Kwa mtazamo wangu sheria za Tanzania zinatekelezwa kwa kufuata 'social status' ya mtu. Mfano, mwananchi wa kawaida akituhumiwa kuwa ametenda kosa fulani la jinai atawekwa chini ya ulinzi na polisi lakini kama ni kigogo fulani serikarini mara nyingi siyo hivyo.
Vilevile, kama mwananchi wa kawaida akitiwa hatiani, mfano, kuua bila kukusudia anawekwa rumande miaka nenda rudi lakini kama ni kigogo fulani inawezekana isiwe hivyo. Je, nimekosea kuwa na mtazamo huu? Naomba mchango wenu.