joto la jiwe
JF-Expert Member
- Sep 4, 2017
- 26,117
- 46,613
Kitendo cha Magufuli kutubutu kuanzisha miradi mikubwa ya maendeleo bila kusubiri pesa za wafadhili, iwe ni funzo kwa viongozi wa Afrika wanaotegemea kukopa toka kwa wafadhili ili kutekeleza miradi midogo sana ukilinganisha na uchumi wa nchi husika.
Nilipata mshituko kusikia kwamba nchi kama Morocco yenye uchumi mkubwa, lakini ilijenga reli ya SGR yenye urefu wa 300km kwa gharama ya $2.6B kwa mkopo wenye riba kubwa na kuzidisha mzigo wa madeni kwa wananchi.
Hivi hii tabia ya kupenda kukopa hata pale ambapo sio lazima kukopa itaisha lini Africa?, tabia hii ndio inalolifanya bara la Africa kuwa tegemezi, omba omba na mzigo ktk uchumi wa dunia. Hongera Magufuli kwa kuonyesha njia. YES AFRICA WE CAN.