Utekwaji wa hoja ya Vita Kawawa ni kwa maslahi ya nani?

Byendangwero

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
871
56
Wakati wa kuchangia bajeti ya wizara ya madini na nishati Vita Kawawa alitoa hoja akimtaka spika apange muda wa kujandili humo bungeni tuhuma zilizoelekezwakwa baadha ya wabunge kwamba walikuwa wamepewa hongo kwaajili ya kuwakingia kifua baadhi ya watendaji waandamizi wa Tanesco waliosimamishwa kupisha uchunguzi. Spika kwanza aliizima hoja hiyo kwa madai kwamba imeletwa kinyume na kanuni husika. Baadaye wakati wa kuhitimisha shughuli za siku hiyo Mh. Kawawa alikaribishwa kuwasilisha hoja yake; kwa mshangao wa baadhi yetu, mahudhui ya hoja iliyowasilishwa na Kawawa ilikuwa ni tofauti na yale ya mwanzoni; wakati hapo mwanzoni hoja yake ilikuwa inataka suala hilo lishughulkiwa kwa mjadala wa wazi unao wahusisha wabunge wote, hoja iliyotolewa hapo baadaye imempa madaraka spika kushughulikia suala hilo kwa jinsi apendavyo. Inavyoelekea Mh. Kawawa alibanwa kulegeza msimamo wake wa awali, kwani hata wakati wa kuwasilisha hoja yake ilionekana wazi kwamba alikuwa akisoma mambo ambayo alikuwa hakuyahandaa yeye mwenyewe. Swali ni jee hayo mabadiliko yalifanywa kwa maslahi ya nani? Siyo siri kwamba katika mpangilio wasiasa hapa nchini inajulikana wazi ya kwamba spika Anne Makinda yuko kwenye kambi la Lowasa na Rostam Aziz; na waathirika katikasakata hili pia wako katika kambi hilo hilo; hivyo madaraka aliyopewa spika Makinda, bila shaka atayatumia kujaribu kadri inavyowezekana kuzima sakata hilo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom