Utendaji kazi polisi unasababisha ajali ambazo zingeepukwa

UJANJAUJANJA

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2012
Messages
227
Points
195

UJANJAUJANJA

JF-Expert Member
Joined Oct 14, 2012
227 195
Wana JF,

Leo nilipata bahati ya kupita karibu na kituo cha polisi cha Chang'ombe, nikaona ni heri nipeleke gari langu pale kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi na ikithibitika liko vizuri basi nipewe stika ya nenda kwa usalama barabarani. Baada ya kufika nilijitambulisha na kuomba gari langu lifanyiwe ukaguzi, cha kushangaza ni kwamba badala ya kwenda kufanya ukaguzi kutambua "road worthiness" ya gari, askari aliyekuwepo pale akaomba kupatiwa nakala ya kadi ya gari akaanza kuandika na baada kunikabidhi stika. Nikamuuliza, ndugu yangu siku hizi utaratibu umebadilika? Akabaki anashangaa. Nikaendelea kumuomba anifahamisha kwa sababu nilikuwa nje ya TZ miaka miwili sasa na kama utaratibu ni kuandika tu au kukagua gari kwanza. Nilichokigundua ni kwamba pamoja na kukabidhiwa majukumu yake, askari yule hajui sheria inamtaka atekeleze na afanye nini. Tuna safari ndefu kuzuia ajali ambazo zingeweza kuepukwa bila ulazima
 

Gogo la choo

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2012
Messages
713
Points
195

Gogo la choo

JF-Expert Member
Joined Oct 8, 2012
713 195
Askari weng ni form four zero sasa unategemea atakagua nini hapo zaidi ya kujichanganya tu mwenyewe..ndo maana ulipomuuliza kuhusu huo utaratibu ametoa macho kama kabanwa mbavu..!!
 

Forum statistics

Threads 1,392,383
Members 528,604
Posts 34,107,575
Top