Utekelezaji wa sera za CCM: Mradi wa mabasi, wananchi wakubaliana fidia

Tume ya Katiba

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
4,896
1,862
Wadau,
Katika kutekeleza sera na ahadi mbali mbali nimeona niwaletee taarifa njema, tuwe wavumilivu soon foleni zitakuwa historia.


WAKAZI wa Gerezani Kota wilayani Ilala, Dar es Salaam na Wakala wa Mradi wa Mabasi yaendayo Kasi Dar es Salaam (DART), jana wameafikiana kuhusu suala la fidia ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya mradi huo.

Muafaka huo ulifikiwa katika mkutano wa wakazi hao, uongozi wa Dart na Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa uliofanyika katika Ukumbi wa Arnatouglou.

Akizungumza katika mkutano huo, Silaa amewataka wakazi hao kufika katika ofisi za Dart kwa ajili ya mchakato wa fidia hizo na kuacha kurubuniwa na baadhi ya watu.

Alisema kitendo cha baadhi ya wanasiasa na wanasheria kuwataka wapinge uamuzi wa kuondolewa eneo hilo, ni kuwachonganisha na Serikali yao, hivyo kuwataka wakazi hao kutumia akili zao.

Awali, Mtendaji Mkuu wa Dart, Cosmas Takule, alisema kufikiwa kwa maafikiano hayo kumeongeza hatua moja kubwa katika ujenzi wa mradi huo unaotarajiwa kugharimu zaidi ya Sh bilioni 400.

Takule alisema makubaliano hayo yatawezesha ujenzi wa kituo kikubwa katika eneo hilo pamoja na kituo cha mawasiliano kwa ajili ya mfumo wa kuongozea vyombo vya usafiri.

Alisema ujenzi wa awamu ya kwanza unaoendelea unatarajia kukamilika ifikapo Februari mwaka 2014.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya Wakazi hao, Rogert Kaniki, mbali na kuishukuru Serikali kwa kufanikisha suala la fidia yao, pia amewataka wenzake kutokubali kudanganyika na watu wa pembeni.

HabariLeo | Mradi wa mabasi, wananchi wakubaliana fidia
 
Mradi huo unafadhiliwa na nani? Serikali au ni msaada?

Nia aibu kujisifia kwa kitu ambacho mwanaume mwenzako akikasirika mradi upo mashakani.
 
hongera zeeetu sisi ccm ila kuna meri kama 4 tumkumbushe raisi asisahau mkuu!
 
Mradi huo unafadhiliwa na nani? Serikali au ni msaada?

Nia aibu kujisifia kwa kitu ambacho mwanaume mwenzako akikasirika mradi upo mashakani.

Ni sera nzuri na zinazotekelezeka tu huvutia wawekezaji mkuu, hata US kuna wawekezaji wa kichina.
 
isije ikawa ile hadithi ya uwanja wa ndege songwe mbeya toka 2003 unajengwa tu ..jana niliangalia jirani zetu kenya wamezinduwa train za nairobi city na bara bara za njia 6 .
umeme wa uhakika hakuna kama upo bei kubwa hao wawekezaji wata wekezaje?
 
Back
Top Bottom