nderingosha
JF-Expert Member
- Mar 20, 2011
- 4,281
- 3,243
Jeshi la polisi TZ ni moja ya taasisi ya muungano...yaani linafanya kazi zake Tanganyika na Zanzibar..na linatakiwa lisioneshe bias kiutendaji katika sehemu hizi mbili za muungano....Kuna mambo yanayofanywa na jeshi letu la polisi TZ yamenifanya niwe na maswali mengi kuhusu agenda za utendaji wa jeshi la polisi TZ....ebu tafakari haya matendo ya jeshi hili alafu kila mtu atakuwa na conclusion yake......
- Ni jambo la kawaida nchini TZ kuona wanafunzi wa vyuo vikuu wenye matatizo ya msingi wanapoamua kuandamana/kutembea kwa amani ili kudai haki zao wakitokewa na kupigwa na kutawanywa na polisi wenye magari yenye maji ya pilipili na mabomu ya machozi....wengine hupigwa na polisi na kuumizwa vibaya...tena wale polisi wanaoitwa FFU....tena mabomu hupigwa kama vile wanaoandamana ni magaidi......
- Ni jambo la kawaida TZ kuona wanaharakati wenye kubeba jumbe za msingi sana kijamaii wanapoamua kuandamana/kutembea kwa amani..hutokewa na kupigwa/kutawanywa na jeshi la polisi....tena kwa kutumia silaha za moto yakiwemo mabomu ya machozi na maji yenye pilipili....mfano...jikumbushe yaliyotokea wakati wanaharakati walipoandamana kushinikiza serikali itatue madai ya madaktari.....walipotokewa na kutawanywa na jeshi la polisi na wengine hata kushikwa na kuwekwa rumande......
- Ni jambo la kawaida TZ kuona jeshi la polisi likizuia maandamano/matembezi ya amani ya vyama vya siasa kuelekea kwenye mikutano yao.....tena waandamanaji hutawanywa kwa mabomu ya machozi na hata kupigwa vibaya na pia kukamatwa na polisi....kumbuka yaliyotokea CDM kule arusha....na pia kumbuka jeshi la polisi walivyowazuia wafuasi wa CDM wasitembee kwa miguu hivi majuzi kuelekea kwenye mkutano wao jangwani.....
- Tumeona jeshi la polisi wakiwapiga hadi kuwaua raia wasio na hatia kule songea walipoandaman/tembea kwa amani kudai haki yao ya msingi ya kulindwa na polisi.......
- LAKINI HIVI MAJUZI KULE ZANZIBAR TUMEONA WAHUNI/WAHALIFU/MAJAMBAZI WAKIANDAMANA NA KUCHOMA HADI MAKANISA.....BILA KUONA HATUA YOYOTE YA POLISI KUINGILIA KWA MABOMU YA MACHOZI AU MAJI PILIPILI AU SILAHA ZA MOTO....KAMA WANAVYOFANYA KWENYE MAANDAMANO/MATEMBEZI YA AMANI TANGANYIKA......HAINGII AKILINI NI KWA VIPI RAIA WALIUWAWA KULE SONGEA KWA KUANDAMANA KWA AMANI...WAKATI WAHALIFU/MAJAMBAZI WAMECHOMA MAKANISA ZENJ HUKU WAKISHUHUDIWA NA HAO HAO POLISI!!!!!!!!HIVI HILI JAMBO LINACHUKULIWAJE???????TAFAKARI........