Utekelezaji wa sera za haki sawa na furaha kwa wote utaifanya nchi kwa mara ya kwanza tangu uhuru ipumue

CUF Habari

JF-Expert Member
Dec 12, 2019
239
234
Hebu fikiria nchi ambayo elimu ni haki ya kila mwenye kuihitaji, bila kujali ukomo anaoutaka na bila kujali kiuchumi amekaaje!

Hebu fikiria nchi ambayo suala la afya bora ni haki ya msingi ya kila Mwananchi bila kujali uwezo wake wa kiuchumi!

Hebu fikiria nchi ambayo kwa mara ya kwanza kutakuwa na katiba inayolinda tunu zote za utawala bora na ambayo inajilinda isivunjwe na watawala wenye nia mbaya na maslahi ya umma!

Hebu fikiria nchi ambayo HAKI IMETAMALAKI na Wananchi hawana hofu kabisa kuwa haki zao zitagandamizwa kwa sababu ya NASABA ZAO, JINSIA ZAO, MAKABILA YAO, DINI ZAO, AU UWEZO WAO WA KIUCHUMI!

Hebu fikiria nchi ambayo ili kuondokana na UDUMAVU (Hivi sasa karibia 50% ya Watanzania wanakabiliwa na aina moja ama nyingine ya udumavu) kina mama wote wajawazito na wale wanaonyoshesha watapewa unga wa uji uliomarishwa kwa viini lishe muhimu!

Hebu fikiria......

Kwa kweli orodha ni ndefu. Kwa nini uhangaike kukimbilia ULAYA au MAREKANI, wakati ULAYA, MAREKANI, JAPANI, KANADA, nakadhalika zinawezekana hapa hapa?!

Haya BEGA KWA BEGA, MKONO KWA MKONO na Chama cha Wananchi - CUF.

Mbona tutafika tu!!
 
Lipumba alipewa fedha na ccm akaenda kununua dagaa Rwanda sasa sijui mtawaambia nini watanzania
Na wasiendelee kulialia,Malim Seifu ameshawaachia lichama lao,waendelee kuungana na lichama lao pendwa.
 
Hamtafanikiwa peke yenu, muwe BEGA KWA BEGA, MKONO KWA MKONO na vyama vingine vya upinzani.
 
poleni sana cuf, mahesabu yenu mnayopiga hayana alama ya = sijui jibu mtaandika wapi.
Hebu fikiria nchi ambayo elimu ni haki ya kila mwenye kuihitaji, bila kujali ukomo anaoutaka na bila kujali kiuchumi amekaaje!

Hebu fikiria nchi ambayo suala la afya bora ni haki ya msingi ya kila Mwananchi bila kujali uwezo wake wa kiuchumi!

Hebu fikiria nchi ambayo kwa mara ya kwanza kutakuwa na katiba inayolinda tunu zote za utawala bora na ambayo inajilinda isivunjwe na watawala wenye nia mbaya na maslahi ya umma!

Hebu fikiria nchi ambayo HAKI IMETAMALAKI na Wananchi hawana hofu kabisa kuwa haki zao zitagandamizwa kwa sababu ya NASABA ZAO, JINSIA ZAO, MAKABILA YAO, DINI ZAO, AU UWEZO WAO WA KIUCHUMI!

Hebu fikiria nchi ambayo ili kuondokana na UDUMAVU (Hivi sasa karibia 50% ya Watanzania wanakabiliwa na aina moja ama nyingine ya udumavu) kina mama wote wajawazito na wale wanaonyoshesha watapewa unga wa uji uliomarishwa kwa viini lishe muhimu!

Hebu fikiria......

Kwa kweli orodha ni ndefu. Kwa nini uhangaike kukimbilia ULAYA au MAREKANI, wakati ULAYA, MAREKANI, JAPANI, KANADA, nakadhalika zinawezekana hapa hapa?!

Haya BEGA KWA BEGA, MKONO KWA MKONO na Chama cha Wananchi - CUF.

Mbona tutafika tu!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom