Utendaji uliotukuka wa Dkt. Anna Makakala ukimpendeza Rais awateue wakuu wengine wa Majeshi yetu Wanawake

Tungehangaika zaidi na uteuzi wa wanawake wenye CV na utendaji bora. Mama wa Uhamiaji amejitahidi japo we expected more from her ilibidi ashughulikie tuhuna zilizoibuliwa Arusha juu ya mtandao wa wanauza visa fake kwa wageni wanaotuhumiwa wakiwemo maafisa wake( hili hata wakili Peter madelekea amelizungumza wazi bila kupepesa macho) haswa wale wanaokaa mipakana na airport.

Zile za kukamata kina kabendera, askofu niwemugizi na wengineo kuhusu uraia limemtia doa kama mtaalamu badala ya kushauri mamlaka uweledi utumike yeye akakumbwa na siasa za mwendazake.

Tukiwa tunafuata Foreign policy iliyoelekea kwenye Economic Diplomacy dunia ya leo si ya kuongeza ukiritimba kwenye utoaji wa passport. Tatizo la ajira ni kubwa sana na hakuna straight policy ya ku export nguvukazi nje ya nchi, maana upatikanaji wa passport wenyewe ni mgumu na mrefu sana hili linafanya vijana kujazana mijini kuuza mitumba ili hali wangeenda hata iran huko kufanya kazi na middle east kwa ujumla. Hili lilitegemea mama kama mtaalamu angeongoza na kupunguza ukiritimba katika utoaji wa passport. Kenya na rwanda diaspora remittance ni kubwa sababu ya watu kutoka kwenda kutafuta nje ya mipaka ya nchi zao.

Ningeshauri mama angerudi kufundisha kule chuo cha uhamiaji maana ni mzuri kwenye kuelimisha zaidi.
Hakika umenena vesa sn
 
Tusianze kufanya majaribio kwenye kazi nyeti kama ya jeshi ,huko magereza ni idara tu sawa na idara ya wanyama pori, Mungu hakuwa mjinga alivyoumba tofauti kati ya mwananmke na mwanaume.Huko jeshini hakuna komandoo mwananmke,unajua ni kwanini. Ni nchi gani duniani ambayo mkuu wa jeshi ni mwanamke?
good questions. nakumbuka america waliwahi kipiga kelele kwann hakuna mwanamke special forces operator. feminist wakataka vigezo vya selection vishushwe.. ikashindakana.

wakaambiwa wakitaka kuingia.. lazima wa pass the same selection wanayo pass wanaume.
same standards.

mpaka leo walikaa kimya.
huwez susha standard za jeshi ktk eneo fulani ili jinsia fulani iingie.
wakitaka hizo nafasi wa perform at higher standards as men.
hakuna cha upendeleo
 
Awamu iliyopita ilikuwa ngumu kiutawala na ilihitaji ujasiri kusimama na kubaki kwenye nafasi ya juu ya uteuzi. Dr. Anna Makakala Ni mmoja wa wanawake waliovumilia nakupambana kwa miaka mitano ya awamu hiyo bila kutumbuliwa.

Kila ukiangalia picha za awamo ya tano utabaini alipokuwa Rais na huyu mama na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi walikuwa naye. Maana yake aliweza kusafiri mchana na usiku kutetea kibarua chake. Hongera sana.

Sasa hivi ni muda wa Rais wa awamu ya sita kutebgeneza safu yake. Naamini yupo mbioni kuteua wakuu wa vyombo kwani waliopo sura zinasadifu kwamba wapo ukingoni. Lakini pia Ni haki yake kina na damu mpya kiutawala nakuruhusu mawazo mapya.

Dkt. Makakala anaweza akabaki au asibaki kwenye nafasi yake ila tuna budi kumpongeza kwa kazi aliyofanya. Nikipitia mitandaoni naona ni kipindi chake ndicho huduma za Uhamiaji ziliimarika namalalamiko yakapungua sana. Yeye Kama mwanamke mwenzetu kwa kweli amewafumbua macho wanaume kwamba wanawake wanaweza bila hata kuwezeahwa.

Tuliaminiwa kwenye sekta nyingine ila kwenye vyombo vya ulinzi ilikuwa bado, Sasa naamini Makakala ametupa mwanga na kutujengea imani kwamba tunaweza bila kuwezeahwa.

Nimwombe Mhe. Rais atusaidie kupata wanawake katika nafasi za juu za vyombo vyetu nikimwakikishia Kama Makakala aliweza katika mazingira ya hakuna kulala Basi watakaoteuliwa Sasa watafanya zaidi.

Tunapenda kuona luten General au meja general au hata CDF akiwa mwanamama.

IGP au Makamishna wa polisi Magereza na zimamoto tuwaone wanawake kwani naamini Wana sifa na maarifa yakuongoza vyombo hivi.

Dkt. Makakala umetuheshimisha, wanawake wengine mtakaopewa nafasi nilizoomba hapa msituangushe, kasimamieni kazi bila kutanguliza tamaa Wala kuonea watu.

Wanawake wanaweza bila hata kuwezeahwa.
Hizo sio post za kisiasa, unatunukiwa kulingana na medani na utendaji wa kazi dio ujingaujinga.
 
Naunga mkono hoja
P
Wewe ulipita JKT unaelewa kabisa jeshi sio CCM. Mtu aende vitani ndio aje kuclaim medal jeshini sio miss Tanzania tafadhali sana. Tutakuja kuwa na CDF ambaye akisikia bomu anamuita mumewe akachungulie. Tunataka kama ni mwanamama awe kweli chuma sio Hawa walimbwende wanaoingia jeshini kutafuta ajira tu.
 
Back
Top Bottom