzi hayo, hukamilika baada ya wawili hao kuwa na hisia sawa za mapenzi. Amini kama upo katika uhusiano na mpenzi ambaye haklupendi, yaani wewe peke yako ndiyo unayempenda, wewe ni mtumwa wa mapenzi! Kama ndivyo, kwanini uwe mtumwa?

Unadhani hakuna mwingine ambaye anaweza kukupenda kwa mapenzi ya dhati na penzi hilo likawa kwa pande zote mbili tofauti na ilivyo sasa? Inawezekana, huna sababu ya kulazimisha penzi kwa mtu ambaye hakupendi!

Mapenzi ni nguzo ya maisha yetu, kama ukifanikiwa kumpata mpenzi ambaye atakupenda na wewe ukampenda ni wazi kuwa maisha yako yatakuwa yenye furaha na hakika utafurahia sana maisha yako na huyo mwandani wako! Mapenzi yapo hivyo na kama ukijaribu kuyabadilisha utaumia mwenyewe!

Wakati mwingine unaweza ukapendwa na mpenzi ambaye hujampenda, unadhani kuna ulazima wa wewe kulazimisha kumpenda? Moyo wako umeshazungumza na wewe, umekuweka wazi kuwa hauna mapenzi ya dhati kwa mtu huyo, kwanini ujilazimishe? Tatizo hili mara nyingi huwa kwa wanawake zaidi!

Anatokea mwanaume anampenda sana, anapomtongoza anajikuta kuwa hampendi, anachokifanya ni kumwambia kuwa atamjibu baadaye! Lengo la kumwambia hivyo ni kwa ajili ya kujipanga na kufikiria! Mapenzi hayafikiriwi ndugu zangu!

Kama mtu unampenda, unapomuona tu siku ya kwanza, moyo wako hutetemeka juu yake na hutamani uambiwe kitu fulani na huyo aliyeuteka moyo wako ghafla. Hii inaama kuwa atakapokuambia kuwa anakupenda, huwezi kusubiri zaidi, hutakuwa na kitu cha kusubiri, ni nafasi uliyokuwa ukiisubiria kwa hamu sana, na hazima utamkaribisha!

Kujifunza kupenda!
Baadhi ya wasichana, akitongozwa na mwanaume ambaye anaona wazi kuwa hampendi, lakini akawa na mali au uwezo mkubwa kifedha, huamua kumkubali kwa lengo la kupata vitu vya mwanaume huyo. Hufanya hivyo ajidanganya kuwa atajifunza kupenda akiwa ndani ya uhusiano na mwanaume huyo.

"pesa anazo, magari anayo, hata kama simpendi nitajitahidi kumpenda taratibu," baadhi ya wasichana huwaza hivi. Baada ya wazo hili kuingia akilini, huwa hana muda wa kusubiri zaidi, anakubali na wakati mwingine huweza kuingia katika ndoa.

Madhara
yapo mengi, lakini kubwa ni lile la kutokutosheka na mpenzi wako uliyenaye. Anaweza akakupa kila kitu lakini ukakosa penzi la dhati, ambalo ndio msingi wa maisha. Unajua kama kuna mtu anakupenda na wewe unampenda, unajihisi furaha na amani siku zote.

Madhara makubwa zaidi ni pale utakapojikuta ukiingia katia uhusiano na mwanaume mwingine kwa ajili ya kusaka penzi la dhati! Unajua kitakachotokea? Kama hutaleta magonjwa ndani basi siku moja utafumaniwa, siku lazima utafukuzwa nyumbani kwa mwanaume huyo, na kama ana hasira, anaweza kukua.

Unatenda haki?
Kamwe usijaribu kuingia katika mkumbo huu, mkumbo wa kujifunza kupenda, ni jambo gumu ambalo huweza likaharibu maisha yako kabisa. Jambo ambalo linaewza kukusababisha ukajuta kuzaliwa.

Kuwa makini, maamuzi yahusuyo mapenzi ni lazima yafanywe kwa umakini wa hali ya juu sana. Unapofanya uamuzi juu ya mapenzi, unakuwa unapanga mustakabali wa maisha yako yajayo. Kumbukeni kuwa nawapenda sana!

Joseph shuluwa
binadamu apaswa kuendeshwa na fikra yakinifu, weka vizuri hili la kuutendea haki moyo, moyo wako waweza angukia kwa dadako vp hapo.
 
Back
Top Bottom