ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,543
Kupitia taarifa ya habari jana Jumatatu saa mbili usiku Azam TV imeripoti habari ya kiwanda kimoja cha kuzalisha vifaranga cha mjini Moshi kuteketeza mamia ya vifaranga kwa kuwatosa kwenye moto mkaili eti kisa tu vifaranga hao wamekosa soko!
Kweli japo kuku wanaliwa kila siku lakini kitendo kilichofanywa na uongozi wa kiwanda hicho ni cha kinyama tena kinyama mno.
Kwa kweli nimepigwa na butwaa baada ya kusikiliza habari ile na kumshuhudia mmoja wa wafanyakazi akitupia box moja baada ya jingine juu ya moto mkali huku vifaranga vikilia kwa uchungu! Aisee imeniuma mno.
Sababu za mkurugenzi:
~ Walivisafirisha vifaranga hivyo hadi Dar ili viuzwe kwa tsh 1000, biashara ikawa ngumu kwa sababu ati kuna watu wengi sasa hivi wana ingiza vifaranga toka nje hivyo soko limetibuka.
Wakaamua washushe bei hadi Tsh 900, bado hawakupata soko. Wakaamua mzigo urudi kiwandani Moshi huko nako wakatangaza bei ya Tsh 900 ikashindikana, uamuzi wao wa mwisho ukawa ni kuwateketeza kwa moto mkali!
Tuiombe serikali kitengo cha watu wa mifugo au kama bado ipo taasisi ya kutetea wanyama iwafuatilie wamiliki wa kiwanda hiki na ikibidi wachukuliwe hatua kali ili iwe onyo kwa wengine watakaofikiria kufanya upuuzi huu.
Maana Mkurugenzi wao ameshasema kuwa vifaranga wengine laki nane na nusu wanatarajiwa hivi karibuni na hajui pa kuwapeleka.
Nimejiuliza kwanini basi hata huku Dar na Moshi wasivigawe kwa mtu yeyote atakayeweza kutunza? Hata kama mtu angechukua 20 mwingine box 4, mwenye vifaranga 60 n.k, wangetangaza tu hadharani, au kuwatangazia hata majeshini, vyuoni pengine wangejaribu kuwakuza vifaranga hao wa nyama na mayai.
Nimalizie kwa kusema kitendo kile ni cha kishetani na hakina budi kulaaniwa na serikali ichukue hatua stahiki na hili lisijirudie.