afrikando
JF-Expert Member
- Jul 24, 2013
- 242
- 109
Jeshi la Polisi jijini Dar Es salaam linatenda kazi zake kwa kuchagua? Au kwa kufuata upepo utakavyovuma tu?
Kamanda S Sirro kama ameingia mitini vile, tujikumbushe Mapambano yaliyopigiwa kelele nyingi mno na mwisho wa siku kufanikiwa kwake ni siri yao. Baadhi ni kama vita ya kuwaondoa machangudoa mitaani., ombaomba, machinga, wauzaji na watumiaji wa Shisha, uhakiki wa umiliki wa silaha, Mapambano na waendesha bodaboda, madawa ya kulevya, kuzuia UKUTA, kutawanya maandamano ya wapinzani, kupambana na uhalifu wa kutumia silaha, kudhibiti matukio ya ajali au usalama barabarani, makusanyo ya pesa kama TRA, kumsindikiza RC katika mishemishe zake, kung'oa gurudumu za magari yanayoingia kwenye Barbara za mwendo kasi, na mengine mengi kama mtavyoongezea na kurekebisha. Tulizoea kumsikia kamanda wa kanda maalum S Sirro akiyatolea matamko, lakini hivi sasa ni Kimya sana. Sijui yupo likizoni au naye amepigiwa ban ya kuandikwa na wanahabari kama DAB au ndiyo pumzi imekata?
Kiujumla Police Force inatakiwa irekebishwe iendane na madhumuni ya uwepo wake. Hii itarudisha imani kwa sisi raia kuwa jeshi hili halitumikii wanasiasa walio mamlakani na walionacho, kukandamiza wasio mamlakani na raia wengine wasionacho.