Utendaji Wa Rais Magufuli Umemfanya Zitto Kabwe Atape Tape Kama Mfa Maji.

Ekethocho

Member
Jul 19, 2018
99
189

Tarehe 20/11/2015 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli analihutumia Bunge kwa mara ya kwanza jijini Dodoma, Wabunge wa Upinzani walitoka nje kupinga walichodai ni uchaguzi wa Zanzibar kutokwenda sawa. Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe alibaki Bungeni akionesha kumkubali Rais Magufuli na kwa maneno yake mwenye alisifia hotuba ya Rais.
kutokana na ukweli kwamba ZITTO ni mtu wa kupenda kunyemelea fursa(Opportunist) , kubaki kwake Bungeni wakati wapinzani wenzake wakitoka hakukuwa kwa bahati mbaya bali alifikiri Magufuli angempa fursa fulani za upigaji kama alivyozoea huko nyuma ikewemo kwenye mifuko ya Hifadhi za Jamii, Migodi ya Madini n.k.

Tarehe 22/07/2017, Rais Magufuli alipofanya ziara katika Mkoa wa Kigoma, Zitto Kabwe alikiri Magufuli anawaletea Wananchi Maendeleo na ndiyo maana wanampenda

Hata hivyo Baada ya Zitto kuona katika Serikali ya awamu ya tano, hakuna uwezekano wa fursa kwake alianza kuishambulia Serikali kwa hoja zisizo na mashiko. Hata hivyo kutokana na Watanzania kumjua vizuri Zitto kuwa ni ndumila kuwili wamekuwa wakiyapuuza mashambulizi hayo jambo ambalo limefanya ZITTO awe anadaka daka na kudandia hoja za wanaharakati na kusahau kuwa yeye ni Mwanasiasa na siyo Mwanaharakati.
Takwimu za uongo za uchumi wa Tanzania, Masuala ya Mashoga na Korosho ni baadhi ya mambo ambayo Zitto alitaka kujipatia Umaarufu lakini Watanzania wakampuuzia.
Kuonesha kuwa ni mnafiki , akawa na tabia ya kuandika kwenye Mitandao ya Kijamii kwa lugha ya Kiingereza eti kwamba na Wazungu nao wajue na waamini kuwa yeye ni kinara wa kuishambulia Serikali. Mbaya zaidi akadiriki hata kwenda Ulaya na Marekani eti kuishitaki Serikali. Sijui Mashitaka yake yaliishia wapi. Aibu kwake ni kwamba hao hao anaokwenda kushitaki kwao ndiyo hao hao wanaokuja Tanzania kuonana na Rais Magufuli, kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuiletea Tanzania Maendeleo na kuahidi ushirikiano mzuri kati ya nchi zao na Tanzania.

Jana tarehe 08/08/2019 Rais Magufuli aliwatembelea WanajeshI wa Jeshi letu la Wananchi Ufukweni mwa Bahari wakifanya usafi. ZITTO kaibukia Twitter eti Rais anaacha anakwenda kuwasalimia Wanajeshi na kuwaacha Wakulima ambao ndiyo wapiga kura wengi. Mawazo ya ajabu sana haya, hakuna mtu alitegemea kusikia mawzo yasiyo na mashiko kama haya. Kila siku Rais anafanya ziara Mikoani na kila akiwa Ziarani anakutana na Wakulima wakiwa na Kero zao na huzitatua zingine papo kwa papo. Ni katika awamu hii ya tano Migogoro Mingi ya Ardhi imetatulia. Serikali ya awamu ya tano imekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha Wakulima wanapata mbegu, Mbolea na masoko ya mazao yao, Zitto kaweka Pamba Masikioni na kufumba macho asiyaone haya na badala yake anataka Rais atumie dakika 20 alizotumia kwenda kuwasalimia Wanajeshio aende kwa Wakuliwa wote wa Tanzania. Aibu kubwa sana na unafiki uliopitiliza.

HITIMISHO: Tabia ya Undumila Kuwili, Ukinyonga na Unafiki kwa mtu anaweza kuwa na ushawishi kwa Wananchi ni harati sana kwa Taifa. ZITTO Anatambua kabisa Serikali ya awamu ya tano inafanya kazi nzuri lakini kwa sababu ya undumila kuwili , ukinyonga na unafiki wake anataka kuwaoneaha wanaharakati na wote wasioitakia mema nchi yetu kuwa yuko nao kumbe ni uongo, SIasa zimemshinda sasa anatapatapa, ni wa kupuuzwa.
 
Nikimtukana mtanifungia. Alikwenda sokoni akitegenea watu wangemlalamikia, akakuta watu wakimfia Magu, ndio akatafuta njia nyingine kumtafuta JPM. Ndipo akapata CinC na watu wake wakiwa fatiki. Naye akawa nao
 
Adui yako muombee njaa ili kumdhibiti vizuri.Magu kamuombea njaa Zito hivyo kamdhibiti sehemu amabazo alikua kazoea kujipatia atakavyo sasa hakuna ndomana anatapatapa kila kukicha ajipatie japo kidichu kama awamu zilizopita ilikua kutishatisha watu matajiri na wanasiasa wenye vijisenti ili awachune sasa zimezibwa hizo njia
 
Tarehe 20/11/2015 wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John pombe Magufuli analihutumia Bunge kwa mara ya kwanza jijini Dodoma, Wabunge wa Upinzani walitoka nje kupinga walichodai ni uchaguzi wa Zanzibar kutokwenda sawa. Zitto Zuberi Ruyagwa Kabwe alibaki Bungeni akionesha kumkubali Rais Magufuli na kwa maneno yake mwenye alisifia hotuba ya Rais.
kutokana na ukweli kwamba ZITTO ni mtu wa kupenda kunyemelea fursa(Opportunist) , kubaki kwake Bungeni wakati wapinzani wenzake wakitoka hakukuwa kwa bahati mbaya bali alifikiri Magufuli angempa fursa fulani za upigaji kama alivyozoea huko nyuma ikewemo kwenye mifuko ya Hifadhi za Jamii, Migodi ya Madini n.k.

Tarehe 22/07/2017, Rais Magufuli alipofanya ziara katika Mkoa wa Kigoma, Zitto Kabwe alikiri Magufuli anawaletea Wananchi Maendeleo na ndiyo maana wanampenda

Hata hivyo Baada ya Zitto kuona katika Serikali ya awamu ya tano, hakuna uwezekano wa fursa kwake alianza kuishambulia Serikali kwa hoja zisizo na mashiko. Hata hivyo kutokana na Watanzania kumjua vizuri Zitto kuwa ni ndumila kuwili wamekuwa wakiyapuuza mashambulizi hayo jambo ambalo limefanya ZITTO awe anadaka daka na kudandia hoja za wanaharakati na kusahau kuwa yeye ni Mwanasiasa na siyo Mwanaharakati.
Takwimu za uongo za uchumi wa Tanzania, Masuala ya Mashoga na Korosho ni baadhi ya mambo ambayo Zitto alitaka kujipatia Umaarufu lakini Watanzania wakampuuzia.
Kuonesha kuwa ni mnafiki , akawa na tabia ya kuandika kwenye Mitandao ya Kijamii kwa lugha ya Kiingereza eti kwamba na Wazungu nao wajue na waamini kuwa yeye ni kinara wa kuishambulia Serikali. Mbaya zaidi akadiriki hata kwenda Ulaya na Marekani eti kuishitaki Serikali. Sijui Mashitaka yake yaliishia wapi. Aibu kwake ni kwamba hao hao anaokwenda kushitaki kwao ndiyo hao hao wanaokuja Tanzania kuonana na Rais Magufuli, kumpongeza kwa kazi nzuri ya kuiletea Tanzania Maendeleo na kuahidi ushirikiano mzuri kati ya nchi zao na Tanzania.

Jana tarehe 08/08/2019 Rais Magufuli aliwatembelea WanajeshI wa Jeshi letu la Wananchi Ufukweni mwa Bahari wakifanya usafi. ZITTO kaibukia Twitter eti Rais anaacha anakwenda kuwasalimia Wanajeshi na kuwaacha Wakulima ambao ndiyo wapiga kura wengi. Mawazo ya ajabu sana haya, hakuna mtu alitegemea kusikia mawzo yasiyo na mashiko kama haya. Kila siku Rais anafanya ziara Mikoani na kila akiwa Ziarani anakutana na Wakulima wakiwa na Kero zao na huzitatua zingine papo kwa papo. Ni katika awamu hii ya tano Migogoro Mingi ya Ardhi imetatulia. Serikali ya awamu ya tano imekuwa mstari wa Mbele kuhakikisha Wakulima wanapata mbegu, Mbolea na masoko ya mazao yao, Zitto kaweka Pamba Masikioni na kufumba macho asiyaone haya na badala yake anataka Rais atumie dakika 20 alizotumia kwenda kuwasalimia Wanajeshio aende kwa Wakuliwa wote wa Tanzania. Aibu kubwa sana na unafiki uliopitiliza.

HITIMISHO: Tabia ya Undumila Kuwili, Ukinyonga na Unafiki kwa mtu anaweza kuwa na ushawishi kwa Wananchi ni harati sana kwa Taifa. ZITTO Anatambua kabisa Serikali ya awamu ya tano inafanya kazi nzuri lakini kwa sababu ya undumila kuwili , ukinyonga na unafiki wake anataka kuwaoneaha wanaharakati na wote wasioitakia mema nchi yetu kuwa yuko nao kumbe ni uongo, SIasa zimemshinda sasa anatapatapa, ni wa kupuuzwa.

Magu Anashindana na Zitto? how can that be, one is in Heaven the other on earth? Ana Dola ana wewe? zitto anamkoseshaje usingizi?
 
mnahangaika na huyu mtu wenu hadi mnatia huruma, hata nyie mnajua hilo. ndo maana mnatafua kila klips za wote wanaomsifia mtu wenu mnaziweka hapa, hasa za watu mnaoona wanao ushawishi kwenye jamii. mbona hamleti za wanaokosoa utekaji, dhuruma, kupotea, kudukuana na kubambikiana mikesi. ni kwenye huu tu utawala watu hamtaki kupingwa hata kama mnasaidia kiushauri.
 
When you talk about hypocrite politician in Tanzania, you talk about zitto zuberi kabwe.
 
Back
Top Bottom