Utendaji wa kusukumwa mpaka lini?

Bashir Yakub

Member
May 27, 2013
64
900
UTENDAJI WA KUSUKUMWA MPAKA LINI ?.

Waraka wa BASHIR YAKUB.
+255784482959.

Kama kuna watu wanapaswa kutumbuliwa ni hawa wanaosubiri mpaka rais aseme halafu ndio waanze kufukuzana na majukumu yao.

Ni ajabu tokea rais aseme alivyochoshwa na ajali, karibia barabara zote za mikoani kunawaka moto.

Makamanda wamechachamaa. Wanakagua magari, wanakagua leseni na kila cha usalama.

Unaweza kufikiri labda kabla rais hajasema ukaguzi huu ulikuwa unakatazwa.

Ni aina ya kasumba mbaya kabisa kwa yeyote mwenye majukumu. Hutendi wala hufanyi mpaka mkubwa achachamae !!!. Ni kati ya mambo mabaya sana.

Zama hizi hazihitaji watu wa aina hii. Kinachoshangaza hawaoni hata aibu. Wanatokea tu mbele ya media na kusema" *_kuanzia leo tukikumata umevunja sheria za barabarani sheria itachukua mkondo wak_ e..._ ."* na maneno mengine yanayofanana na hayo.

Mtu anasema eti " *_kuanzia leo..",_*_ kwani kabla ya hapo ilitakiwa iweje. Ni mambo ya ajabu.

Nakumbuka swali muhimu ambalo karibia kila usaili(interview) huwa linaulizwa, " *uwezo wa kujituma kufanya kazi bila uangalizi/shinikizo.* Kitu hiki ni muhimu sana kwenye utumishi na kukosekana kwake huwezi kukwepa kushuhudia haya tunayoshuhudia leo.

Ukaguzi unaoendelea stendi za Iringa, kahama, Shinyanga, ubungo na nyinginezo haukutakiwa kusubiri mpaka rais aoneshe huzuni ya ajali. Haukutakiwa mpaka waziri awajibishwe. Bali ulitakiwa kuwa desturi na mila.

Na hii sio kwenye hili tu bali hata mengine.Mara nyingi rais akicharukia jambo fulani kesho yake utaona media zote zikionesha wahusika sehemu mbalimbali wakizunguka huku na huku, wakitoa maonyo,wakikemea, wakipiga mikwara nk.

Kwani mnakuwa wapi mda wote!!?,. Au wakati huo mnakuwa hamjajua la kufanya!!?. Ilikuwa hivyo kipindi kile cha makinikia, ikawa hivyo kipindi cha usafi, na sasa ni barabarani.

Watu watekeleze majukumu yao wasisubiri rais aseme. Ningekuwa rais siku nikikemea jambo, halafu kesho yake anaibuka mtendaji kwenye media eti kutoka onyo kwa jambo hilohilo, ambalo liko kwenye majukumu yake ya kila siku , na alikuwa kimya mda wote,basi huo ndio ungekuwa mwisho wake.

Ndio, hawa ndio wanaoturudisha nyuma na ndio waliotufikisha hapa. Wanajisahau mno. Kaeni macho mtaona hata leo raisi akizungumza kuchukizwa na jambo halafu muone kesho hali inakuwaje mitaani na kwenye media kwa wahusika. Kila mtendaji utasikia "kuanzia leo..." Ni aibu.

Unasemaje "kuanzia Leo.." kwa jambo ambalo limo kwenye sheria karibia miaka 50, na wewe umekabidhiwa sheria hiyo ikuongeze kwenye majukumu yako huu karibia mwaka wa 2,3 au miezi kadhaa.

Tekeleza majukumu yako usisubiri rais au mkubwa mwingine aseme bana.
 

UPOPO

JF-Expert Member
Dec 17, 2010
3,061
2,000
Ndio ujue mifumo yaani system inatakiwa kujengwa kwanza na sio watu.Ukiweka mfumo imara sidhani kama haya yangetokea leo.Tumejitawala miaka zaidi ya 50 bado hatuna mifumo endelevu kila siku ni matamko mapya.Hawa polisi na viongozi wengine wangekuwa wanapewa malengo with clear deliverables na wanakuwa wanafanyiwa perfomance appraisal au tathimini kila baada ya muda fulani (usizidi mwaka) na consequences zake ni nini sidhani hata Raisi angepata tabu ya kutoa matamko asubuhi na mchana.Kila kitu kinaendeshwa kisiasa yaani kama tumelogwa ,Ajali zikiisha humsikii mtu anaongea na ndio uzembe uanza.Tunarukia kingine.Tuendeshe nchi kitaalamu na si kisiasa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom