Utekelezaji wa sheria za Tanzania 'double standard'

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,419
2,337
Kwa mtazamo wangu, sheria za Tanzania zinatekelezwa kwa kufuata 'social status' ya mtu na siyo kosa lililotendeka. Mfano, mwananchi wa kawaida akituhumiwa kuwa ametenda kosa fulani la jinai atawekwa chini ya ulinzi na polisi huku uchukunguzi ukiwa unaendelea.

Lakini kama ni kigogo fulani serikani mara nyingi siyo hivyo. Vilevile, kama mwananchi wa kawaida akitiwa hatiani, mfano, kuua bila kukusudia anawekwa rumande miaka nenda rudi. Lakini kama ni kigogo fulani inawezekana isiwe hivyo. Je, haya ninayosema siyo kweli? Inawezekana watu wengine wana maoni tofauti. Naomba tuelimishane kwa hili.
 
Magobe,

Naomba u-develop argument yako zaidi NA kwa kutumia mifano.Kwa mfano mtu anaweza kuku support kwa kuchukulia kesi ya marehemu Ditopile jinsi alivyoua kufungwa na kutolewa kwa dhamana haraka haraka wakati kuna watu wana miaka kumi Keko -rumande, siyo jela-bado wanasomewa mashtaka ya kuua.

Mtu mwingine anaweza kusema ingawa Ditopile alipewa dhamana haraka, hivyo ndivyo inavyotakiwa iwe kwa wote, kwa hiyo double standard ipo lakini focus iwe katika kuondoa ucheleweshwaji wa haki kwa watu wa kawaida kwa sababu kama wanavyosema wasomi wa sheria "haki iliyocheleweshwa ni haki iliyokataliwa"
 
Asante ndugu Pundit kwa ushauri. In fact, nilichosema kimetokana na malalamiko ya watu ambao nimesikia vilio vyao ama kutoka wao wenyewe au kupitia vyombo vya habari na man'gamuzi yangu binafsi.

Ingawa ni wazi mfano ulioutoa ni moja wapo ya mifano inayoonyesha jinsi kundi la watu fulani wanavyoweza kutendewa na hali wengine wakibaki kwenye dhiki kuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom